Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,304
- 12,965
Biashara ya vyombo vya habari kama magazeti, redio na televisheni kwa sasa ina yumba kutokana na uendeshaji wa Vyombo hivyo ambao una walazimisha wamiliki kutoa au kuegemea upande mmoja wakati huko wanako egemea hakuna ruzuku wanayo pata ili kuendesha vyombo hivyo.
Kwa sasa kundi kubwa la wasomaji wa magazeti hali nunui tena magazeti badala yake wana tegemea mitandao ya kijamii. Hali kadhalika wengi hawategemei redio na TV za ndani kupata balanced story badala yake wanategemea vya nje kama DW na BBC. Kwa mtindo huo vyombo vingi vina kosa wasikilizaji wa habari na kwa hiyo kukosa mapato. Kwa sasa vyombo vyenye uhakika wa maisha ni vile vya chama tawala na serikali tu ambavyo hata vikikosea haviadhibiwi lakini wenzangu na mimi tia maji tia maji hali ni ngumu na wakati huo huo pingu ziko mlangoni zina wangoja mfanye kakosa kadogo tu nje ya kusifia.
Hali ilivyo sasa ni kuwa gazeti, redio na TV vina weza kufungiwa au kufutwa bila kupewa nafasi ya kujitetea kwa kuwa mlalamikaji ndiye polisi, hakimu na gereza pia. Poleni sana wamiliki wa Vyombo vya Habari