Biashara ya utalii

aspen

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
501
165
Wadau naomba kuuliza kuhusu hii biashara changamoto zake ni kuhusu kupeleka wageni porini na milimani na ni gari gani linafaa zaidi kati ya landcruiser na landrovers na mtaji wa kuanzia nataka niache na gari moja kwanza natangulisha shukhrani
 
Mkuu si kwamba nakukatisha tamaa, Ila hii biashara ni ngumu kuliko, ingawa hakuna biashara rahisi wala ngumu, ila kwa hii kuna utofauti kidogo na sababu kubwa ni hii

1. Umonopoly unaofanywa na kampuni kubwa

2. Pesa

3. Mtandao

- Makampuni mengi na makubwa ni ya wazungu na wahindi, na wana mitaji mikubwa balaa na wana Maagent huku Majuu mfano Marekani, Ulaya na Asia, so wao kupata watalii si ishu kwa sababu wana ofisi huku huko majuu na ukijumlisha na mitaji yao ilivyo mikubwa ndo maana wana weza kumonopolaize soko,

- Kwa kampuni za wazawa ni chache sana zinazo fanya vizuri na kwa Arusha na Moshi hata sita hazifiki, nyingi za kampuni za wazawa zinasubiria wale wageni walio jijia wenyewe ndo wanawakamata hao, au wale choka mbaya kutoka huko,

- Na tambua kwamba hata kataika watalii kuna Madaraja, kuna wale wenye pesa na kuana ambao hawa tofauti sana na wabongo, Mfano watalii kutoka USA, CANADA hao ndo wenye pesa na ni kampuni chache zinazo weza kuwapata hao na hata gharama za kukodisha magari kwa hao ziko juu balaa

PROPAGANDA
- Hii ishu niliwahi kuambiwa kwamba kampuni nyingi za Wazungu zilizoko huku huwa zinafanya propaganda ya kuwaaminisha watalii kwamba kampuni za wabongo haziamnini na zinazo aminika ni za kwao tu


So mkuu ili ufanikiwe ni lazima uwe na wazungu huko juu tena wazungu wa maana, la sivyo utaishia kuvizia wazungu walio kuja na Mabasi kutoka Nairobi kenya ambao unakuta ni choka Mbaya tu na ni mabairi sana,

Na unaweza cheki nyanja zingine za utalii, mfano cultre tourism kidogo haina mizengwe sana,
 
thanks mkuu nimekuelewa vipi je na ukiwa na gari la kukodisha means unafanya kazi za kukodiwa
 
thanks mkuu nimekuelewa vipi je na ukiwa na gari la kukodisha means unafanya kazi za kukodiwa

Nayo ni shida tupu, make saazingine ukipiga faida unajikuta una hasara make unakodishwa poa unapewa pesa ya Mafuta lakini gari ikharibika unatengeneza kwa pesa yako, na hizi barabara za huko Mbugani ukienda ukirudi ni Service labda gari liwe jipya ila kama ni lazamani ni service kila safari,

Na ni wakati wa high season tu ndo unapata kazi baada ya hapo hakuna kazi inabidi uwe unetembelea mtaani
 
Tuje kwenye mtaji sasa ukiwa na kama 20M zinaweza tosha kwa kuanzia I mean gari moja
 
thanks mkuu nimekuelewa vipi je na ukiwa na gari la kukodisha means unafanya kazi za kukodiwa

Mkuu kama hauko kwy hii industry sikushauri kabisa ununue gari za porini labda van kwa ajili ya aiport transfer na mlimani mfano,Marangu gate,Machame,Momella na kwingineko,natofautiana kidogo na mdau hapo juu aliyesema kua kampuni za wazawa hazifiki 6,kwa uelewa wangu ziko nyingi na zinafanya vizuri mfano Kilimanjaro crown tours,Zara tours,Key's,Tanganyika travel,African spoonbill,Kili climbers,SENE na nyingine nyingi na hzi ni za Moshi tu na wana agent ulaya na Marekani,kama unafanya kazi vizuri na reputation ikiwa poa utapata wageni tu na mtaji mkubwa ni uaminifu kwa sababu mgeni lazima atume pesa inadvance kulingana na package.
 
Binafsi niko kwenye utalii na ndio shughuli inayaniweka mjini hapa, kwa 20m kwanza huwez kupata gari ya kufanyia kaz ama ukipata itakuwa ni spana mkononi ambao huo ni utalii wa zamani sana... sasa basi kama unataka kuinvest kwenye hii sekta na hutaki kuhusika wewe tafuta gari yako nzuri either cruser ama land rover iliyoko kwenye hali nzuri then kodishia kampuni yoyote watakulipa vizuri tu coz kampuni uliyoikodishia gari lako watakuwa responsible na service ya hilo gari coz wanalitumia wao... so utakuwa anamake money ukiwa sebleni kwako

Nadhani umenipata...
 
Binafsi niko kwenye utalii na ndio shughuli inayaniweka mjini hapa, kwa 20m kwanza huwez kupata gari ya kufanyia kaz ama ukipata itakuwa ni spana mkononi ambao huo ni utalii wa zamani sana... sasa basi kama unataka kuinvest kwenye hii sekta na hutaki kuhusika wewe tafuta gari yako nzuri either cruser ama land rover iliyoko kwenye hali nzuri then kodishia kampuni yoyote watakulipa vizuri tu coz kampuni uliyoikodishia gari lako watakuwa responsible na service ya hilo gari coz wanalitumia wao... so utakuwa anamake money ukiwa sebleni kwako

Nadhani umenipata...
Mkuu nimekupata lakini inalipaa ?
 
Hakuna biashara ambayo hailipi... sema kuna moja mbili ukiwa ndani ila kwa hii kama ukipata kampuni nzuri you will never regret hii nakuhakikishia...
Swala la kuanzisha kampuni ni mpaka uwe na agents wa ukweli ambao watakupa wageni ambao sio wa msimu na bei yao isiwe ya chini. ila ukisema ugangamale kibingo bongo huendi mahali...
 
hivi kuna msamaha wa kodi kwa makampuni ya tours kama wanataka kuingiza bidhaa toka nje kama magari kwa ajili ya kampuni?
 
Biashara ya tours inalipa kama una source ya kupata wageni. Kama una gari liweke kwenye mazingira ya ki-tours na umpe best guide awe freelace, atakodishwa na kampuni yoyote. Mwenyewe niko kwenye tourism industry mwaka wa 14 huu.
 
Back
Top Bottom