Biashara ya uwakala M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money

Hio biashara iliingiliwa mdudu ilivyoanza kupigwa kodi za ajabu 😁 ndio kipindi ambacho line ziliuzwa kwa kasi sana hapa nchini. Kila upande unasikia flani anauza line ya M-PESA mara kule flani anauza line ya TIGOPESA watu waliuziana sana line. Biashara ilikuwa ndio imeishia pale walipoanza kuminya commission!

Zamani commission line moja tu kabla watu hawajawa wengi watu walikuwa wanafungasha laki 5-7 ukiwa nazo mbili una uhakika wa 1.4-1.6M ila toka ujinga ukikusanya 150K ujue we mwanaume na kazi kweli umepiga 😂😂😂
Duuuh🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Habari ndugu zangu naomba muongozo mwenye hakika na haya anijuze.

Nawaza kufungua ofisi ndogo ya kuwa wakala wa hudumu za kifedha kupitia mitandao ya simu,

Je, leseni ya biashara inapatikana kwa gharama kiasi gani (Mimi nipo mwanza sijawai miliki hiyo kitu ndo nata kuifuatilia Kisha nisajiri lain izo)

Je, ni faida kiasi gani naweza ingiza kwa mwezi endapo kwa siku nitafanya miamala isiyopungua 500,000 laki tano yaani sawa na 15M kwa mwezi?

Asanteni nasubiria miongozo yenu.
Hivi hii biashara bado inalipa kama zamani?
 
Back
Top Bottom