Biashara ya Usafirishaji wa Mizigo kwa Malori Makubwa: Jifunze Uzoefu, Miongozo, Faida na Changamoto Zake

Pitia hapa

https://www.jamiiforums.com/threads...ra-ya-usafirishaji-wa-abiria-kwa-basi.849209/

https://www.jamiiforums.com/threads...ara-ya-daladala-ni-vema-ukayajua-haya.691330/

 
Wadau nataka kuingia kwenye biashara hii naomba mnishauri.

Nina jamaa yangu ana tela ameahidi kunipa nifanyie kazi kama nikipata kichwa. Natamani kujua kama ninaweza kupata kichwa cha kukodi na kwa bei gani na biashara ikoje kwa ujumla.

Naomba kuwasilisha
Epuka madalali kwa hiyo biashara tuwaache kwenye nyumba na ununuaji wa bidhaa ila inalipa kibaya imetawaliwa na dhulma kupita kiasi ntarudi baadae
 
Modifications zipi manake kila kitu kuanzia engine, chassis,transmission system, breaking system, body specifications na juu yote manufacturer specifications ni za tani 4 na si tani 18?
Kuna watu vichwa ngumu
 
Habarini Wanajamvi.
Mimi ni kijana nina mtaji wa 70m natamani kuagiza fuso na kuja kuifanyia modification hapa ndani ya nchi (Tabata Dampo au Arusha) iwe tandam iweze kubeba tani 18. Sasa nauliza kwa wenye uzoefu na hiyo kazi, wanisaidie gharama za kufanya modification na ushauri kua biashara hiyo inalipa au vipi na pia wanipe changamoto zake
chukua scania 113 ufurahie maisha,ninazo nne zinanilipa sana,mafuso yanaua engine usishwishike na hizo modifications za kubeba mizigo mikubwa
 
Huyo mdogo wako akitaka kupata presha bado mdogo mwambie ajaribu!
Ni biashara kichaa hatari!
Unaweza fanikkiwa kama unafleet ya not less then 20 trucks na uwe na permanent tender!
Lasi ivyo lazma ataingia hadi kwenye uganga!
Wabongo bana
 
Mmmh its an impressive bussiness,,,unajua kila kitu kufanikiwa lazima uwe na nguzo yako kuu,ambayo ni either Mungu ama Shetani,,,ukiwa katikati especially in this bussiness no where you will reach,,,kukushauri,kwanza inabidi ufanye ujasiriamali na biashara tofauti ambazo zitakuweka on platform alafu ununue scania zako,,,kupitia biashara zako utapata jukwaa la kupata connections kirahisi,,ila ukiingia moja kwa moja no where you will go.
Duuh, akili za mswahili
 
Ni biashara nzuri sana. inahitaji uwe nayo karibu sana. ktk hiyo mia 4 uliyosema mimi naweza pata truck 4 na ziko vizuri sana. kikubwa ktk hii biashara uwe na mafundi wazuri. ambao hawabahatishi. uwe na store ya spear nk. uzuri wa biashara hii ni kwamba haihitaji matangazo kazi zilizopo ni nyingi sana. ukiwa na magari kazi utazipata tu japo zinapitia kwa wakala ( Agent) kufanya kazi na agent kuna unafuu mkubwa sababu yeye ndiyo anatafuta mzigo na kama mzigo ukipotea ukafanyaje sijui yeye ndiye analipa.
Pia kwa upande wa ajari bima wapo tafuta kampuni nzuri isiyo na longo longo mara nyingi kwa gari moja huwa ni 4.5 .5m kwa comprehensive.

Tengeneza communication system nzuri . nunua madereva wazuri . kaka utaende . nina rafiki yangu mwaka 2009 . alianza na truck 1. nilisindikiza kununua hapo kinondoni kisha akanunua trela toka mombasa. baada ya muda akaanza kuagiza mwnyewe.mwaka huu ana truck 7.

Anza kiongozi tupate ajira!.
Good good
 
Mhh , katika gari ambazo sizikubali kama zinarudisha pesa vizuri ni hayo mafuso tandam, modification ni nyingi mno na nasikia huwa hazikai sana na engine yake kutokana na mzigo mkubwa zinaobeba( by default fuso inabeba tani 4)
Kwa nini usifikirie semi kwa pesa unayotaka kuwekeza?
Habar mkuu. Kwa mtaji 70m inawezekana kupata scania 93 au 113 kipisi au semi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tandam unapoifanyia manuva ni lazima na mashine uibadilishe uweke kubwa yake.. pia tandam inataka sana kubembelezwa bora avute scania 94D 310 kipisi tani 15-18 uhakika wa maisha ni mkubwa kuliko tandam
Mbona mtaani Tandam namba A zipo kibao mkuu, nadhan n matunzo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu upo field kweli au we ndo upo kijiweni? Kwa taarifa yako scania kipisi ina maisha kuliko tandam,
Ni kweli tandam inapakia sana ila haidumu barabarani
Mkuu kama hutojali rudi hapa kidogo... Bado niko kwenye uchunguzi wangu huku nikiendelea kudunduliza

Mtaani huku, fuso tandam namba B na A naziona nyingi mno , inakuaje zinapata sifa ya kutodumu sana ila kuna kampuni wanazo namba A Kabisa, siri nyuma ya hili n nini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Danpol,
Scania na fuso zote zinadumu tofauti yao ni kwamba fuso inahitaji matengenezo ya mara kwa mara tofauti na scania.
 
Back
Top Bottom