Ushauri kuhusu biashara ya kuuza vinywaji vya aina zote (Vikali na vya kawaida)

Wakuu, habari za Jumapili.
Ningependa kujua zaidi kuhusu biashara hii kwa wazoefu, nahitaji kuifanya biashara hii sehem ya mjini. Kuuza vinywaji baridi tu:
-Soda aina zote (chupa na take away)
-Maji
-Juice
-Tanga Fresh - Mtindi.
Ningependa kujua zaidi kwa bei za jumla vinapatikanaje na mchanganuo wa faida zake.
Kwa wale wazoefu.
Ahsanteni.
 
Habari wakuu

Ninafikiria kuanzisha biashara ya vinywaji vya jumla (Soft Drinks) hapa Tabata kinyerezi Dar Es Salaam na kwa kuanza nataka kuanza na maji ya kunywa ya jumla. Sasa kama ilivyo kwa biashara zingine, ningependa nipate ushauri na maoni kutoka kwa wadau wa ujasiriamali na hasa wale wenye uzoefu wa biashara hii kuhusiana na changamoto za biashara hii.Ahsanteni
 
Habari wana JF,

Naomba nisaidiwe namna ya kuwa distributor/agent wa vinywaji laini kutoka Kwenye kampuni za bonite, Pepsi, Azam, Mo n.k nataka kuanza biashara ya vinywaji vya jumla.
 
Hongera mkuu kuwa specific Usaidiwe kivipi?

Kama mtaji unao, frame unayo,vitendea kazi baadhi vipi fika ofisini kwao utapata majibu mazuri zaidi. Ni vizuri wakukute umeshaanza kuuza.

Na huu msimu wa mavuno sherehe zipo nyigi jisogeze sana kwenye kamati za harusi,send off ili uwe unapata tenda ya kupeleka vinywaji.pia usicheze mbali na misiba.

Yote kwa yote ukihitaji kijana wa kukusaidia kazi zako nipo hapa mkuu
 
Nashukuru mkuu kikubwa pia nlitaka kujua kama naweza kufanya nao biashara ya Mali kauli kama nikisimama vizuri
Hongera mkuu kuwa specific Usaidiwe kivipi ?

Lazima ufanye nao kwanza kazi tena kwa uaminifu mkubwa na viwango vyake mtaji ukishakua mkubwa wanakua wanakuletea mzigo wenyewe wanaacha hapo unauza
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom