Biashara ya Usafirishaji wa Mizigo kwa Malori Makubwa: Jifunze Uzoefu, Miongozo, Faida na Changamoto Zake

Jun 28, 2017
72
125
NAMNA YA KUENDESHA BIASHARA YA USAFISHAJI MIZIGO

Nami naongezea kidogo kwa walichochangia wenzetu

1. Biashara ya usafirishaji (utangulizi)
Uzoefu nilionao ni katika kusafirisha mizigo ya nje ya nchi ie transit cargo kwa zaidi ya miaka 10. Ni biashara nzuri yenye faida kama utaiendesha kwa kufuata taratibu na mpangokazi sahihi. Njia nilizo na uzo

2. Mtaji
Ni kweli hii biashara inahitaji mtaji mkubwa kidogo kwani kuanzia vitendea kazi vyake ie malori ni gharama kubwa. Kwa mtaji unaosema wa mil 400 kweli unaweza kuanza na magari 3 na sehemu ya hela ukaigawanya katika gharama za kuanzia kama masuala ya usajili wa kampuni, vibali, kukodi eneo la gereji nk

3. Ununuzi wa magari
Suala hili limekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya watu niliopata kufanya nao kazi. Unakuta yeye anataka kununua lori aina fulani mfano scania r420 kwa sababu anaona kampuni fulani inayo. Tambua ile kampuni tayari ipo sokoni na ina mtandao wa kibiashara. Zingatia haya kabla ya kununua aina ya gari hilo
a) Gharama za uendeshaji
Angalia masuala gharama za service, spea, uwezo wa madreva ulionao au utakaokuwa nao kumudu gari hilo
b) Kianzio cha mtaji
Kama mtaji wako ni mkopo wa benki jitahidi kupata gari ambayo ipo katika kiwango cha juu sana ubora. Wengi kwa sasa tunakimbilia magari ya Kichina kwa sababu ya gharama za mwanzo za uendeshaji zipo chini ukilinganisha na gari za mtumba za Ulaya. Kama utakuwa na wateja na mzigo hivyo kuwa na mzunguko mzuri hadi zinaanza kusumbua tayari ushalipa pesa ya benki na we umenufaika
c) Uwiano wa matumizi ya mafuta
Mtaji wa biashara hii umelala katika mafuta na matairi. Jitahidi kuwa na lori lenye uwiano mzuri wa matumizi ya mafuta. Mathalani unaweza labda ukampa dreva lita 1200 kwenda Rwanda kwa Daf xf lakini umbali huohuo ukampa lita 1300 wa Scania r480 labda. Hiyo lita 100 inayoongezeka ujue ni gharama ya ziada kwako kwa sababu wote mnaenda kwa bei moja mfano $3000 n.k

4. Rasilimali watu
Tatizo jingine katika biashara hii ni kukuta mwenye gari ana mambo mawili ambayo either yeye ndiyo kila kitu au kajaza watu wasiofit katika uendeshaji hii biashara. Hii ina maana kwamba. Mwenye gari kuwa kila kitu maana yake yaani anaiendesha biashara hata kama ana fleet ya magari 5,10 nk sasa huwezi kazi zote wewe mwenyewe kudeal na tracking, kutafuta mizigo, kuhangaikia mizigo ya kurudi, vibali, uajiri nk. Tengeneza timu ya malengo. Wape mwongozo na nini malengo ya jumla ya kampuni yanatakiwa kufikiwa. Kuwa na timu ya watu wachache lakini yenye ufanisi. Epuka kujaza ndugu, jama na marafiki katika biashara. Hakikisha unakuwa na code of conduct kwa wote hasa madreva kwani ukimchekea dreva kila siku utapata hasara. Mara nyinyi husema kuwa na roho mbaya kwa
kifupi

5. Mfumo wa uendeshaji wa biashara
Jitahidi magari kama ya ruti za transit kuwa na sifa za kuuzika kibiashara. Hii ina maana ya kwamba kupitia timu yako ya kazi hakikisha yanakuwa monitored ktk tracking, (gharama za tracking kwa gari 35,000Tzs kwa mwezi). Tengeneza gari kama ina tatizo, achana na kutengeneza gari barabarani. Usione lori lina dreva pekee kwa sababu kampuni ina uhakika wa uzima wa lori. Jenga tabia ya kuhakikisha gari linahudumiwa kwa kiwango sahihi.

6. Uombaji wa mizigo
Andika 'profile company' nzuri, baada ya hapo pita makampuni mbalimbali unaacha kitabu hicho na barua ya maombi. Usione aibu kuomba mzigo. Hii itakusaidia kuwa na uhakika wa mizigo kwani kampuni nyingi zikiona umeenda katika mfumo rasmi kama huu utapata mkataba na kipaumbele cha kupata mzigo. Mkataba unaweza kuwa wa myda mrefu au muda mfupi lakini tayari ushakuwa na uhakika wa mizigo na mzunguko wa uhakika.

NITAENDELEA!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jun 28, 2017
72
125
Nami naongezea kidogo kwa walichochangia wenzetu
1. Biashara ya usafirishaji (utangulizi)
Uzoefu nilionao ni katika kusafirisha mizigo ya nje ya nchi ie transit cargo kwa zaidi ya miaka 10. Ni biashara nzuri yenye faida kama utaiendesha kwa kufuata taratibu na mpangokazi sahihi. Njia nilizo na uzo
2. Mtaji
Ni kweli hii biashara inahitaji mtaji mkubwa kidogo kwani kuanzia vitendea kazi vyake ie malori ni gharama kubwa. Kwa mtaji unaosema wa mil 400 kweli unaweza kuanza na magari 3 na sehemu ya hela ukaigawanya katika gharama za kuanzia kama masuala ya usajili wa kampuni, vibali, kukodi eneo la gereji nk
3. Ununuzi wa magari
Suala hili limekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya watu niliopata kufanya nao kazi. Unakuta yeye anataka kununua lori aina fulani mfano scania r420 kwa sababu anaona kampuni fulani inayo. Tambua ile kampuni tayari ipo sokoni na ina mtandao wa kibiashara. Zingatia haya kabla ya kununua aina ya gari hilo
a) gharama za uendeshaji
Angalia masuala gharama za service, spea, uwezo wa madreva ulionao au utakaokuwa nao kumudu gari hilo
b) kianzio cha mtaji
Kama mtaji wako ni mkopo wa benki jitahidi kupata gari ambayo ipo katika kiwango cha juu sana ubora. Wengi kwa sasa tunakimbilia magari ya Kichina kwa sababu ya gharama za mwanzo za uendeshaji zipo chini ukilinganisha na gari za mtumba za Ulaya. Kama utakuwa na wateja na mzigo hivyo kuwa na mzunguko mzuri hadi zinaanza kusumbua tayari ushalipa pesa ya benki na we umenufaika
c) uwino wa matumizi ya mafuta
Mtaji wa biashara hii umelala katika mafuta na matairi. Jitahidi kuwa na lori lenye uwiano mzuri wa matumizi ya mafuta. Mathalani unaweza labda ukampa dreva lita 1200 kwenda Rwanda kwa Daf xf lakini umbali huohuo ukampa lita 1300 wa Scania r480 labda. Hiyo lita 100 inayoongezeka ujue ni gharama ya ziada kwako kwa sababu wote mnaenda kwa bei moja mfano $3000 n.k
4. Rasilimali watu
Tatizo jingine katika biashara hii ni kukuta mwenye gari ana mambo mawili ambayo either yeye ndiyo kila kitu au kajaza watu wasiofit katika uendeshaji hii biashara. Hii ina maana kwamba. Mwenye gari kuwa kila kitu maana yake yaani anaiendesha biashara hata kama ana fleet ya magari 5,10 nk sasa huwezi kazi zote wewe mwenyewe kudeal na tracking, kutafuta mizigo, kuhangaikia mizigo ya kurudi, vibali, uajiri nk. Tengeneza timu ya malengo. Wape mwongozo na nini malengo ya jumla ya kampuni yanatakiwa kufikiwa. Kuwa na timu ya watu wachache lakini yenye ufanisi. Epuka kujaza ndugu, jama na marafiki katika biashara. Hakikisha unakuwa na code of conduct kwa wote hasa madreva kwani ukimchekea dreva kila siku utapata hasara. Mara nyinyi husema kuwa na roho mbaya kwa kifupi
5. Mfumo wa uendeshaji wa biashara
Jitahidi magari kama ya ruti za transit kuwa na sifa za kuuzika kibiashara. Hii ina maana ya kwamba kupitia timu yako ya kazi hakikisha yanakuwa monitored ktk tracking, (gharama za tracking kwa gari 35,000Tzs kwa mwezi). Tengeneza gari kama ina tatizo, achana na kutengeneza gari barabarani. Usione lori lina dreva pekee kwa sababu kampuni ina uhakika wa uzima wa lori. Jenga tabia ya kuhakikisha gari linahudumiwa kwa kiwango sahihi.
6. Uombaji wa mizigo
Andika 'profile company' nzuri, baada ya hapo pita makampuni mbalimbali unaacha kitabu hicho na barua ya maombi. Usione aibu kuomba mzigo. Hii itakusaidia kuwa na uhakika wa mizigo kwani kampuni nyingi zikiona umeenda katika mfumo rasmi kama huu utapata mkataba na kipaumbele cha kupata mzigo. Mkataba unaweza kuwa wa myda mrefu au muda mfupi lakini tayari ushakuwa na uhakika wa mizigo na mzunguko wa uhakika.
NITAENDELEAA......!Sent using Jamii Forums mobile app

NAMNA YA KUENDESHA BIASHARA YA USAFISHAJI MIZIGO

Habari zenu, pili nawatakia sikukuu njema ya Eid el haj!

7. Kudhibiti na kuthibitisha gharama za kuiendesha biashara
Kumekuwa na tatizo la kudhibiti na kuthibitisha gharama za uendeshaji wa biashara hii. Gharama hizo ni za safari ie trip expenses and business running expenses. Usifanye biashara hii kwa kusikia fulani huwapa kiasi fulani cha pesa na mafuta. Pata uzoefu toka kwako lakini fanya tafiti ya gari yako na weka mfumo wako katika gharama za safari. Hizi ni baadhi ya gharama amabazo unapata na risiti

1. Rwanda trip
Road toll $152, fuel 1200lts(daf xf), comesa/insurance $267 kwa mwaka, container fee $18, driver allowance depends with the company policy lkn utamsainisha dreva petty cash voucher.

2. Zambia trip
Road toll $356 (Tunduma lusaka Tunduma), road permit 290,000Tzs/3months, carbon tax 75,000Tzs/3months, insurance/comesa $267 per annum, agaent fee 20,000Tzs, city council 40,000Tzs, Zambia tax levy 240,000Tzs/annum
3. Lubumbashi, D. R Congo
Hapa gharama zinalipwa kwa kuongezeka mipaka ie Tz to Zambia border, Zambia to Congo border hivyo itakuwa hivi

a) Tunduma/Nakonde border
Road toll $356 kwa trip, road permit 290,000Tsh/3months, carbon tax 75,000Tsh/3months, Comesa/insurance 224,000/3months, city council 40,000Tsh/trip, na agent fee 20,000/trip kama una ajent wako wa kufuatilia na kupush documentation process. Suala la bond inategemea kulipwa na mwenye mzigo au gari kutokana na malipo mliyokubaliana na makubaliano yenu ambayo ni $100 au yaweza kuwa pungufu kidogo

b) Zambia border (kasumbalesa 1)
Entrance in &out fees $200, city council 40,000kwacha, agent fee $200

c) Congo border (kasumbalesa 2)
Peage $300, wisk $30, seal fee $10, kisanga in n out $60, Entry fees in n out $200, visa driver n tboy $100 km waruhusu wawili
Angalizo. Gharama hizi zinabadilika kutokana na kushuka na kupanda kwa dola na sera za nchi. Hivyo inatakiwa kila mara kuwa wafanya cross check. Kujua gharama hizi itakusaidia kujua unapeleka mzigo kwa faida au hasara

Pili ni gharama za kuiendesha biashara yenyewe. Hii ni gharama za jumla kuanzia ofisi na lori. Unaweza ukawa wafurahia kupeleka mzigo Rwanda kwa sababu ni ruti fupi hivyo kwenda hadi trip 4 kwa mwezi lakini gharama zikawa kubwa za wear & tear, service et za gari kuliko yule aendae Congo. Mtathmini dreva wako gharama zake kwako zipoje. Angalia mishahara ulipayo na kinachozalishwa na kufikia malengo vinaendana? Jitahidi ujue pesa yako halisi na halali baada ya kutoa gharama zoote ikiwa na service ambazo waweza kuzirekodi katika ledger books, trip expenses na office running expenses. Usije ukawa waona akaunt yako ina pesa nyingi kumbe yote si yako bali inapita tu mkononi mwako

8. Faida za hii biashara
Kiukweli biashara hii kama utapata malori sahihi, madreva sahihi, staff members sahihi na channel za mizigo utapata faida nzuri sana. Ndo maana unaona kuna makampuni yana magari hadi mia 800, na kuna watu gari zinazidi kuisha tu kutokana na miongoni mwa masuala yaliyochangiwa hapo juu

8. Hasara zake
Mtaji wake ni mkubwa sasa lori linapopata ajali na kama hujakata comprehensive insurance inakuwa ni hasara kubwa sana katika biashara. Kuibiwa kwa mzigo hasa mzigo wa kurudi kama vile shaba. Ule mzigo utalipwa na kampuni ya bima lakini inasumbua sana maana hapo tarajia changamoto ya usumbufu kuanzia watu wa dola na bima pia. Lakini vilevile inaharibu status quo ya kampuni kwani mteja wako tayari ataanza kuwa na shaka na mwenendo mzima wa kampuni

9. Changamoto zake
Zipo nyingi kama vile
a. Kufanya kazi na madreva wasio waaminifu hivyo kukupa hasara kwa kuiba mafuta
b. Kuyumba kwa upatikanaji wa mizigo kwa mfano Tanzania japo kwa sasa hali kidogo imeanza kuimarika
c. Kushuka kwa malipo
Malipo ya transit cargo yameshuka utaona kutoka $5000 hadi $3600 Zambia, Congo $7000 hadi $5500/5000 Congo et al wakati gharama za uendeshaji zipo palepale
d. Utitiri wa vibali
Vibali vingi na lazima ulipie ili uwe salama kuepuka faini mbalimbali.

Mwisho
Nimejitahidi kuweka mambo muhimu kwa kiasi chake na wengine waongezee kwani hii ni biashara pana sana. Vilevile naomba mniwie radhi kwa kuchanganya lugha mbili tofauti kutokana na nafasi finyu niliyonayo katika kuandika kwa utimilifu wake kwa lugha moja.
Nawasilisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
1,500
INAENDELEA
Habari zenu, pili nawatakia sikukuu njema ya Eid el haj!
7. Kudhibiti na kuthibitisha gharama za kuiendesha biashara
Kumekuwa na tatizo la kudhibiti na kuthibitisha gharama za uendeshaji wa biashara hii. Gharama hizo ni za safari ie trip expenses and business running expenses. Usifanye biashara hii kwa kusikia fulani huwapa kiasi fulani cha pesa na mafuta. Pata uzoefu toka kwako lakini fanya tafiti ya gari yako na weka mfumo wako katika gharama za safari. Hizi ni baadhi ya gharama amabazo unapata na risiti
1. Rwanda trip
Road toll $152, fuel 1200lts(daf xf), comesa/insurance $267 kwa mwaka, container fee $18, driver allowance depends with the company policy lkn utamsainisha dreva petty cash voucher.
2. Zambia trip
Road toll $356 (Tunduma lusaka Tunduma), road permit 290,000Tzs/3months, carbon tax 75,000Tzs/3months, insurance/comesa $267 per annum, agaent fee 20,000Tzs, city council 40,000Tzs, Zambia tax levy 240,000Tzs/annum
3. Lubumbashi, D. R Congo
Hapa gharama zinalipwa kwa kuongezeka mipaka ie Tz to Zambia border, Zambia to Congo border hivyo itakuwa hivi
a) Tunduma/Nakonde border
Road toll $356 kwa trip, road permit 290,000Tsh/3months, carbon tax 75,000Tsh/3months, Comesa/insurance 224,000/3months, city council 40,000Tsh/trip, na agent fee 20,000/trip kama una ajent wako wa kufuatilia na kupush documentation process. Suala la bond inategemea kulipwa na mwenye mzigo au gari kutokana na malipo mliyokubaliana na makubaliano yenu ambayo ni $100 au yaweza kuwa pungufu kidogo
b)Zambia border (kasumbalesa 1)
Entrance in &out fees $200, city council 40,000kwacha, agent fee $200
c) Congo border (kasumbalesa 2)
Peage $300, wisk $30, seal fee $10, kisanga in n out $60, Entry fees in n out $200, visa driver n tboy $100 km waruhusu wawili
Angalizo. Gharama hizi zinabadilika kutokana na kushuka na kupanda kwa dola na sera za nchi. Hivyo inatakiwa kila mara kuwa wafanya cross check. Kujua gharama hizi itakusaidia kujua unapeleka mzigo kwa faida au hasara
Pili ni gharama za kuiendesha biashara yenyewe. Hii ni gharama za jumla kuanzia ofisi na lori. Unaweza ukawa wafurahia kupeleka mzigo Rwanda kwa sababu ni ruti fupi hivyo kwenda hadi trip 4 kwa mwezi lakini gharama zikawa kubwa za wear & tear, service et za gari kuliko yule aendae Congo. Mtathmini dreva wako gharama zake kwako zipoje. Angalia mishahara ulipayo na kinachozalishwa na kufikia malengo vinaendana? Jitahidi ujue pesa yako halisi na halali baada ya kutoa gharama zoote ikiwa na service ambazo waweza kuzirekodi katika ledger books, trip expenses na office running expenses. Usije ukawa waona akaunt yako ina pesa nyingi kumbe yote si yako bali inapita tu mkononi mwako
8. Faida za hii biashara
Kiukweli biashara hii kama utapata malori sahihi, madreva sahihi, staff members sahihi na channel za mizigo utapata faida nzuri sana. Ndo maana unaona kuna makampuni yana magari hadi mia 800, na kuna watu gari zinazidi kuisha tu kutokana na miongoni mwa masuala yaliyochangiwa hapo juu
8. Hasara zake
Mtaji wake ni mkubwa sasa lori linapopata ajali na kama hujakata comprehensive insurance inakuwa ni hasara kubwa sana katika biashara
Kuibiwa kwa mzigo hasa mzigo wa kurudi kama vile shaba. Ule mzigo utalipwa na kampuni ya bima lakini inasumbua sana maana hapo tarajia changamoto ya usumbufu kuanzia watu wa dola na bima pia. Lakini vilevile inaharibu status quo ya kampuni kwani mteja wako tayari ataanza kuwa na shaka na mwenendo mzima wa kampuni
9. Changamoto zake
Zipo nyingi kama vile
a. Kufanya kazi na madreva wasio waaminifu hivyo kukupa hasara kwa kuiba mafuta
b. Kuyumba kwa upatikanaji wa mizigo kwa mfano Tanzania japo kwa sasa hali kidogo imeanza kuimarika
c. Kushuka kwa malipo
Malipo ya transit cargo yameshuka utaona kutoka $5000 hadi $3600 Zambia, Congo $7000 hadi $5500/5000 Congo et al wakati gharama za uendeshaji zipo palepale
d. Utitiri wa vibali
Vibali vingi na lazima ulipie ili uwe salama kuepuka faini mbalimbali.
Mwisho
Nimejitahidi kuweka mambo muhimu kwa kiasi chake na wengine waongezee kwani hii ni biashara pana sana. Vilevile naomba mniwie radhi kwa kuchanganya lugha mbili tofauti kutokana na nafasi finyu niliyonayo katika kuandika kwa utimilifu wake kwa lugha moja.
Nawasilisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naweza kukuona
 
Bexb

JF-Expert Member
Oct 24, 2016
275
500
NIMEWAHI KUWA DEREVA MIAKA 6 NIKAHAMISHIWA OFISINI. HUU NI UZOEFU WANGU

Asante. Kwanza kwa wasifu mfupi nimekua truck driver kwa miaka sita pia kwa sehemu nilipata tatizo kidogo so nikatoka katika udere nikahamishiwa ofisini hivyo nikawa nimefanikiwa kupata mawili matatu kuhusiana na hii biashara.

1. Biashara hii inazo hasara zake tena kubwa kubwa lakini hili lisikutishe kwani kila biashara ina changamoto zake.

2. Unaweza ukaanza na magari idadi yoyote kwa local trips(ndani ya nchi) na kama utaamua kufanya transit goods bas nakushauri uanze na angalau gari 10 whether ni vichanja au tanker lakini nashauri kwa kuanza anza na vichanja kwa transit.(Nitafafanua kwa nini)

3. Hakikisha wewe mwenyewe mmiliki au mtu uliyemuweka kuisimamia biashara hii ana ufahamu mkubwa na wa kina kuhusu magari makubwa sio dere anakwambia rejeta imekufa inatakiwa milion 5 na wewe huna swali lolote.

A. LOCAL TRIPS (biashara ndani ya nchi)
Katika hizi kazi ni lazma uhakikishe wewe(management) unatafuta tenda za kutosha ili kuhakikisha kuwa gari yako inazunguka muda wote. Mfano labda kwa route zinazouza za Dar-njombe, mbeya, kahama au mwanza unaweza kuwa umepata kazi ya kupakia mbao toka Njombe to Dar unachotakiwa kufanya ni kuwatafuta wamiliki wa hardwares hata watatu au wanne ambao utaongea nao kuhusu kuwaletea mizigo yao toka dar hapo utakua na uhakika kua kila ukienda njombe kupakia mbao basi utakua na uhakika wa kuuma nundu ya kutosha kupeleka dukani.

Pia hakikisha unaestablish mahusiano mazuri na madalali wa maeneo utakayokua unapeleka/kufuata mizigo ya wateja wako. Kwa dar hili lipo wazi kuwa madalali ni kila kitu katika kuifanya gari yako iwe na mzunguko mzuri. Hakikisha ofisi yako inaandaa mfumo mzuri na shawishi wa commission kwa dalali atakaekutafutia mzigo ili kuifanya gari yako iwe na mzunguko wa kutosha hivyo uhakika wa kipato.
Mtimizie driver vile mlivyokubaliana na mjali pia pale anapokulilia shida. Hapa unatakiwa umfanye driver wako aione kazi ni nzuri na yenye kuonesha matunda mema kwa upande wake, hii itasaidia kutofanya michezo ya ajabu awapo kazini kama vile kuuza tyres mpya kisha kunnua chakavu na ku'retread' au kuichosha gari kwa kupiga cha juu kwa kuzidisha mizigo mingine huko njiani.

B. TRANSIT GOODS (biashara kati ya Tz na nje ya Tz)
Hii ni zaidi ya biashara kichaa kama utakua ndo umeingia kwenye tasnia na ndo ukaanza nayo. Hapa ninaasume kuwa unaanza na angalau gari 10. Sasa huku ndo kuna 'MADALALI PAPA' yaani unaweza kufa garizoote zinazunguka vibaya mno lakini wallet haisomi jomba!

Hapa kwa kuanza ni vema ukaanza na vichanja(flat beds) kwani hii itakupa faida mara mbili kulinganisha na tankers . Kwenye tankers mjomba kuna kitu kinaitwa 'SHORT'!! hii ni ile umepima diezel lita 39000 pale namba 5 halafu unafika Lusaka unakutana na jamaa flani maarufu sana pale anaitwa BONGE utatamani kufa pale anakuambia gari yako imeshusa lita 30000. Huna namna zaidi ya kampun yako kuingia mfukoni kuanya compensation ya hiyo loss. Na kikubwa hapa ukienda kigamboni unajaza tanker kwa fimbo na ukishusha Lusaka unashusha kwa 'FLOW METERS' vitu viwili kabisa yaani hadi uje kuijua michezo yao unakua umeshapata vidongda vya tumbo umekondeana vya kutusha huku ukiwa wodini unapata sindano za presha ya kushuka.

Tafuta dalali (main contractor) wa uhakika. Bila kificho, kwa experience yangu TRH na INARA ni wazuri sana ukiwatumia kwa dry cargo pia WORLD OIL ni wazuri sana ukiwatumia kwa tankers. Hapa simaanishi kuwa wana bei nzuri lah!! hayo siyajui ila utakua na uhakika wa gari zako kuzunguka zaidi hivyo kuongeza kipato zaid kwani wana tenders za kutosha.

Chagua route nzuri na rafiki kiuchumi. Mimi ni mzoefu kidogo kwa routes za Congo DRC. kwa huko congo kuna sehemu ukienda hata kama utakua unapewa 7000$ aisee utaijutia mfano ni sehemu inaitwa KIPUSHI au Likasi huko tenda zipo nyingi tu ila hakupitiki kwani sehem kubwa ya mwaka ni mvuana barabara ni mbovu kupita maelezo yaani unaweza ukalipwa 7000$ lakini gari isirudi na faida zaid ya kuongeza hasara.

RELIABLE TRUCK AND TRAILERS. Hili ni jamabo la muhimu kuzingatia kwa safari za transit hasa Congo. Hakikisha unaanza na gari nzuri na zisizochoka ili kuepuka vitonda vya tumbo. Kuna brand nzuri lakini brand za kichina zimeonekana kuperfom vizuri kwenye rough roads za Congo ukilinganisha na akina 'khadija kopa' wa ulaya hata katika bei zake. Pia faida nyingine ya brands za kichina kama vile FAW na HOWO ni kuwa zina 'high Return of Investment' japo sio rafiki sana kwa afya ya driver lakini ni very good in perfomance. Kwa upande wa trailers hebu vuta mzigo piruuu kabsa kuna zile brand tunaziita 'alitumia babu hadi mjukuu ataiacha' hapa kuna HENRED FRUEHAUF pia BHACHU aisee hapo utaipenda gari yako.

Service ni lazima. Hii haina option yaan hakikisha unapata fundi mwenyeujuzi stahili pamoja na uzoefu wa kutosha katika fani hii. Sio unatoka Dar unafika iringa inatokea tatizo ambalo lingeweza kuponywa wakati gari ipo gereji dar hii itasaidia kuokoa gharama zisizo za lazma. Pia ajiri professionals wa kukusaidia katika uendeshaji wa mifumo yote ya kampuni yako. Zile zama za kujifanya kuwa wewe mmiliki ndo unakua fundi mkuu mara marketing officer mara procurement manager mara HR ZILISHAPITWA NA WAKATI, ajiri watu makini watakaokusaidia kuinuka juu.

C. CHANGAMOTO
Katika biashara yoyote changamoto hazikosekani hata hu pia zipo tena za kutosha tu.

a. Wizi/ upotevu wa mizigo. Hapa huwa kuna kampuni zinakatia bima ile mizigo ambayo ipo likely kupitiwa na vipanga. katika hili hakikisha gari zako zinatembea muda wa mchana na hata ikiwa ni usiku isizidi saa tatu usiku.

b. Gari kuharibika. Hili ni jambo la kawaida gari ipo Kapiri ikaua diff au engine ikaknock na ikahitajika milioni 20 ya fasta. Hapa hakikisha kuwa akaunti yako inasoma pesa kwa ajili ya emergency yoyote.

c. BIMA wapo brokers wa bima wasio waaminifu yaani gari yako ikipata tatizo anakua hana uwezo wa kukusaidai. Hapa hakikisha unapata broker mzuri na pia isikuume kukata comprehensive kwani ina msaada mkubwa wakati wa majanga na hutakuja kujuitia.

Dah hayo ni machache ninayoyafahamu kuhusiana na biashara hii ya trucking ndani na nje ya nchi.
 
HIRAMA

Member
Jun 26, 2012
10
20
Habarini Wanajamvi

Mimi ni kijana nina mtaji wa 70m natamani kuagiza fuso na kuja kuifanyia modification hapa ndani ya nchi (Tabata Dampo au Arusha) iwe tandam iweze kubeba tani 18. Sasa nauliza kwa wenye uzoefu na hiyo kazi, wanisaidie gharama za kufanya modification na ushauri kua biashara hiyo inalipa au vipi na pia wanipe changamoto zake.
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
3,766
2,000
Mhh, katika gari ambazo sizikubali kama zinarudisha pesa vizuri ni hayo mafuso tandam, modification ni nyingi mno na nasikia huwa hazikai sana na engine yake kutokana na mzigo mkubwa zinaobeba(by default fuso inabeba tani 4)

Kwa nini usifikirie semi kwa pesa unayotaka kuwekeza?
 
mmbangaya

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
1,002
2,000
Nunua scania tani 15 brother hautajuta. Scania ndio gari ya mtu wa kipato cha kati hiyo fuso utapata hela mwanzo tuu ila baada ya miaka 2 itakuwa nyang'anyang'a ila scania trust me hata baada ya miaka 6 itakuwa vile vile. Nakuambia from my own experience.
 
Mahole

JF-Expert Member
May 17, 2018
683
1,000
Tandam ukipata dereva anaejielewa pamoja na msimamizi mzuri ndani ya mwaka mmoja au mmoja na nusu pesa yako isharudi na inaweza kudumu miaka ming sana tatzo la scania kipisi hua inasumbua mizani inatakiwa usizidishe hata kidogo tani15 kamili ukizidisha inakula kwako.
 
Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
1,252
2,000
Nunua ila kumlinda dereva asipige dili zake bila wewe kujua nicheki, ntakufungia kifaa cha kujua sehemu yoyote linapokuwepo, udanganyifu na dili za dereva zinakomea hapa, na pia usalama wa chombo ikitokea upotevu au kuibiwa.

Malipo ni ya mara moja ju, hakuna ya mwezi wala mwaka kama wanavyofanya makampuni mengi.

Napatikana dodoma kwa sasa.
 
Afrolink-Tz Consult Ltd

JF-Expert Member
Feb 25, 2018
399
1,000
Mkuu nakushauri nunua scania kwa hela hy unapata. Kwa mfano hapo Tabata Dampo kuna jamaa anauza (scania 113 top linear na trailer) anauza kwa mil 50 bei ya kuanzia, trailer flatbed za kubeba hadi tani 35 zimesimama sana. Kwa hy hela yako naamn gari hz za gharama za uendeshaji zipo chini unaweza kutoboa. Badala ya kununua fuso.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom