Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,265
- 23,198
Tulikotoka, tuliko na tunakoelekea...! CCM yatuchezesha sindimba. Je leo wanaokamata na wanaokamatwa, miaka kumi iliyopita walikuwepo?
Kabla ya mwaka 2005, taifa letu lilikuwa imefikia pabaya na matumaini ya Watanzania kujikwamua kijamii, kiuchumi na kisiasa yalianza kufifia sana chini ya uongozi wa chama tawala, CCM. Ni kwa sababu hii Uchaguzi Mkuu wa 2005 ulitawaliwa na ahadi kemkem kutoka kwa mgombea Urais kupitia CCM, Jakaya Mrisho Kikwete.
Moja katika ahadi hizo ilikuwa ni kupiga vita biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa kuhakikisha inatokomezwa nchini. Hebu tufuatilie kidogo hii historia na labda tutaweza kupata kamwanga kwa nini leo, miaka zaidi ya kumi baadaye, bado inatokea hii kamata kamata ya Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Hebu tufuatilie mwaka kwa mwaka toka wakati huo hadi leo...
2006
WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.
Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili niwafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.
Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.
Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya viongozi wa dini wa madhehebu fulani.
Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na marobota ya mitumba.
Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu waDar es Salaam na Zanzibar.
Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.
Source: Written by Mwananchi
Monday, 18 September 2006
*Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
*Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
*Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
*Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani
2007
Naibu Kamishna wa Polisi (ACP), Peter Kivuyo, ameonyesha mbele ya waandishi wa habari kitabu kilichoelezwa kuwa na orodha ya watu wanaotuhumiwa kuhusiana na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa majina hayo yalikuwa yakichunguzwa.
Pamoja na mambo mengine, Kivuyo alisema kuwa kitabu hicho kilikuwa na orodha ya majina pamoja na taarifa ya kila mtuhumiwa kuonyesha anahusikaje na biashara hiyo.
“Hiki kitabu kina kila kitu ni swala tu la muda, lakini ukweli ni kwamba wahusika wote wapo humu na hata mali wanazomiliki. Pia tunaendelea na zoezi la kuwapata wengine,” alikaririwa Kivuyo akisema.
Mwezi Juni 2007, mbunge wa viti maalum kupitia tiketya Vijana CCM, Amina Chifupa Mpakanjia alikufa kifo chenye utata baada ya kutishia kuanika bungeni majina ya watuhumiwa vigogo wa madaya ya kulevya.
Ni mwaka huo Mtandao wa Wikileaks ulipofichua taarifa zilizotokana na nyaraka za siri, na kuitaja Tanzania kama kituo kimojawapo maarufu kinachotumika kupitishia dawa za kulevya barani Afrika.
Madai hayo yalikuja siku chache baada ya mtandao wa Wikileaks kuibua mambo mazito juu ya Tanzania, moja likidai Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea anakwamishwa na Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua katika kesi muhimu.
2008
Naibu Kamishna wa Polisi (ACP), Peter Kivuyo amesema baada ya kukamilisha kazi ya kuwachunguza wanatuhumiwa wote wa biashara ya dawa za kulevya, ushahidi umeonesha ni watu zaidi ya 100 wanaojihusisha na biashara hiyo.
Mapema katika mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, jeshi hilo lilisema lilipata na majina ya watuhumiwa 225 nchi nzima 78 kati yao wakiwa ni wakazi wa mjini Dar es Salaam.
Hata hivyo orodha inayohusisha watu 34 walioonekana kuwa ni ‘vigogo’, ilikwishakabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete tokea mwezi November waka uliopita.
2010
Inaaminika kuwa woga wa kashfa ya madawa ya kulevya ulimlazimisha mgombea wa CCM Jakaya Mrisho Kikwete kukacha mdahalo uliopangwa kati ya wagombea.
Tutaendelea kufuatilia hii historia...