ni ngumu
JF-Expert Member
- Sep 25, 2016
- 4,292
- 7,157
Pole sana mkuu! Ila mimi naona tu nikualert kuhusiana na ushauri walioutoa wadau hapo juu! Kuna mdau kakushauri kutumia daftari akimaanisha maybe unachanganya katika mahesabu yako, umemhakikishia kuwa huwa upo makini! Kuna mdau mwingine kakushauri uwe unaombea na kukemea sehemu yako ya kazi ili kuikabidhi katika ulinzi wa Mungu, ukamwambia sawa utafanya hivyo! Then kuna mwingine kakwambia weka na mkaa na ndimu kwenye droo au mfuko unamohifadhi fedha, naye pia ukasema sawa utajaribu kufanya hivyo!......Ok umefanya vizuri kwa kuwa muungwana wa kupokea kila ushauri! Sasa na mimi nakushauri kwamba, ukiamua kujikabidhi kwa Mungu kwa imani ya dhati kabisa, basi usijichanganye na nguvu za aina nyingine kwani utafanya nguvu ya Mungu ijitoe kwako! Mfano kama umeamua kuweka mkaa na Limau, Hata ukiomba ulinzi wa Mungu hapo ni kazi bure manake utakuwa unalinganisha nguvu ya Mungu aliyekuumba wewe na wewe ukalima limau na kuchoma mkaa, alafu unamlinganishana nguvu ya Limau na mkaa! Hapa simaanishi kuwa napingana na wadau waliotoa ushauri wa kutumia ndimu na mkaa, bali natahadharisha mazingira ambamo nguvu ya Mungu huwa inafanya kazi na mle ambamo Mungu hawezi kujichanganya hata kwa kumchanganya! Ukiweka ndimu na mkaa basi amini katika hivyo na ukijikabidhi kwa Mungu, amini katika yeye tu!
Mkaa unatengenezwa na mti,Je miti kaumba nani???
Mti unaotoa malimao umeumbwa na nani?
Hivi mnajua huko kanisani kuna vitu mnadanganyana ambavyo Mungu hajawahi kabisa kuviita uchawi??
Hivi miti aliyoumba Mungu kwa ajili ya kumkinga mtu na nguvu za kichawi nayo mnaiita uchawi???unadhani kwanini Mungu ameumba miti hii na kwanini kaipa nguvu ya kupingana na nguvu za giza?ina lengo gani?inasaidia kwa watu wake?think think think
Achenk kukalili jamani hapo mkifika kanisani mnapewa vitambaa vya upako mara mafuta ya upako lakini limao tu kwenye sehemu ya hela for good purpose tayari uchawi....