Biashara ya vipuri vya pikipiki: Ushauri, michango, mawazo

Ila kwanza haujasema upo maeneo gani na ni pikipiki gani kwanza zinapatikana maeneo hayo maana kuna baadhi ya pikipiki vifaa vyake ni ghali na nyingine vifaa vyake ni rahisi kidogo
Maeneo ya Kisarawe,
Pikipiki nyingi ni Sanlg na Boxer kiasi fulani.
 
Nikipata hela nitafungua duka la kuuza bia na vinywaji vikali vya jumla ndani ya mwaka mmoja, naachana nayo naenda kununua gorofa upanga naishi humu maisha yangu yote yaliyo baki hapa duniani.....
Hizi biashara siku hizi kila mtu anafanya halafu wateja wamepungua sana. Viroba vilikua na faida sana mkuu. Pombe za chupa na wine hazitoki sana. Niliwahi fungua pale mbagala nikaumia
 
Maeneo ya Kisarawe,
Pikipiki nyingi ni Sanlg na Boxer kiasi fulani.
Ok sawa ila chamsingi ni uzingatie eneo utakalofungua awepo fundi maana wateja wengi hawapendi kununua vifaa sehemu tofauti na wanapotengenezea labda iwe ni spare ambayo haipatikani hapo kwenye fundi, pia spare za boxer zipo juu kidogo kwa bei ila unaweza kuanza na vile vifaa vidogo vidogo ambavyo mara nyingi ndio vinaharibika mapema, unaanza kidogo kidogo mpaka unajaza vitu vyote
 
Ha ha ha ha ha laki nane??? .....utani huu hapo baba huna mtaji kabisaaa nimeuza sana spea za pikipiki my dady ndo biashara yake mtaji wake sio wa kitoto kajipange upya angalau ungesema una million tatu kidoogo ungeanza sio laki
 
Mkuu,
Nimekuelewa, nitadunduliza mtaji mkuu.
 
Inabidi ujipange zaidi kuhusu mtaji maana laki hiyo laki 8 ni kidogo sana ukiangalia na kodi unayotakiwa kulipa kila mwezi.
Kwa vifaa vidogo vidogo na vinavyotoka labda uanze na cable aina zote na indicators pamoja na breaks zote na oil pia uwe na fundi hapo hapo.
Ungeanza na hivyo kwanza maana hiyo hela haitoshi kabisa kwa hiyo biashara.
Kila la kheri
 
Mkuu umeshauri vema, Ila ungenisaidia makadirio ya kiasi cha chini cha kuanzia angalau kiasi gani?

Pango usiihesabie kwani nimeshailipia.
 
Ndugu yangu Udochi idea yako ni nzuri tu wala haina mashaka na kwa vile tayari umeshapanga fremu hapo ndio tunasema maji umeshayavulia nguo. Biashara hii kwa kweli ina siri kubwa (mimi sifanyi) kwanza kabisa unatakiwa kujua kwamba sisi wa Tz ni price sensitive sana, tunajali sana bei ya kitu husika. Mtu anaweza acha kununua kitu Gongolamboto akaenda kununua kariakoo kwa tofauti ya elfu moja tu. Gongolamboto kinauzwa elfu 6 kariakoo elfu 5. sasa weka picha vifaa vya pikipiki na kwa jinsi hao watu wanavyozurura dar yote. Kwa hio first approach tafuta mchina bei chee na utauza zaidi na kwa hio pesa uliyonayo unaweza kupata mzigo kidogo mkubwa, halafu tafuta vifaa ambavyo ni hot cake ambavyo vinauzika fasta kwa mfano plagi, wazo la kuwa na fundi pembeni sio baya lakini mimi kwa kuanzia nisingependa ufanye hivyo, unamleta fundi hapo wakati tayari umeweka mzigo kwenye frame umetuila, ila cha kufanya mtafute tu fundi akupe idea (fundi na sio dereva) ikiwezekana mlipe kidogo kwa information atakaokupa. Kwa kukusaidia mtafute mtu anaitwa gkileo wa hapa hapa JF namba yake ya simu ni 0658131333. atakusaidia
 
Huyo gkileo si ndiyo wewe!!
 
ahahaha broo cheguevara gkileo sio mimi kaka. Unajua hizi nyuzi za watu kutaka kufanya biashara hizi na zile sio ngeni hapa jf, mwaka 2010 kama sikosei kuna mtu alileta hio nyuzi na huyo jamaa gkileo akajitokeza kusaidia kama sikosei ako na duka kariakoo huyo. Mimi sipo Africa kaka.
 
Mkuu umeshauri vema, Ila ungenisaidia makadirio ya kiasi cha chini cha kuanzia angalau kiasi gani?

Pango usiihesabie kwani nimeshailipia.
10m ni vizuri kuanzia lakini kama utaweza kupata au kiasi unatafuta fanya biashara nyingine kwa mtaji huo
 
Asaalam wanabodi! Kwa kipindi cha muda sasa nimefanya ufuatiliaji/uchambuzi juu ya biashara ya vipuri vya pikipiki(motorcycle spare parts) kwa mujibu wa matokeo na maelezo kwa baadhi ya wahusika kwa namna moja ni biashara inayokuwa kwa kasi na inalipa.

Kwa matokeo hayo nimeshawishika kwa kiasi kikubwa kuanza biashara hiyo kwa moyo mmoja.
Ufahamu naotaka kupata namna bora ya kuendesha biashara husika pamoja na maduka ya bidhaa hizo kwa bei ya jumla katika Jiji la Dar es Salaam.
Mimi ni mkazi wa Jiji la Arusha na biashara husika natarajia kuifungua Arusha.

Mungu awabariki sanaaa
 
mm naifanya biashara hii na niko arusha pia , nikushauri kitu kimoja, hii biashara bila kuwa na fundi mzuri hapo nje ya duka lako huwezi pata wateja, bidhaa nimenunua hapa hapa arusha kuna maduka ya jumla ya wachina meneo ya posta,
 
Oooh nitakucheki unisaidie ushauri zaidi. Asante sana
 
Hii biashara ikoje?

Faida yake ikoje? Faida unaweza kupata hata sh. 10000 kwa baadhi ya bidhaa?

Hasara zikoje juu ya biashara hii. MAANA NASIKIA BIASHARA HII INALIPA MNO.

MWENYE KUJUA ATUJUZE JAMANI
 
Muone mshana Jr akupe msukule ndo italipa mkuu
 
Back
Top Bottom