Biashara ya usafirishaji wa anga ni biashara kichaa, sijui nani alimshauri Hayati Magufuli

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,453
8,319
Hii biashara ya usafirishaji wa ndege ni ngumu sana ndio usishangae taifa kubwa kama USA kupitia serikali yake kutojiusisha na biashara hii.

Pesa tulizopoteza kununua madege kwa nchi changa kama hii zingeweza kuboresha viwanja vya ndege kwenye mikoa iliyo na kuitaji huduma na kuita wawekazaji ndani na nje kila mtu kufanya biashara.

Kuna matajiri waliopo ndani tz na nje anaweza kununua ndege yake moja kwa ajili ya kufanya usafiri wa mkoa wake kama viwanja vingekuwa vimeboreshwa.

Serikali inatakiwa kushauriwa kuondoa ubinafsi kwenye sekta ambazo kwa sasa ilitakiwa kuachana nazo ili kupata mapato kwa njia nyengine.

Wekezeni kwenye miundo mbinu kama viwanja,barabara,bandari kavu,bandari za kisasa na n.k ili watakao kuja kufanya biashara muwatoze kodi mbona mnaweza kutengeneza masoko kwa ajili ya wafanya biashara wadogo mkashindwa hayo.
 
Umeamua kuandika tu basi. Tuachane na mambo ya mwendazake. Ila kuwa na ndege ni wazo Zuri la kibiashara. Tena maendeleo ni pale watanzania wataamua kutumia ndege zaidi kuliko usafiri mingine hususani mikoa ya mbali. .

Natoa wazo wanunue ndege za kusafirisha misiba. Waweke usafiri mbadala uwanja wa ndege ili wakishusha maiti iwe rahisi kuwafikisha waombolezaji majumbani mwao. .

wazo la pili nitaamdika baadae
 
Umechukia mno ndege kununuliwa! Unadhani hatuna haja ya kuwa na ndege?

Au unashauri watanzania tusiwe tunapanda ndege kabisa!??
 
Hata mimi nafikiri ingekuwa vizuri zaidi kama serikali ingeboresha na kujenga viwanja vipya zaidi ndege halafu serikali angebaki kama regulator tu. Hii biashara ni kichaa haswa
 
Ndege zilinunuliwa zipo, ni wazo zuri na maamuzi mazuri mtu kuwa na chakwako.

Wewe kinakukera nini labda?

Hizo hela za kununulia ndege, mfano zisingelinunua ndege halafu zikapigwa kifisadi, wewe layman ungeelewa?

Kama unaona zinafanya kwa hasara, washauri wahusika wazipaki zisubiri mfumo sahihi wa biashara, lakini ziwepo.

Heri kuwa na kitu kuliko kukosa kitu.
 
Mtoa mada upuuzi wako huu umevuka mipaka! 😂

Au hujasoma kabisa hata sekondari , wenzio waliosoma Jiografia walikutana mpaka na maswali ya NECTA kwenye essay kuhusu faida za transport and communication.

Unatia huruma sana wewe! Hata kama ulisoma basi ulikua mtoro mpaka ulipofeli na kupata zero

Aliyenunua zile ndege alijenga viwanja vya ndege pia fly over, aliboresha bus stands na masoko ya kuuzia bidhaa, pia alianza na mikakati ya kutengeneza bwawa la kuzalisha umeme, Lakini kubwa hukujua lengo lake kubwa baadae amalizane na Viwanda kwa kukamilisha hayo

Sasa wewe mlevi unaongea nini tukuelewe😁
 
Mtoa mada upuuzi wako huu umevuka mipaka! 😂
Au hujasoma kabisa hata sekondari , wenzio waliosoma Jiografia walikutana mpaka na maswali ya NECTA kwenye essay kuhusu faida za transport and communication.

Unatia huruma sana wewe! Hata kama ulisoma basi ulikua mtoro mpaka ulipofeli na kupata zero

Aliyenunua zile ndege alijenga viwanja vya ndege pia fly over, aliboresha bus stands na masoko ya kuuzia bidhaa, pia alianza na mikakati ya kutengeneza bwawa la kuzalisha umeme
Lakini kubwa hukujua lengo lake kubwa baadae amalizane na Viwanda kwa kukamilisha hayo

Sasa wewe mlevi unaongea nini tukuelewe😁
Umakaa kabisa na wewe unachangia mada hata ulichokiongea ujui unachangia nini?

Ulishawai hata kusafiri kuvuka mipaka yako ya nchi ukajionea sekta ya usafiri wa anga ulivyo kwa nchi kubwa. Ndege utaisikia tena ukipanda basi ni mikoa michache itakayo kufikia kuwa na viwanja.

Wewe ulisoma wapi kwamba kujibu unaanza na matusi na vyeo kusoma
 
Tatizo la Tanzania ilikuwa ni kukosekana kwa carrier mwenye uwezo, alikuwepo Fastjet bei zake zilikuwa nzuri ila ilikuwa na matatizo yake mengi ie uchelewaji.
 
Tatizo la Tanzania ilikuwa ni kukosekana kwa carrier mwenye uwezo, alikuwepo Fastjet bei zake zilikuwa nzuri ila ilikuwa na matatizo yake mengi ie uchelewaji.
Nilichogundua serikali ya tanzania inaogopa changamoto kibiashara kwenye utendaji na ndio maana nikatoa wazo ni bora kuruhusu wawekazaji wa usafiri ndani na yenyewe kudili na viwanja.

Mbona wingereza wameshindwa kumiliki vilabu vyao wakaamua kuwapa wawekezaji wa nje ili wao wao dili na viwanja na mapato
 
umakaa kabisa na wewe unachangia mada hata ulichokiongea ujui unachangia nini?.
ulishawai hata kusafiri kuvuka mipaka yako ya nchi ukajionea sekta ya usafiri wa anga ulivyo kwa nchi kubwa.ndege utaisikia tena ukipanda basi ni mikoa michache itakayo kufikia kuwa na viwanja.

wewe ulisoma wapi kwamba kujibu unaanza na matusi na vyeo kusoma
Kwanza wewe naona tutapata tabu kukuelezea faida za ndege
Wakati walimu wako walishindwa kukufundisha kutokana na ubishi wako

Leo hii unataka ufanane na USA kisa yeye hafanyi kitu fulani nawe ufuate

Tanzania ni nchi inayoendelea na USA ni nchi iliyoendelea tayari hivyo tunahitaji ndege katika kukuza utalii, usafirishaji wa bidhaa pamoja na wafanya biashara kutoka mataifa mbalimbali kuzidi kukuza uchumi

Sasa wewe hoja yako ndio haieleweki ?unakuja kubwabwaja tu ooh sijui USA ooh sijui biashara kichaa😂

Ongea fact tukuelewe
 
tabu unapata wewe ambaye hupo hupo kuto kujibu unacho kiona unajua.
watanzania wengi kama wewe ukiambia eleza unaanza matusi na kubeza eleza.na kushauri kuna kazi ya kuchambua mchele leo siku ya wapenda nao
 
  • ndege biashara ngumu Sana especially Kwa nchi masikini
  • ndio maana wapinzani walishauri kuwepo na bussines plan juu ya kuanzisha biashara ya ndege,
 
Kwanza wewe naona tutapata tabu kukuelezea faida za ndege
Wakati walimu wako walishindwa kukufundisha kutokana na ubishi wako

Leo hii unataka ufanane na USA kisa yeye hafanyi kitu fulani nawe ufuate

Tanzania ni nchi inayoendelea na USA ni nchi iliyoendelea tayari hivyo tunahitaji ndege katika kukuza utalii, usafirishaji wa bidhaa pamoja na wafanya biashara kutoka mataifa mbalimbali kuzidi kukuza uchumi

Sasa wewe hoja yako ndio haieleweki ?unakuja kubwabwaja tu ooh sijui USA ooh sijui biashara kichaa😂

Ongea fact tukuelewe
  • mpaka Sasa ndege zetu zimeleta watalii wangapi?
  • kwani Watalii hawawezi kuja kwa ndege za Mashirika mengine? Mfano Emirates nk?
 
Wengi mmemshambulia mtoa mada lakini ana point to prove. Serikali ilinunua ndege ikazikodisha? Au ikaendesha biashara yenyewe? Tuanzie hapo
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom