Biashara ya utumwa mamboleo: Mbinu inayotumiwa ni kufumbia macho wahamiaji haramu!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
6,952
2,000
Dunia imestushwa na biashara haramu ya binadamu huko Libya. lakini ukweli ni kuwa utumwa upo sana huko Marekani na ulaya! Mbinu inayotumika ni kufumbia macho wahamiaji haramu.

Kila mhamiaji haramu huchunguzwa sana, wakijiridhisha kuwa hana madhara kwa kwa nchi yao, wanaamua kumwacha na kumtumikisha kwa ujira duni na kwa kazi zisizo na hadhi.

Hii pia huwakumba wanafunzi wanapomaliza masomo yao na kuamua kubaki huko kutafuta maisha. Hufanyishwa kazi mahotelini kunyonyoa Kuku na kufanya usafi!

Kazi nyingine huwa ni kuwahudumia na kuwaogesha vikongwe kwenye makazi yao kwa ujira duni sana!

Ukilalamika unatishiwa kukamatwa kwa kuwa ni mhamiaji haramu! Kuna maelfu ya watumwa wa jinsi hiyo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom