Ukweli ni upi?si kweli
Ukweli ni upi?si kweli
Nami naongezea kidogo kwa walichochangia wenzetu
1. Biashara ya usafirishaji (utangulizi)
Uzoefu nilionao ni katika kusafirisha mizigo ya nje ya nchi ie transit cargo kwa zaidi ya miaka 10. Ni biashara nzuri yenye faida kama utaiendesha kwa kufuata taratibu na mpangokazi sahihi. Njia nilizo na uzo
2. Mtaji
Ni kweli hii biashara inahitaji mtaji mkubwa kidogo kwani kuanzia vitendea kazi vyake ie malori ni gharama kubwa. Kwa mtaji unaosema wa mil 400 kweli unaweza kuanza na magari 3 na sehemu ya hela ukaigawanya katika gharama za kuanzia kama masuala ya usajili wa kampuni, vibali, kukodi eneo la gereji nk
3. Ununuzi wa magari
Suala hili limekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya watu niliopata kufanya nao kazi. Unakuta yeye anataka kununua lori aina fulani mfano scania r420 kwa sababu anaona kampuni fulani inayo. Tambua ile kampuni tayari ipo sokoni na ina mtandao wa kibiashara. Zingatia haya kabla ya kununua aina ya gari hilo
a) gharama za uendeshaji
Angalia masuala gharama za service, spea, uwezo wa madreva ulionao au utakaokuwa nao kumudu gari hilo
b) kianzio cha mtaji
Kama mtaji wako ni mkopo wa benki jitahidi kupata gari ambayo ipo katika kiwango cha juu sana ubora. Wengi kwa sasa tunakimbilia magari ya Kichina kwa sababu ya gharama za mwanzo za uendeshaji zipo chini ukilinganisha na gari za mtumba za Ulaya. Kama utakuwa na wateja na mzigo hivyo kuwa na mzunguko mzuri hadi zinaanza kusumbua tayari ushalipa pesa ya benki na we umenufaika
c) uwino wa matumizi ya mafuta
Mtaji wa biashara hii umelala katika mafuta na matairi. Jitahidi kuwa na lori lenye uwiano mzuri wa matumizi ya mafuta. Mathalani unaweza labda ukampa dreva lita 1200 kwenda Rwanda kwa Daf xf lakini umbali huohuo ukampa lita 1300 wa Scania r480 labda. Hiyo lita 100 inayoongezeka ujue ni gharama ya ziada kwako kwa sababu wote mnaenda kwa bei moja mfano $3000 n.k
4. Rasilimali watu
Tatizo jingine katika biashara hii ni kukuta mwenye gari ana mambo mawili ambayo either yeye ndiyo kila kitu au kajaza watu wasiofit katika uendeshaji hii biashara. Hii ina maana kwamba. Mwenye gari kuwa kila kitu maana yake yaani anaiendesha biashara hata kama ana fleet ya magari 5,10 nk sasa huwezi kazi zote wewe mwenyewe kudeal na tracking, kutafuta mizigo, kuhangaikia mizigo ya kurudi, vibali, uajiri nk. Tengeneza timu ya malengo. Wape mwongozo na nini malengo ya jumla ya kampuni yanatakiwa kufikiwa. Kuwa na timu ya watu wachache lakini yenye ufanisi. Epuka kujaza ndugu, jama na marafiki katika biashara. Hakikisha unakuwa na code of conduct kwa wote hasa madreva kwani ukimchekea dreva kila siku utapata hasara. Mara nyinyi husema kuwa na roho mbaya kwa kifupi
5. Mfumo wa uendeshaji wa biashara
Jitahidi magari kama ya ruti za transit kuwa na sifa za kuuzika kibiashara. Hii ina maana ya kwamba kupitia timu yako ya kazi hakikisha yanakuwa monitored ktk tracking, (gharama za tracking kwa gari 35,000Tzs kwa mwezi). Tengeneza gari kama ina tatizo, achana na kutengeneza gari barabarani. Usione lori lina dreva pekee kwa sababu kampuni ina uhakika wa uzima wa lori. Jenga tabia ya kuhakikisha gari linahudumiwa kwa kiwango sahihi.
6. Uombaji wa mizigo
Andika 'profile company' nzuri, baada ya hapo pita makampuni mbalimbali unaacha kitabu hicho na barua ya maombi. Usione aibu kuomba mzigo. Hii itakusaidia kuwa na uhakika wa mizigo kwani kampuni nyingi zikiona umeenda katika mfumo rasmi kama huu utapata mkataba na kipaumbele cha kupata mzigo. Mkataba unaweza kuwa wa myda mrefu au muda mfupi lakini tayari ushakuwa na uhakika wa mizigo na mzunguko wa uhakika.
NITAENDELEAA......!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naweza kukuonaINAENDELEA
Habari zenu, pili nawatakia sikukuu njema ya Eid el haj!
7. Kudhibiti na kuthibitisha gharama za kuiendesha biashara
Kumekuwa na tatizo la kudhibiti na kuthibitisha gharama za uendeshaji wa biashara hii. Gharama hizo ni za safari ie trip expenses and business running expenses. Usifanye biashara hii kwa kusikia fulani huwapa kiasi fulani cha pesa na mafuta. Pata uzoefu toka kwako lakini fanya tafiti ya gari yako na weka mfumo wako katika gharama za safari. Hizi ni baadhi ya gharama amabazo unapata na risiti
1. Rwanda trip
Road toll $152, fuel 1200lts(daf xf), comesa/insurance $267 kwa mwaka, container fee $18, driver allowance depends with the company policy lkn utamsainisha dreva petty cash voucher.
2. Zambia trip
Road toll $356 (Tunduma lusaka Tunduma), road permit 290,000Tzs/3months, carbon tax 75,000Tzs/3months, insurance/comesa $267 per annum, agaent fee 20,000Tzs, city council 40,000Tzs, Zambia tax levy 240,000Tzs/annum
3. Lubumbashi, D. R Congo
Hapa gharama zinalipwa kwa kuongezeka mipaka ie Tz to Zambia border, Zambia to Congo border hivyo itakuwa hivi
a) Tunduma/Nakonde border
Road toll $356 kwa trip, road permit 290,000Tsh/3months, carbon tax 75,000Tsh/3months, Comesa/insurance 224,000/3months, city council 40,000Tsh/trip, na agent fee 20,000/trip kama una ajent wako wa kufuatilia na kupush documentation process. Suala la bond inategemea kulipwa na mwenye mzigo au gari kutokana na malipo mliyokubaliana na makubaliano yenu ambayo ni $100 au yaweza kuwa pungufu kidogo
b)Zambia border (kasumbalesa 1)
Entrance in &out fees $200, city council 40,000kwacha, agent fee $200
c) Congo border (kasumbalesa 2)
Peage $300, wisk $30, seal fee $10, kisanga in n out $60, Entry fees in n out $200, visa driver n tboy $100 km waruhusu wawili
Angalizo. Gharama hizi zinabadilika kutokana na kushuka na kupanda kwa dola na sera za nchi. Hivyo inatakiwa kila mara kuwa wafanya cross check. Kujua gharama hizi itakusaidia kujua unapeleka mzigo kwa faida au hasara
Pili ni gharama za kuiendesha biashara yenyewe. Hii ni gharama za jumla kuanzia ofisi na lori. Unaweza ukawa wafurahia kupeleka mzigo Rwanda kwa sababu ni ruti fupi hivyo kwenda hadi trip 4 kwa mwezi lakini gharama zikawa kubwa za wear & tear, service et za gari kuliko yule aendae Congo. Mtathmini dreva wako gharama zake kwako zipoje. Angalia mishahara ulipayo na kinachozalishwa na kufikia malengo vinaendana? Jitahidi ujue pesa yako halisi na halali baada ya kutoa gharama zoote ikiwa na service ambazo waweza kuzirekodi katika ledger books, trip expenses na office running expenses. Usije ukawa waona akaunt yako ina pesa nyingi kumbe yote si yako bali inapita tu mkononi mwako
8. Faida za hii biashara
Kiukweli biashara hii kama utapata malori sahihi, madreva sahihi, staff members sahihi na channel za mizigo utapata faida nzuri sana. Ndo maana unaona kuna makampuni yana magari hadi mia 800, na kuna watu gari zinazidi kuisha tu kutokana na miongoni mwa masuala yaliyochangiwa hapo juu
8. Hasara zake
Mtaji wake ni mkubwa sasa lori linapopata ajali na kama hujakata comprehensive insurance inakuwa ni hasara kubwa sana katika biashara
Kuibiwa kwa mzigo hasa mzigo wa kurudi kama vile shaba. Ule mzigo utalipwa na kampuni ya bima lakini inasumbua sana maana hapo tarajia changamoto ya usumbufu kuanzia watu wa dola na bima pia. Lakini vilevile inaharibu status quo ya kampuni kwani mteja wako tayari ataanza kuwa na shaka na mwenendo mzima wa kampuni
9. Changamoto zake
Zipo nyingi kama vile
a. Kufanya kazi na madreva wasio waaminifu hivyo kukupa hasara kwa kuiba mafuta
b. Kuyumba kwa upatikanaji wa mizigo kwa mfano Tanzania japo kwa sasa hali kidogo imeanza kuimarika
c. Kushuka kwa malipo
Malipo ya transit cargo yameshuka utaona kutoka $5000 hadi $3600 Zambia, Congo $7000 hadi $5500/5000 Congo et al wakati gharama za uendeshaji zipo palepale
d. Utitiri wa vibali
Vibali vingi na lazima ulipie ili uwe salama kuepuka faini mbalimbali.
Mwisho
Nimejitahidi kuweka mambo muhimu kwa kiasi chake na wengine waongezee kwani hii ni biashara pana sana. Vilevile naomba mniwie radhi kwa kuchanganya lugha mbili tofauti kutokana na nafasi finyu niliyonayo katika kuandika kwa utimilifu wake kwa lugha moja.
Nawasilisha!
Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu sanaMkuu naweza kukuona
Nnitakuita kwenye simu leo.Karibu sana
Ofisi zetu zipo Jengo la Mariam Tower, ghorofa ya nne, mtaa wa makutano ya Shaurimoyo na Lindi!
Simu:0659211222
Barua pepe: iconsultbuzness@gmail.com
Sawa MkuuNnitakuita kwenye simu leo