20180417_15_23_14.jpg

Kuku wanahitaji uangalizi wa hali ya juu ili kuwajua changamoto zake,mimi binafsi ukiachilia kufanya ufugaji huu km sehemu ya ujasiriamali pia napenda sana kufuga kuku yaani huwezi amini ni muda mrefu sasa nafuga lakini hata ladha ya kuku wangu au mayai sijui ni bora nikanunue huko lakini sio kuku wangu,naomba km kuna wenzangu humu tunaofuga kuku kuwapenda tukutane tubadilishane mawazo jinsi ya kuwalea hawa viumbe.
Mimi nina changamoto moja naomba nisaidiwe,nimetengeneza viota km hivyo hapo chini na kuku wangu wametaga km hivyo tatizo hapo linakuja,akitotoa kuku mmoja kabla ya wenzake basi wote wanaacha mayai na kuanza kulea vifaranga vya huyo aliyetotoa msaada wa ushauri tafadhali..Ahsante J.f.
gnyozda-dlya-kur-nesushek.jpg
 
UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA

Hii ni simulizi ya mjasiriamali anayeshuhudia alivyobadilisha ufugaji wa kuku kutoka ule wa mazoea na kuwa wa kibiashara. Naamini nawe waweza kunufaika na uzoefu wake.

Safari yangu ilianza baada ya kukutana na mhamasishaji aliyenitia chachu kwamba 10 x10 x 10 you become a millionea! Kwamba ukianza na kuku 10 kila mmoja akazaa 10 na hao watoto na mama zao wakazaa kila mmoja 10 unakuwa millionea! Wakubwa kuongea ni rahisi utekelezaji ukawa mgumu sana! Changamoto kuu aipatayo mfugaji wa kuku wa kienyeji ni kuzalisha vifaranga wengi na kuweza kuwakuza! Bila hivyo kundi haliwezi kukua na kukupa kipato cha uhakika!

Safari ya ufugaji niliianza kwa kununua mitetea 30 na jogoo watatu! Ilibidi nisubiri muda hadi kuku waanze kutaga! Muda ukafika kuku wakaanza kutaga kwa fujo sana! Nilikuwa na banda moja tu ambamo kuku wote walikuwa wakilala humo. Nilitengeneza viota vingi kwa ajili ya kuku kutagia. Asubuhi nilikuwa nawafungulia! Changamoto nilizoanza kupambana nazo kwanza kama mjuavyo kuku tofauti walikuwa wanataga kwenye kiota kimoja! Ilipofika wakati wa kuatamia ikawa kila kwenye kiota kimoja kuna kuku kadhaa wamebanana wanaatamia! Hali hii haipaswi kutokea kwani kuku mmoja anaweza kuwa amejilundikia mayai mengi ambayo hawezi kuyapa joto la kutosha na kuku mwingine anakuwa amekaa kando tu hana hata yai moja. Hii ilibadilika ikawa kero kubwa! Nilijua utotoaji unaweza kuathirika sana!

Ili utotoleshe vifaranga vingi kwa wakati mmoja badala ya kutumia mashine ya kutotolea (incubator), tumia hao hao kuku. Wakianza kutaga kila siku okota mayai na kuyahifadhi mahali salama ili kuku wasiyatie joto! Kuku wengi wanapotaga kwa pamoja hufikia wakati mayai huisha tumboni na unakuta wamelala kwenye viota wakiwa wameatamia mayai yaliyopo au udongo tu! Kuku anaekuwa amefikia kuatamia utamjua kwani ukimshitua haondoki kwenye kiota. Kuku anaetaga ukimshitua hukimbia! Kwa hiyo kama nimepanga kutotolesha vifaranga 100 kwa mara moja nikishagundua kuwa kuna kuku 8 wameanza kuonesha dalili ya kuatamia hapo husubiri usiku ninawawekea mayai amabayo nilikuwa nimeyahifadhi. Ambapo mimi huwekea kila kuku mayai 15. Kwa hiyo kuku 8 hufanya jumla ya mayai 120.

Kwa kuwa banda langu ni hilo moja tu kuku wengine wanaoendelea kutaga walikuwa wanaendelea kutagia kwenye viota ambavyo kuku wengine walikuwa wanaatamia! Hali hii ilikuwa inaleta tabu sana kwani ilikuwa si rahisi kutambua mayai mapya na yenye siku nyingi. Kuondoa shida hii nilinunua MARKER PEN (rangi yoyote) na siku ya kuwawekea mayai kuku ili waatamie niliyachora mduara kuzunguka yai ili iwe rahisi kuyatambua mayai mapya. Huo mchoro hauwatishi kuku na hakuna dosari yoyote. Kwa hiyo kila siku jioni ninapokuja kuokota mayai yaliyotagwa nilikuwa pia nakagua kila kiota cha kuku walioatamia na kuondoa mayai mapya. Kumnyenyua kuku anaeatamia na kuondoa yai haileti shida yoyote!

Kuku akifikia wakati wa kuatamia ukamnyima mayai hawa wanatabia kuendelea kung'ang'ania kuatamia, hapo ilibidi kutengeneza JELA! Watu wengine wana mbinu tofauti kumwachisha kuku asiatamie! Mbinu ya kumtia kuku stress inafanya kazi nzuri sana! Jela inaweza kuwa ni Tenga, au Box kubwa au chumba kidogo kilichopo. Ukimfungia kuku JELA bila maji wala chakula kwa kutwa mbili siku ukimfungulia akili yake huwa ni kutafuta chakula tu hakumbuki kurudi kwenye kiota! Njia hii ilifanikiwa sana na ilifanya kuendesha shughuri zangu bila bughudha! Kuna wakati JELA ilikuwa na kuku kibao hivyo unapaswa kutengeneza kibanda cha JELA. Hawa kuku wakitoka JELA hutaga mapema sana amabapo bila hivyo wangekuwa wanaatamia. Pia kuku wakishaatamia kwa muda wa siku 10 nilikuwa nayapima mayai ili kubaini kama kuna mayai yasiyoweza kuanguliwa! Ni rahisi sana kama una Tochi! Ukimulika yai Kwa kulizungushia vidole kiganjani kama ni yai zima linakuwa na giza kama ni yai bovu linapitisha mwanga kama yai lililotagwa siku hiyo!

Jinsi ya kuzungushia vidole yai, tengeneza duara kwa vidole vyako na dole gumba kisha pachika yai katikati ya duara ili mwanga wa tochi upenye kwenye yai! Kwahiyo unaweka tochi inayowaka chini ya yai na hii ifanyike gizani au ndani ya chumba chenye mwaga mdogo. Kadri ya yai linavyokaribia kutotolewa ukilimulika huwa na giza zaidi! Ukimulika mayai toa mayai yasiyoweza kutotolewa maana hayo hutumia joto la Mama bure!

Mayai viza! Mayai yasiyototolewa kwangu ni hazina kubwa kwani huyatumia kuwawekea kuku ili wasubiriane! Yaani inaweza kutokea kuku wameanza kuonyesha dalili ya kuatamia ili aishituke akaahirisha kuatamia huwa namlundikia hayo mayai yasiyoweza kutotoleshwa! Hufanya hivi hadi idadi ya kuku ninaotaka waatamie ikitimia, siku hiyo huondoa mayai feki na kuwawekea siku moja kuku wote mayai halisi ya kuatamia! Hakika nilikuwa ninasisimka sana inapofikia siku ya siku kuku wote wanamwaga vifaranga kwa siku moja!!

Ufugaji huu wa kuharakisha kuwa na idadi kubwa ya kuku huendana na kutenganisha vifaraga na mama zao. Watu wa mjini hufanikisha kirahisi sana kwa kutumia taa za umeme kuwapatia joto vifaranga! Wengine wanaweza kutumia majiko ya mkaa! Ni wazi kwamba ukiwanyang'anya mapema vifaranga Mama zao ndani ya siku 10 huwa wanaanza kutaga mayai tena, ambapo bila hiyo angeendelea kulea vifaranga wake hadi miezi 3. Kwa kumnyang'anya vifaranga kuku hutotoa vifaranga wengi kwa mwaka! Sasa kazi ndiyo ipo hapa! Ukinyang'anya vifaranga mama zao halafu ukawarundika vifaranga wenye umri tofauti sehemu moja hapo ni balaa! Vifaranga wenye umri mkubwa huhakikisha vifaranga wadogo hawali! Vifo vingi vinavyosababishwa na lishe duni hutokea kwa vifaranga kutokana na ubabe unaotokea kwamba wale wenye umri mdogo hawashibi! Kwa hiyo ni muhimu kutotolesha vifaranga wote siku moja ili uwakuze pamoja!

Kwa mazingira yasiyokuwa na umeme nilifanikiwa kukuza vifaranga kwa kutumia mama zao! Kwenye kuatamisha kila kuku nilimpa aatamie mayai 15 baada ya kutotoa nilikuwa kila kuku mmoja ninamkabidhi vifaranga 30! Kuku alikuwa anatandaza mabawa yake na kuwafunika wote! Vifaranga wakirundikana ndani ya mabawa ya mama yao wanazalisha joto la kutosha na wala si kwamba wanategemea joto la Mama yao tu! Kwa kufanya hivi vifaranga waliototolewa na kuku 8 walilelewa na kuku watatu au wanne tu! Kwa hiyo wale kuku wengine 4 au 5 walipelekwa JELA ili kuondoa usumbufu na baada ya kutoka JELA baada ya siku 10 wanaanza kutaga mayai!

Nilivyoendelea kufuga baada ya kuona kuwa kuku wanaoatamia wanapata usumbufu sana kutoka kwa kuku wanaoendelea kutaga, banda langu la kuku nililigawa kukawa chumba na sebule! Nitaeleza wakati ukifika nilivyojenga mabanda yangu. Kwa hiyo chumbani niliweka viota na ndiko ambako nilikuwa nawaweka kuku wanaoatamia ili wasibughudhiwe kabisa na kuku wenzao. Mlango wa kuingia chumbani nilitengeneza geti la mianzi iliyopigiliwa karibu karibu kuzuia kuku kupenya. Hapo sebuleni ndiko kuku wote watagao na wasiotaga walikuwa wanalala, kwa hiyo kulikuwa na viota vingi ambavyo juu yake nilikuwa naviwekea kizuizi kwa kutumia Mabanzi ya mbao ili usiku kuku wengine wanaposimama juu yake wasichafue kwa kinyesi chao kwenye viota.

Viota hivi nilikuwa navitengeneza kwa kuweka kutenganisha (partitions) kwa kutumia tofari za tope, zenye saizi kama ya matofali ya kuchoma. Kwa hiyo kwa kuambaa ukuta nilikuwa nalaza tofari nne chini kwenda juu, nilifanya hivyo kila baada ya upana wa futi moja, juu ya hizo tofali ndiyo niliweka Banzi! Ndani ya hivyo vijivyumba nilitifua umbo kama kijibeseni na kuweka Majani laini ili mayai yatulie yasisambae. Huko chumbani wakati wote kulikuwa na chombo chenye chakula na chenye maji! Hakuna kuku kutoka na hakuna kuku wa kuwaingilia! Ilikuwa ni incubator TOSHA! Nilikuwa nawaona kuku kama wananishukuru kwa kuwatengenezea mazingira safi maana walikuwa hawabughudhiwi na walikuwa wanashiba chakula vizuri tu!

Nitaeleza siku nyingine juu ya harakati zangu za kutengeneza chakula na changamoto nilizokutana nazo! Huko chumbani nilikuwa nimetandaza carpet la nyasi; kando kando ya kuta zote kulikuwa na viota ambavyo nilivizamisha ndani ya hilo kapeti la nyasi nadhani mtanielewa! Ninaposema carpet la nyasi, ni nyasi tu nilizisambaza kwa unene wa kama sm 15 au nchi sita! Kwa hiyo kipindi hawa kuku wanapokuwa wanaatamia nilikuwa nazuia wengine wasiatamie hadi hawa watakapototoa! Kwa hiyo mayai yanayopatikana wakati hawa wengine wanaatamia nilikuwa ninakula na mengine kuuza maana mpango wangu ilikuwa kutotolesha mara moja tu kuku mia kwa mwezi! Hii ndiyo Incubator yangu ambayo nilikuwa ninatotolesha vifaranga 100 kwa siku moja!! Kwa kuwa nilikuwa ninajukumu pia la kulea kuku utotoleshaji nilikuwa ninaudhibiti uendane na miundombinu yangu ya kulea kuku na vifaranga.
========
 
View attachment 747567

View attachment 747566
SOMA HIYO POST YANGU (JAPO NI C&P) HUENDA UKAJIFUNZA CHOCHOTE
 
Hayo ma kuku ya kisasa ndo zao
Yanadeeeeka km ni mdogo wa nanii!
Mm nafuga wa kienyeji,
Lkn mm pia napenda tu ile kuwaona na kuwahudumia najiskia raha,
Huwa naumia sana nikiona kuku kaumia,
 
Mkuu nina shida ya mayai ya kuku chotara.nipo Dar
 
SOMA HIYO POST YANGU (JAPO NI C&P) HUENDA UKAJIFUNZA CHOCHOTE
Inawezekana nisiwe sahihi lakini mbona hiyo post unayosema kuwa ni ya kwako inafanana kila kitu na post ya mdau Kubota ? Kama ni kweli ni ya Kubota huoni ni vizuri kama ukampa credit ?
 
soma post number 3309 utaona maneno haya C&P>>> Copy and Paste
 
Habari zenu wadau. Kutoka na vyuma kukazaa ile mbaya MTU mzima niliamua kuwekeza kwenye ufugaji wa kuku nimekutana na changamoto mbali mbali ,ila hii niliyokutana siku za karibuni ndo amenifanya kuomba msaada kwa wazoefu humu ndani JF. Kuku wawili wanataga mayai sehemu moja na yamechanganyika idadi yapo matano je? Nini nifanye ili kila kuku aendelee kutaga eneo lake bila kuathiri utagaji wao .tusaidiane tafadhari kuuliza si ujinga.
 
Wakuu habarini za muda huu naomba kufahamishwa ni kuku aina gani bora kufuga ambao watakupa tija na faida kati ya kuku wa kienyeji pure
Kroiler kuchi na kuku wa mayai
Nomba kupata mchanganuo kwa wanaofahamu kuhusu kuwafuga hawa ndege na faida zake zikoje na garama
Nawasilisha asanteni
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom