bitimkongwe
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 7,323
- 6,716
Kulalamika peke yake hakusaidii, kuchukua hatua ndiyo kutakupeleka mbele.Nani mwenye hiyo teknolojia bongo hii? Wakulima kila siku wanalalamika unadhani hawajui hizo ngonjera za teknolojia?
Shida ya kilimo cha kwetu, kwanza vijana hawapendi kujishughulisha na kazi hiyo, imebakia ya wazee huko vijijini. Unataarajia utapata maendeleo yo yote?
Pili, hapa kwetu kila mtu ni mtaalamu wa kilimo, yaani ukichoka maisha tu unakwenda kwenye kilimo. Hiyo siyo sawa. Kilimo ni taaluma kama kazi nyingine.
Angalia hata vijana wachache wanaofanya kazi ya kilimo (ya uhakika) uone mafanikio yao.