Biashara ya waste engine oil (oil chafu)

Abuhunna

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
405
228
Wadau naomba kuelimishwa, sikuhizi kumezuka biashara ya ukusanyaji wa oil chafu katika mikokoteni, yaani kuna vijana hutembea sehemu mbalimbali hususan magereji wakiwa na mikokoteni yenye madumu ambayo hununua oil iliyotumika kutoka katika mitambo mbalimnali, swali langu kwa wadau, je oil hiyo inafanyiwa nini?
 
Inatumika katika shughuli mbali mbali, mojawapo kuulia mazalia ya mbu
 
Aaah! Hiyo kitu acha tu, Ni deal kama (sio vizuri kuwataja hawa watu coz wako vulnearble).

Mchina anaitumia kama mali ghafi. Inakuwa recycled ili nyie mnaopenda vya bei rahisi muuziwe muweke kwenye magari yenu. Wakati wengine tukinunua oil ya BP, Ile premium lita sh elfu kumi, nyie mtakuwa mnauziwa hii kwa lita sh elfu mbili.

Bac mnaona mmepiga bao, kumbe mmeuziwa oil mtumba. Alafu baada ya mda, magari yenu chali, mnaanza kulaumu, eti jirani flani aliazima gari juzi, ndio atakuwa ameliua!
 
Aaah! Hiyo kitu acha tu, Ni deal kama (sio vizuri kuwataja hawa watu coz wako vulnearble).
Mchina anaitumia kama mali ghafi. Inakuwa recycled ili nyie mnaopenda vya bei rahisi muuziwe muweke kwenye magari yenu. Wakati wengine tukinunua oil ya BP, Ile premium lita sh elfu kumi, nyie mtakuwa mnauziwa hii kwa lita sh elfu mbili. Bac mnaona mmepiga bao, kumbe mmeuziwa oil mtumba. Alafu baada ya mda, magari yenu chali, mnaanza kulaumu, eti jirani flani aliazima gari juzi, ndio atakuwa ameliua!

Hahahaaaa mkuu umenivunja mbavu, kwa hiyo wanawaona walonunua oil ya Sh 40,000 kwa galon wajinga kweli eeh ? Hahahaaa inaonekana huyo jirani ana nuksi sana hahahaaa
 
Wadau naomba kuelimishwa, sikuhizi kumezuka biashara ya ukusanyaji wa oil chafu katika mikokoteni, yaani kuna vijana hutembea sehemu mbalimbali hususan magereji wakiwa na mikokoteni yenye madumu ambayo hununua oil iliyotumika kutoka katika mitambo mbalimnali, swali langu kwa wadau, je oil hiyo inafanyiwa nini?

lnachemshwa na kuchanganywa na omo kisha hujazwa kwenye madumu au mapipa na kuuzwa tena
 
Inatibu kabisa tatizo sugu la upungufu wa nguvu za kiume kwa kuchanganya na mkojo wa paka nusu kijiko cha chai na kunywewa mara 2 kwa siku..
 
Kwenye maeneo yenye nyoka ukimwaga oil chafu wanahama kabisa, inasemekana kuwa nyoka hudhurika wakigusana na hayo mafuta
 
Oil chafu. Kama jina lilivyo ni oil iliyokwisha tumika huwa inakuwa nyeusiiii ila naona inanunuliwa tena kwenye ma garage huwa inapelekwa wapi kwa kazi gani? Nackia kuna watoto wa mjini huifanyia mambo yao na huigeuza kuwa kama mpya je kuna ukweli juu ya hili? Haiathiri chombo kama ni kweli?
 
Usemayo yote ni Kweli..hata huku mtaani kwetu WAPO
Nijuavyo mimi ni kwamba oil chafu hutumika kwa kazi hizi

1. Kupakwa kwenye mbao hasa za kupigia paa kuzuia mchwa na wadudu wala mbao na hii ndio kazi kubwa.

2.hutumika kumwagia kwenye vyoo vyenye harufu chafu hasa vya shimo ili kupunguza harufu.

3. Kina mama hupenda kutumia kusafishia nyumba kwani baada ya kusafisha nyumba hungaa sana hasa nyumba zenye flour ya cement chini na sio marumaru.

4. hutumika kwenye nguzo/ mistimu humwagiwa chini pale ili kuzuia mchwa
5. Hutumiwa kuwekwa kwenye miti ya mtunda au miti ya fance kuzuia miti hiyo kuliwa na mchwa na kusababisha miti hiyo kukauka

Hivyo baada ya kuonekana kuwa oil chafu imepata matimizi muhimu hasa hilo la mbao za ujenzi ndipo ilipo anza kuuzwa na kuwa dili lakin zamani ilikuwa ina mwagwa tu bila kujali
 
Kwa matumizi ya mtindo huu ndio maana wapiga nyoka hawatokaa waishe mjini
gari likisimama tu , wao washa piga spana ili wanyonye nyoka.

Nijuavyo mimi ni kwamba oil chafu hutumika kwa kazi hizi
1. Kupakwa kwenye mbao hasa za kupigia paa kuzuia mchwa na wadudu wala mbao na hii ndio kazi kubwa
2.hutumika kumwagia kwenye vyoo vyenye harufu chafu hasa vya shimo ili kupunguza harufu
3. Kina mama hupenda kutumia kusafishia nyumba kwani baada ya kusafisha nyumba hungaa sana hasa nyumba zenye flour ya cement chini na sio marumaru
4. hutumika kwenye nguzo/ mistimu humwagiwa chini pale ili kuzuia mchwa
5. Hutumiwa kuwekwa kwenye miti ya mtunda au miti ya fance kuzuia miti hiyo kuliwa na mchwa na kusababisha miti hiyo kukauka

Hivyo baada ya kuonekana kuwa oil chafu imepata matimizi muhimu hasa hilo la mbao za ujenzi ndipo ilipo anza kuuzwa na kuwa dili lakin zamani ilikuwa ina mwagwa tu bila kujali
 
Why ujauliza ukifua taulo maji yanakua meusi kwanin lakin hayo hayo badae unaenda ku flashia choo
 
Oil chafu. Kama jina lilivyo ni oil iliyokwisha tumika huwa inakuwa nyeusiiii ila naona inanunuliwa tena kwenye ma garage huwa inapelekwa wapi kwa kazi gani? Nackia kuna watoto wa mjini huifanyia mambo yao na huigeuza kuwa kama mpya je kuna ukweli juu ya hili? Haiathiri chombo kama ni kweli?
hapana mkuu nijuavyo mm ni kuwa hiyo oil chafu hupelekwa viwandani na huwa inatumika hasa kwenye viwanda vya chuma kama nondo hutumika kwaajili ya kukipa uimara. au huwa wanapoozea vyuma au nondo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom