Nakushauri ufuge wa kisasa - Layers. wa kienyeji it takes time na faida si kubwa vile unavyodhani - nitafute nikupe ushauri wa bure - meanwhile angalia kazi hii hapa

attachment.php


Hawa wako 900, wanatoa Tray 24 kila siku kila Tray 5000- Chakula chao ni kilo 125 approx Tshs 55,000/-

Mtaji wa kuanzia unahitaji kuwa na not less than 6m before you start production. Kama unataka mchakato mzima sema nitakutumia database yangu.
mkuu help me with this thing you call database. please!
 
Mbona hata 1000 (buku) unatajirika? Ingia sokoni majira ya jioni au alfajiri bei ya bidhaa iko chini.

DAY1
Nunua Tikiti zima la 1000 ( buku), nenda sehemu yenye uhitaji katakata pata vipande 5. Jero isevu.

500× 5= 2500

DAY2
Nunua matikiti 2 kwa 2000 na mia tano itumie tu.

Katakata tena safari hii utakuwa na vipande 10.

500× 10 = Sh. 5000

DAY3
Nenda nunua tikiti 5.

Hapa kila tikiti 1 vipande 5 ×5 = 25
500×25 =7,500

DAY 4
Tikiti 8 kwa nikimaanisha 7500 + 500 uliyosevu DAY1 = 8000.

This time tikiti 8 utapata vipande 40
40 × 500 = 20,000

DAY 5
Tikiti 20
Utapata vipande 100

100×500= 50,000

DAY6
Tikiti 50
Utapata vipande 5 × tikiti 50= 250
Vipande 250 × 500 = 75,000

DAY 7
Nenda kachukue tikiti 75 na fungua kijiwe kingine weka kijana afanye internship.

Hapo utakuwa na vipande 375 ukiuza kwa bei yetu 500 unapata Sh. 187500/=

Wiki inayofuata kuwa constant tu kwamba

Kila siku unachukua tikiti 100 za bukubuku kwa Sh. 100,000. Ile 87,500 isevu.

Tikiti 100 kwa wastani wetu wa kila tikiti moja vipande 5 na unauza kwa 500.

Kila siku utakuwa unauza vipande 500 unapata Sh. 250,000/=.

250,000 × siku 30 (mwezi1) = 7,500,000

7,500,000 × mara miezi 12= 90,000,000

Kipato chako kwa mwaka kitakuwa Sh. 90,000,0000.

Huna mtaji wa 1000 (Buku!) Unasubiri nini kuanza.
Kama vile rahisi
 
Tunauza Vifaranga wa Kuroiler wa wiki moja kwa Tshs. 1,200 wenye chanjo za awali za Marek na Newcastle. Pia tunauza Vifaranga wa Kuroiler wa mwezi mmoja kwa Tshs. 4,000 wenye chanjo za awali za awali za mwezi mmoja za Mareks, Newcastle na Gomboro.

Tunapatikana Kimara Kona ila Tunaweza kukuletea Mahali popote Dar es Salaam.
Kwa Mawasiliano tupigie 0768570655.

Karibu Sana Tufuge Kimkakati.
 
Mpendwa msomaji wetu, yawezekana umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Kulalamika tu vyuma vimekaza haitakusaidia kitu kama hutaki kujiongeza ili uongeze kipato chako.

Yako mambo mengi ya kufanya ili kujikwamua kiuchumi. Usitegemee mshahara wako tu. Mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.

Somo ni dogo tu lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana.
Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo.

Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4.

Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa majike watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga.

Utakuwa na kuku 200 + 25( ulioanza nao) =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

Ndugu msomaji, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000.

Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku baadhi ili upate fedha ya kuwalisha ????

Ukiuza kuku 1000, utabaki na kuku 1000, kati yao tuseme majike ni 750. Ndani ya Miaka 2 maanake ni 750(majike) x 10 = kuku 7500 (uza wengine upate pesa ya kutumia kuwalisha) .

Tuseme sasa utabakiwa na kuku jike 3000 x 10( jike moja ni mayai 10) = kuku 30,000.

Hao kuku 30,000 ukiwauza wote utapata; 30,000x 13000( bei ya kawaida kbsa)= 390,000,000. Je, bado utakuwa masikini? Bado vyuma vitakuwa vimekaza?

Nina uhakika, mpaka mwisho wa mwaka huo wa pili utakuwa umefanikiwa sana kuukimbia UMASIKINI.

Kwenye hayo mamilioni, hata ukitoa milioni 100 kwamba tuseme ndo zimetuka kuendeshea mradi wako, bado utakuwa ni milionea tu. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi.

NB: Ukiyapata hayo mamilioni ya pesa, kumbuka kutoa Zaka, sadaka na kusaidia masikini wasiojiweza ili ubarikiwe zaidi
AMEN!
 
Kama kuna concept wajasiriamali wengi wana overate ni hii hapa, hayo mahesabu yanavutia kuangalia lkn ukiingia kwenye practice utaambulia hasra moja takatifu.
From experience kuna vitu kma magonjwa, chakula, security na mengine. Nilijidanganya Just like mtoa mada, i lost pesa nyingi sana mainly because hatuna experts wa kutosha linapokuja kwa kuku wa kienyeji. Inshort never buy the dogma


Sent using Jamii Forums mobile app
Yeye katoa the positive side of it! Sasa the negative side ISIKUZUIE KUINGIA MZIGONI. Na zaidi ya yote, ukifikiria KUSHINDWA, MAGONJWA, SIJUI NINI HUWEZI KUFANYA LOLOTE. Yule bwana aliyegundua hii "bulb" iwakayo hapo kwenu sasa hivi, alijaribu mara 1999 bila kufanikiwa. Ile ya 2000 ndiyo ikaleta hiyo bulb; lakini yeye hasemi alishindwa mara 1999, anasema alifanikiwa kidogo mara 1999!. Hiyo ndiyo spirit ya wajasiriamali! Usiogope failures, see them as opportunities ili usonge mbele hadi mafanikio AU SIYO!?
 
Nitaweka picha hapa baadae, majuzi tu hapa nimenyoosha mikono kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji! Nilinunua majike ambayo tayari yanataga. nikajengea mabanda safi, hadi mlinzi nikaweka, wakataga mayai yanawateja sana, mengine wakaatamishia nilikuwa kwenye mpango wa kununua incubator, magonjwa nkayadhibiti hakuna vifo cha kuku vya kutisha!

Wamefika kuku 200+ ikaja changamoto ya CHAKULA, kuku wanakula hadi mshahara wangu mapato kiduchuuu! Kwa ufupi nimekula HASARA, sijuhi haya mabanda yangu mazuri nifugie nini! Kuku wa kienyeji sio wa kuchezea, naomba wafugaji wazoefu waniambie wanawalisha nini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom