Biashara ya ulanguzi kwa watoto na madanguro Tanzania

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,504
2,816
:angry:
Nimeona nitumie kiswahili ili aibu hii ya Biashara ya Ulanguzi kwa watoto na Biashara ya Madanguro tuisome na kuichangia kitanzaniatanzania Maana Kwa kiingereza nimeona nitakuwa nimejianika mno kwa walio nje na maono mema ya nchi hii.

Nimefusatilia sana mjadala wa BBC kwa siku tatu na umemalizika leo asubuhi.

Muhtasari
Siku ya kwanza
Mtangazaji wa BBC aliwahoji watoto wanaojihusisha na biashara ya Udanguro. walieleza namna walivyoingia Jijini wakihadaiwa kuwa wanaletwa Jijini kufanya kazi nzuri ya kipato. wengi wamedanganywa kutokea vijijni ambako maisha ni magumu. Na walivyofika wakajikuta wanafugwa kama watumwa na kazi iliypo ni kulazimishwa kuuza miilio yao!! walieleza namna ambavyo hawapendi lakini hawana pa kutokea. Hebu fikiria mtoto umri wa miaka 11, 12 au hata 13!!! Tena mmoja wao akasema wanaondesha madanguro hayo wakamatwe!! Wanapochukuliwa hupewa labda elfu 50,000 huambulia kiduchu to 10,000 au zaidi kidogo. na kama mtoto akirudi na pesa kidogo basi hapewi hata senti tano!!! anaaambiwa utajijua mwenyewe!!

Siku ya pili
Mtangazaji alimhoji mmoja wa wamiliki madangauro na wafanya biashara hiyo chafu, mbaya, fisadi, yenye kutia kichefuchefu!
Alitamba kuwa alirithishwa na bibi yake. Kwa hiyo haoni shida yoyote. Maana hakusoma!! hivyo kazi yoyote kwake ni halali!!!
'mtu akija ananiachia mzigo wangu naye anaondoka na mzigo wake!!' Hawa watoto wadogo ndo mizigo!! na akaendelea kulonga namna anavyowakamua hawa watoto. wakipewa elfu hamsini yeye anachukuwa 30,000 na 20,000 anamwachia mtoto.( UONGO!!) Mchafuzi huyo aliendelea kutamba kuwa na kocha maalum wa kuwafunza watoto hawa nmna ya kujituma wakiwa kazini!!

Siku ya tatu- Niliyokuwa nasubiri!!
Mtangazaji aliwahoji watu wa kiwawode (NGO) Then Waziri Sofia Simba na msemaji wa Jeshi la Polisi (Tena mwanamke!!)
Hapa ndo uozo, upupu, uzandiki, uongo, ufinyu wa uelezi ulivyojitokeza!! Hasa kwa wawili wa mwisho.
Sofia Simba alidai kuwa wanajitahidi kutekeleza na kulinda maslahi ya watoto. Ingawa alikiri kuwa tatizo lipo. Lakini hakueleza bayana nmna wanavyolishulikia. msemaji wapolisi alidai kuwa kama wananchi watartipoti polisi basi hatua zitachukuliwa.

Sasa wanajamii Nina maswali mengi tu
Mpaka mwandishi wa BBC anawahoji ina maana kweli serikali haina habari?
Maana mpolisi huyo alidai wanafanya kwa siri- je a kina Willy Gamba Polisi hawpo?
Anyway nisimalize yote mengi ya maswali tuendelee kudadavua hapa labda na njia za kukomesha unyama huu. Ila serilaki 100% inakoroma usingizini!!
Nawasilisha 

kisu

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
941
321
Serikali ya magamba (hasa viongozi) imeshindwa kusimamia watoto wetu na wananchi kwa ujumla kwa kuwajengea mazingira mazuri ya Elimu, Afya, Ajira, Miundo mbinu n.k.Wao wanafikiria matumbo yao tuu. Mpaka Katiba na Uongozi ubadilishwe. Kila siku maafa na maisha magumu.
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
4,531
2,523
Maarifa, umesahau kama yule mama mwenye danguro alisema hao askari wakenda huko kukamata watoto hao basi wengine 'humaliziana kistaili' yaani kwa ngono, na akajitapa kwa kusema kuwa 'unaona ch*chu za hao binti wengine zilivyosimama'. Na akaongezea kuwa anawapeleka Arabuni mpaka China.

Kwa kweli nilifuatilia mjadala ule na kuona kwenye nchi hii kuna watu na viatu, na wasemaji wa Serikali walijikanyaga weeeee hamna la maana walilosema.
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,830
Kasumba ndiyo inayotuharibia utamaduni wetu. Haya madanguro nchi za magharibi yamehalalishwa na ndiyo yaliyosababisha biashara ya ngono za online kushamiri. Biashara ya madanguro ndiyo soko kubwa la picha za ufuska, wakati ulaya ilikoanzia biashara hiyo inapoanza kusuasua, bara la asia ndo limeshamiri kwa kuwa umaskini nao huchangia kwa kiasi kikubwa. Afrika nayo imeingia kwenye mkumbo huo wakati mataifa ya Afrika magharibi yakiwa na mawakala wakubwa wa kutafuta wasichana kuingizwa kwenye system hiyo na kuwapeleka kwenye mahoteli ya ufukweni. Inatisha kwani kuna wabongo kadhaa wamenaswa katika biashara hiyo.

Hii biashara ya madanguro ndiyo western civilization wanaiita Escort Service na ni rasmi inayotambuliwa na serikali na wanalipia kodi, na
ipo kwenye yellow pages. Ni utamaduni wao au mfumo wao wa kufanya ufuska hasa kwa wanaopendelea maisha single na pia ina mshiko kwa wale wasio na dhamiri ya dini wala utamaduni, wanajisikia huru kufanya kile moyo inapenda. Ni biashara ya kwenda kwa mbele kama vile kubadilisha kanga kila kukicha. Biashara hiyo ndiyo iliyozindua wanasayansi kubuni mbinu malimbali ya kutengeneza maungo ya kuvutia kwa kudunga sindano (plastic surgery), kama kutunisha matiti yaliyo tepetepe, kutunisha makalio yaliyosinyaa nk. Wengi wanaojihisisha na biashara hiyo maumbo yao yanavyoonekana si original bali ni make up.

Turudi kwenye mila na desturi zetu, vijana wapitie formal and informal education itasaidia kuwapa sense ya maisha vinginevyo haya madanguro watafikiria ndio ustaarabu kwa vile hata ulaya wanafanya hivyo.
 

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
yani watoto wanahangamia wao wanajidai hawajui.................inasikitisha kwakweli,huyu waziri sishangai kusema hvo mana kichwa chake kinawza ngono tu
 

kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,346
1,675
Hii habari inasikitisha sana sana kwani kadiri ya mleta mada inahusisha watoto chini ya miaka 18!! Hii hakika ni JINAI na hamna namna yoyote ya kuhalalisha. Kama ni kweli hiyo biashara inafanyika hapa Tz na imeweza hata kuripotiwa na BBC na hamna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali wala vyombo vya dola ni hatari zaidi.Kimsingi hii ni kashfa ambayo ingempasa waziri mwenye dhamana na watoto awajibishwe haraka sana!! Pia mitandao inayotetea haki za binadamu inapaswa kufuatilia hili jambo kwa uzito mkubwa kwani huu ni unyama na ukatili mkubwa kwa watoto!
 

mbasamwoga

Member
Jul 6, 2011
70
11
Eeh mungu utusamehe kwa kuwachagua viongozi viziwi na vipofu wasiosikia shida za watu wao.
Habari hii ni miongoni mwa habari zinazonitia simanzi
 

Kisusi Mohammed

JF-Expert Member
Aug 10, 2009
563
461
Inauma sn, lakini hapa ndo huja dhana ya jamii kujichukulia sheria mkononi, je cc km wana forum tumefanya nini kulipinga na kulikomesha hili? Km tunaweza kualikana vikao na kuchangia harusi kwa nini tusitoe mchango wetu kwenye suala hili? Wanaoangamia ni dada zetu, watoto wetu na hatimae jamii nzima, nguvu kazi ya kuzalisha inanyonywa na vitendo kama hivi, je hatuoni umuhimu wa kuwaokoa hawa wazalendo wenzetu na kuwashirikisha kwny uzalishaji mali wa nchi hii? Nipo tayari kujitolea kwa lolote kukomesha uny
 

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,181
1,867
Inauma sn, lakini hapa ndo huja dhana ya jamii kujichukulia sheria mkononi, je cc km wana forum tumefanya nini kulipinga na kulikomesha hili? Km tunaweza kualikana vikao na kuchangia harusi kwa nini tusitoe mchango wetu kwenye suala hili? Wanaoangamia ni dada zetu, watoto wetu na hatimae jamii nzima, nguvu kazi ya kuzalisha inanyonywa na vitendo kama hivi, je hatuoni umuhimu wa kuwaokoa hawa wazalendo wenzetu na kuwashirikisha kwny uzalishaji mali wa nchi hii? Nipo tayari kujitolea kwa lolote kukomesha uny

Kisusi thanks kwa hili! Seriously mimi pia napata shida sana kwani mambo mengi tunaishia kuyajadili tu na hakuna hatua yeyote tunayochukua kukabiliana nayo huku tukijua fika kwamba sisi ni wahanga kama sio directly basi ni indirectly. Ongea na wasomi including lecturers kwenye universities na kokote kule hawana majibu ya matatizo zaidi ya kuongea then basi hakuna kinachofanyika. Ni kichekesho kwamba tunatarajia lolote kutoka kwa Mama Sofia Simba, jamani of all the people mlitarajia huyu mama ajibu nini kwenye hili? Kama mlitarajia jibu tofauti kutoka kwake ni wazi kwamba hamjaifahamu vizuri aina ya serikali tuliyonayo.Great thinkers jamani tufanyeje serikali imeshindwa kudeliver hata vitu vidogo kabisa.
 

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
409
Kwa kweli kile kipindi cha BBC kilinitia huzuni sana na hii laxity ya vyombo vyetu inasikitisha zaidi.
 

PatPending

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
490
80
Jamii yetu imekuwa ni jamii ya kibinafsi sana kiasi cha kwamba wadhalimu hawa tunaishi nao mitaani, tunawafahamu na hatuchukui hatua zozote zile hata ile ya kuzungumza nao kuhusiana na udhalimu wao. Mfumo wa utawala wa serikali za mitaa unaainisha uwepo wa mabalozi wa nyumba kumi kumi ambao wanatakiwa kuwa ndio mhimili wa kwanza wa utawala wa sheria katika ngazi ya chini kabisa. Ni vyema watanzania tukahamasika na kuanza kupiga vita uozo huu na mwingine uliozagaa mitaani kwetu.
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,788
9,115
Serikali ya magamba (hasa viongozi) imeshindwa kusimamia watoto wetu na wananchi kwa ujumla kwa kuwajengea mazingira mazuri .
<br />

kila kitu lazima tulalamikie serikali! Kwa swala wa watoto jamii nzima ihusike. Wapo watoto wanatimuliwa kwenye nyumba zao za urithi, wapo wanaoishi sehemu nzuri lakini bado hawapati huduma zao muhimu. Ni wangapi kati yetu huwasaidia wale watoto omba omba wa mtaani japo hela ya kula?! Kiukweli Idadi ni ndogo. Kabla ya kutupa lawama kwa watawala, tujiangalie na sisi michango yetu kwa hao watoto. Tusiwe wepesi wa kuongea na kulaumu.
<br />
 

nandipha

Member
Sep 15, 2011
12
3
Kwa hili la kuwahusisha watoto kwenye biashara ya ngono, nadhani tunakoelekea kama taifa si pazuri kabisa, kuna mambo mengi ya kufanya na ama kurekekebisha hii ni pamoja na sera zinazohusu masuala ya kijamii kwa ujumla. Tukichukulia mfano sera zinazosimamia maslahi ya watoto hasa wale wanaoishi ktk mazingira magumu(yatima na watoto wa mitaani,pamoja na walio ktk familia ila hawapati malezi sahihi,sera hizo haziko wazi ktk kumtetea mtoto ila sana jukumu limeachwa kwa jamii , yaani hakuna chombo maalum ambacho kinabeba jukumu la huyu mtoto 1 kwa 1. Nitamnukuu naibu waziri wa maendeleo ya jamii,wanawake na watoto ktk kikao cha bunge kilichokwisha alikuwa akijibu swali la mb. wa kigoma mh. Kafulila khs nini hatma ya watoto wa mitaani, serikali ina wajibu gani ktk hili? alisema " Jukumu la kumtunza mtoto wa mitaani liko mikononi mwa jamii husika, kwa kuwa mtoto huyu alizaliwa na baba na mama yaani mwanamke na mwanaume toka ktk jamii,hivyo watoto wote wa mitaani wana kwao,serikali inawajibika tu ktk kusimamia vyombo ambovyo vinajihusisha na kuhudumia watoto hawa lakini si kwa kuviwezesha 1 kwa 1". Hapa utaona kuwa watu binafsi na NGO's wana baraka zote khs hawa watoto, na ndiyo maana mtu anaweza kuendesha danguro bila hofu kwa kuwa anakuwa amejificha kwa mwanvuli wa NGO ya kuhudumia watoto wasiojiweza,yatima,wanaoishi ktk mazingira magumu n.k. Maana yake ni kuwa nyingi ya zinazojiita NGO za watoto si hasa lengo lake, ila biashara kuu ni kuuza hao watoto.
 

MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,794
1,985
System nzima ya usalama Tz ipo kuangalia maslahi ya CCM tu. Hapo ingekuwa swala linahusu cdm ungeona moto wake.
Mwito wangu kwa jamii, jamani tuchukue hatua wenyewe. Tunapoona madanguro tusisubiri wazuia maandamano watusaidie. Chukulia kama ndugu yako kalaghaiwa hivyo, hata biblia inatoa adhabu ya mtu huyo kufungiwa jiwe la kusaga na kutupwa kati kati ya kilindi cha bahari.
 

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,718
1,378
Hli tatizo halitaisha bila kupunguza umaskini vijijini na kuongeza fursa za elimu kwa watoto wa kike tena za bure.
 

nkasafari

New Member
Nov 9, 2010
1
0
Mtizamo wangu ni kwamba kuna mfumko mkubwa sana wa wazazi na walezi wasiopenda kuwajibika kwa watoto wanaowalea.Matokeo yake watoto wengi wanakosa makuzi mazuri,wanakuwa hawaza mtizamo/ndoto za maisha yao ya baadaye.Chukulia mfano wamama wa leo unakuta mama anamvalisha mtoto mavazi na urembo ambavyo ni kama mtu mzima.Kisha anamwambia mtoto jichojicho,guuguu. Jamani huu ni mfano tu,lakini haya na mengine yanawahamasisha watoto kuanza ngono mapema.
Pia wazazi/walezi wa leo hatupendi kuchoka (kuwa pamoja na watoto wetu.)Tumewakabithi kwa walezi wengine kama luninga,vibanda vya picha mitaani,makundi ya michezo mitaani tusiyoyafahamu fika,majumba ya majirani tusiyofahamu maadili yao vema,ilimradi sisi tuko bize na ulevi,umbeya,ukahaba,ufisadi na mengine kama hayo.
Utakuta ni saa moja usiku eti mtoto hajarudi nyumbani anacheza kwa jirani. Mtoto tangu asubuhi hadi saa sita/saba mchana anacheza kwenye majumba ya watu. Ofcourse kama watoto wako hawaishi hivyo unaambiwa unaringa,unawafungia watoto. Wapendwa wanaoishi vijijini ndo kabisaa,eti nenda na mwanangu ukamtafutie chochote cha kufanya.Jamani ni vipi wazazi wabaki kijijini na mtoto wamtume kwenye kazi wasiyo ifahamu vema? Wazazi/walezi makini hata kama mtoto anakwenda kufanya kazi za ndani wanafahamu anakwenda wapi.Angalau hawampi mtu wasiyefahamu maisha yake vizuri mtoto wao. Kwa hiyo naamini Familia ndio walinzi wakubwa wa watoto,then serekali. Huu ni mtizamo wangu tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom