Biashara ya upandaji wa miti ya mbao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya upandaji wa miti ya mbao

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by KVM, Apr 5, 2012.

 1. K

  KVM JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,765
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

  Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

  Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

  Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

  Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
   
 2. W

  Wenger JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 424
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Hiyo biashara Mufindi, Njombe na Makete inalipa sana. Kule Njombe vijijini kwa sasa mti mmoja wa kupasua mbao ukiuza jumla unakwenda kwa bei kati 10,000 mpaka 15,000 kutemegea na size yake na wateja wapo sio wakutafuta wanakufuata wenyewe, sasa ukiwa na miti 100,000 tayari milionea. mwenye nimenunua mashamba huko kwaajili ya kupanda Pines .
   
 3. c

  collezione JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  pia kuna mpango wa kimataifa unakuja. Utakuwa unalipwa hela kutokana na idadi ya miti unayotunza...

  This has been started by international organisations, concerning with environment and global warming.

  Nia kubwa ni Ku_promote upandaji na utunzaji wa mazingira. So ukiwa na shamba la miti, utakuwa unalipwa kila mwezi hela kadhaa.

  Mradi umeanza nchi za ulaya na asia. Kwa africa bado. Sina uhakika kwa nn kwa africa, bado haujaja.
   
 4. K

  KVM JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,765
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Kwa mti unaoweza kutoa angalau mbao tatu ndefu za 2" x6" hiyo bei ni ndogo sana ukilinganisha na atakachopata mnunuzi. Ubao mrefu wa 2x6 na uliopakwa dawa DSM una siyo chini ya Shs 17,000. Bei ya mti moja pale Mafinga (Sao Hill) ni zaidi ya Shs. 50 000. Tatizo kule vijijini watu wananunua vimiti vichanga sana.
   
 5. k

  kakaamiye Senior Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ninashukuru sana kwa hii topic, hata mimi nipo interested sana na kupanda miti na ni idea ya muda sasa, issue kwangu ni namna ya kuanza especially kupata shamba kwa ajili ya kupanda. Ningeomba kupata japo idea kama ninaweza kupata eneo huko njombe na kwingineko ukizingatia mimi ninaishi dar. Na price inakuwaje, pia gharama za miche kwa sasa ni kiasi gani na kuotesha plus kutunza. Please please mwenye data ninaomba
   
 6. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Wasiliana na Malila, ni memba humu, mtafute
  All the best mkuu.
   
 7. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,925
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  Kuna miti inaitwa mitiki,hii vipi kupanda mpaka kuvuna inachukua miaka mingapi? Je hizo pines na eucalyptus nikipanda kwenye heka 10 ninunue miche mingapi? Au unaweza kunisaidia kupanda miche ya hekari kumi?
   
 8. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Halafu mkubwa KVM umelete uzi mzuri ila mwaga maujuziyako zaidi kwenye hii habari ya miti ili na wengine tupate nguvu au mwamko,pengine tukatoka kiaina. Mfano miti hiyo uliyoitaja inachukua muda gani kutunzampaka kuvuna, je yaweza kutoa mbao ngapi n.k
   
 9. K

  KVM JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,765
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Subiri kidogo nitakupa data/hadithi ya upandaji miti.
   
 10. K

  KVM JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,765
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Kazi ya kupanda miti inachukua muda mrefu kidogo. Hesabia siyo chini ya miaka kumi na mbili hivi
  toka upande ndiyo unaanza kuvuna. Unatakiwa kwenda nayo taratibu. Kila mwaka panda miti kiasi
  fulani ili utakapoanza kuvuna uendelee kuvuna kila mwaka na kupanda ulikovuna.
  Kuhusu gharama za kupanda zinatofautiana kufuatana na kijiji. Kijijini kwangu kwa sasa nadhani ni
  aghali kidogo kwani ni watu wengi wanopanda miti. Muamko umekuwa mkubwa sana. Ni mimi niliwastua
  baada ya kuona kazi niliyokuwa naifanya. Kwa sasa nadhani mche mmoja upo chini ya Sh 100 nakuupanda
  ni Shs 30. Mimi nilianza kwa kununua mche Shs 30 na kupanda Shs 20. Hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita
  lakini leo mti huo naweza kuuza siyo chini ya Shs 10,000 mpaka 20,000.

