wandugu =kama ukijifunza changamoto za biashara hasa ufugaji pia ukafanya reserch ya masoko,,

,,ukawa na mtaji wa chakula na madawa,,
Ufugaji hasa wa kuku wa mayai unalipa sana,

,,Mm nimefuga sana,,,kuku wanihitaji usimamizi madhubuti,,Wamenipa faida nyingi sana
 
Mpendwa msomaji wetu, yawezekana umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Kulalamika tu vyuma vimekaza haitakusaidia kitu kama hutaki kujiongeza ili uongeze kipato chako.

Yako mambo mengi ya kufanya ili kujikwamua kiuchumi. Usitegemee mshahara wako tu. Mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.

Somo ni dogo tu lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana.
Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo.

Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4.

Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa majike watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga.

Utakuwa na kuku 200 + 25( ulioanza nao) =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

Ndugu msomaji, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000.

Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku baadhi ili upate fedha ya kuwalisha ????

Ukiuza kuku 1000, utabaki na kuku 1000, kati yao tuseme majike ni 750. Ndani ya Miaka 2 maanake ni 750(majike) x 10 = kuku 7500 (uza wengine upate pesa ya kutumia kuwalisha) .

Tuseme sasa utabakiwa na kuku jike 3000 x 10( jike moja ni mayai 10) = kuku 30,000.

Hao kuku 30,000 ukiwauza wote utapata; 30,000x 13000( bei ya kawaida kbsa)= 390,000,000. Je, bado utakuwa masikini? Bado vyuma vitakuwa vimekaza?

Nina uhakika, mpaka mwisho wa mwaka huo wa pili utakuwa umefanikiwa sana kuukimbia UMASIKINI.

Kwenye hayo mamilioni, hata ukitoa milioni 100 kwamba tuseme ndo zimetuka kuendeshea mradi wako, bado utakuwa ni milionea tu. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi.

NB: Ukiyapata hayo mamilioni ya pesa, kumbuka kutoa Zaka, sadaka na kusaidia masikini wasiojiweza ili ubarikiwe zaidi
Kuku hawaumwi??
Soko tu ni mtuhani mwingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuku wa kienyeni hawajawahi kosa soko.Tatizo ni muda wa kukomaa, maxingira, magonjwa, wezi nk
 
IMG_20190228_090336.jpg
 
Tatizo wana Jamii wengi hawajawahi hata kufuga kuku hata mmoja enzi za utoto wao, sasa inakuwa taabu kweli kweli kuwasaidia mawazo how to go about it.

Mama Joe wala usihangaike kwenda Ruvu kutafuta vifaranga wa kienyeji - kama kweli umeamua kufuga kuku kwa nini usianze na majike 30 na majogoo 3 tu - bei ya hao ukiwapata toka mkoani itakugharimu sh 6,000 kila mmoja Jumla inakuwa 198,000/- Tshs.

Baada ya siku 60 hayo majike yatakuwa na vitoto average 10 kila mmoja = utakuwa na vifaranga 300. Utawanyan'ganya mama zao na kuviweka chumba chenye joto linalotakiwa na utawapa chakula na maji.

Utawaruhusu majongoo yaanze kazi yao immediately baada ya kuwanyanganya vifaranga, then after 2 months hao wanataga tena -- Simple circle!! - after 2 year's utakuwa na hao kuku zaidi ya 1000 unaowataka.
Baada ya kuwanyang'anya vifaranga had majike ni wiki 2 au 3 tu wanaanza kutaga tena
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom