Naomba ushauri biashara ya kusajili laini na kuuza vocha

Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
2,896
4,495
Wakuu natumaini mu wazima,

Nina mpango wa kuanza kuuza vocha za jumla za mitandao ya Tigo na Vodacom, naomba kujuzwa ni wapi naweza kuzipata na pia kwa lolote linalohusiana na hii biashara karibuni tujadili.

Asante
 
Mkuu mi niko musoma watu wanaouza vocha za jumla wanapesa noma sasa sifahamu kama zinatokana na vocha tu au kuna kingine ila jaribu uone
 
Unajua kwanza kuna wale Super Dealers,ambao wanamitaji mikubwa si chini ya 50m kwenda mbele.
Hawa wanatambuliwa na Makampuni ya sim,sasa ili wewe uweze kuuza ni lazima upitie kwao wao ndio wakuuzie.
Sasa we nenda Ofisi ya Voda mkoa au unapoishi kisha wao watakuambia kwamba Super Dealer ni nani ili wakuunganishe ufanyenae kazi.
Hii niliwahi kuuliza miaka kama 6 iliyopita sijui kama wamebadilisha utaratibu.
 
Me mwenywe nataka kuifanya hyo biashara ya kuuza vocha za jumla but cjui wap pa kuanJia
 
hii biashara inakupasa uwe na pesa ya maana jamaa iwapo unapouzia kuna mzunguko mkumbwa usije ukawa una m.2 ukaanza kuiwazia....epuka kuzinunua mtani kwa watu wasioeleweka utauziwa mzigo feki....huwa kuna madealer wakubwa wanaonunua mzigo mkubwa zaidi i.e kanda ya ziwa kwa Airtel kuna Mega ltd na Freedom tel kwa Tgo voda fika voda shop iliyokaribu watakulink na wauzaji wakubwa/ma agent.
Vocha faida yake ni kubwa kama utakuwa unanua mzigo mkubwa kwa hao madealer sababu utaupata kwa bei pouwa na uwe na mzunguko mkubwa angalau uweze kuuuza m.10 kwa wiki moja
 
Kwanza kabisa heshima mbele kwa wote wakubwa na wadogo!

Wadau nataka kufanya biashara ya kuuza vocha za jumla & rejareja inatakiwa niwe na msingi wa bei gani na wapi pakuanzia asante.

Natumaini kuna wana JF wanafanya au wanajua hii biashara nahitaji kujua
 
best vocha za jumla zina hitaji mtaji mkubwa ili upate faida, japo unaweza kuanza na mtaji mdg kama ml 1.5 na ziikiisha zote faida yk haizidi sh elfu 20,000 piga ua galagaza.

labda kama unabiashara nyingine uchanganyie

ujiandae pia kukabiliana na changamoto za vibaka ñahata majambazi!!

zinapatikana pale fire nyuma ya sheli

nawakilisha tu
 
Habari!

Kama endapo mada kama hii ilishawahi kuzungumzwa humu ndani, basi mnisamehe na mnielekeze ili nikasome hizo post zilizopita. Lakini kama hutojali naomba kujua machache juu biashara ya kuuza vocha? nafahamu faida yake ni ndogo, lakini kwangu haina shida maadamu nimeshaamua kuanzia ujasiriamali kupitia biashara hii.

Kwa wale mnaoijua biashara hii kwa namna yoyote ile, tafadhali nishaurini lolote, je ni nzuri? au mtandao gani ni bora zaidi kuuza vocha zake? nahitaji ushauri wenu please, maana nilikuwa nawaza tu lakini sasa nimeamua kuifanya.

Nimeamua nianze na kununua tigo za 500 pisi (10) na 1000 pisi (10) + voda za 1000 na 500 pisi 10 kila moja. jinsi nitakavyouza, nimepanga kuwa nazo kidogo hapa ninapofanyia shughuli zangu, na zingine nitampa rafiki yupo mahala field na zingine nitamuachia mdogo wangu fulani yeye kwasasa yupo nyumbani tu, hivyo ataniuzia huko nyumbani. Wadau je niache au nitapoteza muda tu, wazoefu wa hii biashara ushauri wenu please. Baada ya ushauri naweza nunua hizo vocha hata leo jioni hii.

Tafadhali kama huna chochote cha kunishauri acha wengine watoe yao. Nipo tayari kushaurika

Karibuni.
 
Hakuna Biashara Mbaya inategemea na Location yako na Mahitaji ya sehemu husika, sababu umeshajua margins ni kiasi gani basi kilichobaki ni wewe kujaribu kuona wateja sehemu ulipo wakoje na kazi ya mzigo kutoka. Mimi naweza kuuza ICE (Barafu) ni vigumu ila kumbe nipo kwa Eskimos wakati mtu aliyopo jangwa la sahara hii inaweza ikawa Hot Cake...

Kwa ushauri kama mtaji unao na unaona hizo margins sio mbaya tafuta hizi Paypoints (Selcom, Maxmalipo et al..) hapa hautasumbuka kuwa na stock ya vocha utakuwa unauza vocha ya aina yoyote na denomination yoyote mteja anayotaka..

Ila kwa ushauri wangu usinfanye hii kama biashara pekee bali biashara ya ziada wakati unauza na vitu vingine
 
Mkuu asante kwa ushauri mzuri, hii nimechukua kama shughuli ya ziada tu, ili niweze fikia malengo yangu. Samahani hizo paypoints, sijakupata vizuri unanishauri nikawuzie huko au nikaweke hapo vocha zangu, samahani nahisi sijakuelewa sawia ktk hili?
 
Niliposema hii iwe ni kitu cha ziada kuuza nilimaanisha kama ni kibanda usiuze vocha peke yake unaweza kuweka pipi, magazeti, na bidhaa nyingine...

Kuhusu paypoint kuna vile vifaa kama Selcom ambacho wewe unachofanya ni kujaza balance tu, na unaweza kuuza vocha zote na LUKU hii itakusaidia sana kama akija mtu wa kununua vocha ya elfu kumi, au mia mbili au elfu tano na wewe unazo za mia tano peke yake.., yaani mtu unampa vocha yoyote atakayotaka yenyewe inarushwa direct kwenye simu yake
 
Asante sana, nitaifanya hii biashara kama nilivyopanga naamini lengo langu litatimia.
 
Niliwahi kusikia kuwa voucher moja faida yake ni sh. 50 (stand to be corrected).

Kwa maana hiyo, endapo kwa siku ukauza voucher za mia tano mia tano 100 utapata faida ya sh. 5000 kwa siku ambayo ni sawa na sh. laki moja na nusu kwa mwezi.

Kwahyo itategemea zaidi malengo yako.
 
Ni kweli mkuu, nimenunua naanza naamini nitafikia lengo tu
 
mdogomdogo ndio mwendo

Umejuaje mkuuu, yani vocha zinaenda mkuu na amini mambo yatakua mazuri zaidi, ile kuwaambia watu nyumbani, majirani wote wakasema afadhali umetusaidia maana duka lile liko mbali, (si kwamba duka liko mbali sana, kawaida tu, ila duka la karibu zaidi na home haliuzi vocha. - kwasasa natafuta uwezekano wa kupata kibanda kikae eneo la karibu na chuo, nijiongeze.
 
Back
Top Bottom