  Kiasi cha mbao utakazopata inategemea na aina ya miti, matunzo,umri wa mti, na ulipanda
  kwa nafasi gani (distance between trees). Mazungumzo yangu hapa yanahusu zaidi miti aina ya Pines.
  Kwa kawaida tegemea kupata kati ya mbao tano za 2x6 kama ukiharakisha kuvuna lakini mtihuo
  kama umekomaa (miaka 25 hivi) umetunzwa vizuri na ulipandwa kwa nafasi nzuri unaweza kutoa hadi
  mbao 30. Wengi wetu ikifika miaka 12 tunavuna, na kinachopatikana siyo haba lakini nadhani ni
  nzuri zaidi kuvuna kuanzia miaka 15 au 16 hivi kwani utakuwa na uhakika wa kupata pingili siyo
  chini ya mbili na mbao ndefu za 2x6 angalau 6 nakwenda juu . Ubao mmoja wa 2x6 uliopakwa dawa
  hapo DSM unauzwa siyo chini ya Shs 17,000 na kule Mafinga kiwandani bila dawa ni Shs 10,000
  bila kupungua senti tano.

  Maeneo Mazuri za Kupanda Miti

  Miti ninayozungumzia hapa ni Pines, Cypress na Eucalyptus. Miti hii inaota na kustawi vizuri sana
  nyanda za juu kusini. Ukitaka kupanda miti nakushauri uende Njombe halafu kutoka hapo fuata barabara
  nne: Kwenda Makete, Kwenda Ludewa, Kwenda Songea na Kwenda Lupembe. Utakapopita sehemu hizo zote
  utaoona maeneo mazuri sana ya kupanda miti. Kupata eneo unaweza kununua kijijini au kwa wananchi.
  Nakushauri usikubali kukodishiwa. Bei inategemea na eneo. Kuna sehemu upandaji wa miti umeshika kasi
  sana kwa hiyo maeneo hayo ardhi itakuwa aghali kidogo japokuwa ndiyo sehemu nzuri kwani wananchi
  wake watakuwa na uzoefu wa upandaji miti na hutakuwa peke yako kwenye kuhangaika kudhibiti moto.

  Matunzo ya Miti

  Baada ya kupanda unaweza kufyekelea mara moja au mbili mpaka mti ukomae. Pruning nayo unaweza kufanya
  mara mbili. Njia za kuzuia moto (Fire Lines) unatakiwa utengeneze kila mwaka bila kukosa. Kwa vile
  mimi nimepanda eneo kubwa basi niliamua kununua ng'ombe ambao wananisaidia kupunguza majani
  pembezoni mwa shamba.

  Ili uweze kumudu vizuri upandaji wa miti mingi, hasa kama utapanda kila mwaka, na nakushauri upande
  kila mwaka kwa kweli inabidi uajiri kijana, kama siyo mwanzoni basi baada ya miaka kadhaa kupita.
  Yeye ndiye atakayekuwa ndiyo wa kwanza kujua shamba linakabiliwa na matatizo gani na namna ya kuyatatua
  haraka iwezekanavyo. Mimi shamba langu ni kubwa (siyo chini ya ekari 1500) nimeajiri vijana watatu.
  Mmoja wao anaishi ndani ya shamba na ndiye anayetunza ng'ombe. Pamoja na ukubwa wa shamba lakini
  nimelipanda polepole kwa miaka kama kumi hivi.

  Nimeamua kuambatanisha picha chache za mradi wangu nashindwa kuleta nyingi zaidi kwa vile zinatumia muda mrefu mno kuload.
   

  Attached Files:

 11. A

  Ameir JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Biashara ya mbao inalipa sana aisee ndungu. Namjua jamaa yangu mmoja anafanya na rafiki yake. Nimeongea nae jana tu aliniambia wanaenda kijijini.
   
 12. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu safi sana nimeipenda sana project yako pamoja na ng'ombe wazuri wa kienyeji. Karibu sana hapo juu kwenye jukwaa la ujasiriamali kuna nondo za kutosha, NB kuna thread yetu initwa "Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani?" tulijadili pia miti ya mbao karibu kwenye mjadala
   
 13. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 2,668
  Likes Received: 1,183
  Trophy Points: 280
  Kilimo Kwanza in the move...nimeipenda sana hii topic. Alijisemea Mwalimu Kilimo ni uti wa mgongo ni kweli kabisa. Shukrani mkuu kwa mada hii
   
 14. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Mkubwa, umetisha sana kwa kweli. Haya ndiyo mambo tunapaswa kufanya ili kujinasua na pingu za ajira, na kwa wale tunaoanza kuchungulia anga hizo za ujasiriamali basi wewe ni mmoja wa WAALIMU wetu.
  Ahsante sana kwa mchango wako na usiishie hapo, endelea kutoa darasa based on your experience.
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,837
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Mi hii biashara nimeishtukia ila tatizo nikupata maeneo ya kupanda miti maeneo mengi yameshwa panda mi nacho kifanya sasa nanua maeneo kwa wenyeji wanauza pamoja na miti.
   
 16. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 7,919
  Likes Received: 3,784
  Trophy Points: 280
  hii mitiki(teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja(wanatumia kwa nguzo za umeme ,kujenga meli na fenicha za gharama) , kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000
   
 17. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 453
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee hizi taarifa ni za muhimu sana,tuna eneo moshi karibu heka kumi sijajua naweza kupata wapi taarifa za miti itakayochukua muda wa wastani chini ya miaka kumi ili nipande,miti baadhi iliyopo ni cyprus ila naona kama inachukua miaka mingi mno,kama naweza kunisaidia ushauri
   
 18. K

  KVM JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,765
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Cypresses kwa kawaida zinachukua muda mrefu kidogo. Pines watu wanaweza kuvuna zikiwa na miaka hata kumi lakini kwa kweli ni vizuri kuvumilia kidogo angalau ifikie miaka kama 15 hivi kwani hapo kipato chake kinaweza kuwa maradufu. Sina uhakika na hali ya hewa ya Moshi kama Pines zinastawi vizuri.
   
 19. K

  KVM JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,765
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Ardhi ya kupanda miti kama pines bado ni nyingi sana hasa kwenye karibu ya mkoa wote wa Njombe has kwenye wilaya za Njombe, Ludewa na Makete. Nadhani kuna sehemu za mkoa wa Rukwa na mbeya miti hii hustawi vizuri pia.

  Mimi nawatia moyo nyote ambao mnataka kupanda miti kufanya hivyo. siyo lazima uwe na kipato kikubwa sana. Huu ni mradi mzuri kwa wafanyakazi. Mimi nimepanda miti kutumia mshahara wangu tu. Tunaweza kupishana kipato lakini panda angalau eka 10 au 20 kwa mwaka. Ni gharama ndogo tu. Hata mimi mshahara wangu siyo mkubwa sana lakini kwa uvumilivu sana nimeweza kupanda miti ya kutosha.

  Kazi ya kupanda inafanyika mwezi wa 12 kwa mikoa ya kusini. Ukishapanda huo mti unasubiri miaka ya kustaafu basi unaanza kuvuna. Ni kiunua mgongo kizuri kwa wafanyakazi. Lakini ukiwa kijana bado ni kipato tosha na cha uhakika kwa kila mwaka. Mbao za Tanzania zinauzwa Kenya, Uganda, South Sudan, Somalia na Uarabuni. Kwa sasa hivi mbao za Tanzania hazitoshi kwa hiyo wapasuaji wanakwenda mpaka Malawi kununua miti huko.

  Uzuri mwingine wa kupanda mti ni kuwa unawatia hamasa wenyeji wa eneo utakalopanda miti. Wakati naanza kupanda miti pale kijijini nilikuwa karibu peke yangu tu. Baada ya kuwashauri wanakijiji nao kufanya kile nilichokuwa nafanya nao wakaanza kupanda miti. Leo hii kijiji kimezungukwa na mashamba mengi ya miti ya wanakijiji. Baada ya miaka mitano uchumi wa kile kijiji utapaa sana kwani nitakuwepo kuhakikisha hawalaliwi na walanguzi wa miti.
   
 20. W

  Wenger JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 424
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda january 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
   
Loading...