hangera kwa hapo ulipofika.....pole kwa kupoteza kuku 80.

ndui ya kuku ni miongoni mwamagonjwa yanayo sababishwa na viruses na huwa hayana tiba ili kuepuka ndui nakushauri uwape chanjo ya ndui kuku wako Mara tu wanapo timiza miezi miwili,hakikisha chanjo unanunua kwa wauzaji wanao aminika ili usije uziwa chanjo fake au iliyokwisha muda wake.

pia uwe makini kuna ugonjwa unafanana na ndui kiasi fulani na wengi wanachanganya na ndui,ugonjwa huo ubasababishwa na kuku kukosa vitamini A huu ugonjwa unatibika kwa kuwapa kuku vitamini A pia na kutibu vidonda na macho kwa kutumia ayodini,maji ya vuguvugu yaliyochanganywa na chumvi pamoja na mafuta ya alizeti.

kuhusu mbegu kubwa ya kienyeji pure unaweza kufuga kuchi.


kama kuku wako unawaachia wajitafutie chakula wenyewe kuhusu fomula ya chakula isikuumize kichwa sana pumba inatosha kwa kuku wakubwa ila sivibaya kama utawapa dagaa n.k kama vinapatikana kwa unafuu lakini kwa kuku wadogo kilicho changanywa ni muhimu sana hasa cha kununua ni vizuri kama utapata cha kiwaandani kama utanunua tofauti na cha kiwandani basi ununue kwa mtu ambae anaaminika na yuko competitive .
 
Kama ndo unaanza bas andaa banda lako kabla ya kuleta vifaranga piga V-RID kuua viroboto n kunguni kisha weka taa za joto na uweke vifaranga ndani. Siku ya kwanza kama umewasafirisha umbali mrefu lazma wapate maji ya glucose na chakula na wale ambao hawajiwez wanyweshe

Utaratibu wa chakula
Week 1-6 wape broiler starter, week 6-8 wape broiler finisher. Week 8- 16 wape growers na week ya 17 kuendelea ni layers

Utaratibu wa chanjo
Kabla hujanunua hakikisha anayekuuzia amewapiga chanjo ile ya kifaranga mwenye siku moja. Siku ya 7 chanjo ya Newcastle, siku ya 14 chanjo ya gumbolo na siku ya 28 rudia chanjo ya gumbolo baada ya miezi Miwili wapige chanjo ya ndui

Ni hayo tu karibu kama una swali
Mtoa mada anaulizia chanjo ya ndui kwa vifaranga, wengi wenu mnakuja na majibu ya kinadharia ya kuchanja kifaranga akiwa na miezi miwili wakati huo ameshapata ndui na amekufa utamchanjaje?
 
Mtoa mada anaulizia chanjo ya ndui kwa vifaranga, wengi wenu mnakuja na majibu ya kinadharia ya kuchanja kifaranga akiwa na miezi miwili wakati huo ameshapata ndui na amekufa utamchanjaje?

sasa ulitaka tuje na majibu ya kivitendo?kama ujaelewa ni bora kuuliza.

mlolongo wa chanjo unaendana na umri wa kuku ambapo siku kifaranga kinapototolewa udungwa chanjo ya marek,baada ya siku saba chanjo ya kideri,baada ya siku 14 gumboro na mwisho baada ya wiki 6 hadi 8 chanjo ya ndui,hapo hautarudia chanjo zote isipokuwa chanjo ya kideri ndio utarudia kila baada ya miezi mitatu zoezi hilo ni endelevu.
 
Unaweza kufanikiwa iwapo vikishatotolewa vikusanye vyote, lets say hao 100 wametoto wote vifaranga 7 (minimun number) utakuwa na vifaranga 700.

Watunze kwenye chumba chenye joto la wastani ili wasipate baridi, wanunulie chakula (Chic starter ) 50kgs, unaweza ongeza soya iliyosagwa 5kgs hivi changanya fresh.

Nunua OTC plus na any multivitamins (dawa za packet) hizi ni za unga, zichanganye pamoja kisha uwe unawapa vifaranga hvi kwenye maji ya kunywa.

Wiki ya kwanza - chanja Gombolo
Wiki ya Pili chanja Newcastle.
Wiki ya tatu rudia Gombolo
Wiki ya nne rudia Newcastle
Wiki ya sita chanja Ndui (Pox) (Muhimu sana )

Wakifika wiki ya 9, watoe bandani waanze kutafuta msosi wao wenyewe, unaweza kuwa unawaongezea bumba ili wakue vizuri zaidi.

Muda huo mama zao watakuwa wameshatotoa tena, kwa hiyo unaweza kuwa na kuku zaidi ya 6,000 at the end of 2018.

Kama utauza kuku kwa bei ya kutupwa ya 15,000 basi ndugu utakuwa na 15,000 times 6,000 = 90m.

Kazi njema, ila siyo kazi ndogo kufikia hapo, unahitaji kufanya kazi kubwa mno hasa kwenye utunzaji na ulishaji.
Ni jambo jema ku-share na wengine maarifa na fursa, hasa na wale wenye moyo wa uthubutu!
 
Kwa Arusha wanunuzi wa kuku wa kienyeji na mayai ya kienyeji wa jumla wako wapi?
 
Nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji, bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje.
Kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri, pros and cons etc.

By the way, nimeanza na Jogoo mmoja, ila natarajia kuongeza kuku within a week, projections ni kuwa na kuku 1,000, hapo ndio nianze kuuza, matarajio yangu ni kuuza via interent - hapa nalenga watu wa DAR, ambao wako bize, I can do delivery maofisini within city center, na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni, e.g Mwenge Junction, Morocco Petrol Station, etc. Malipo via M-Pesa, SMS banking pia na mahoteli.

Sitarajii faida ya haraka, naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii, au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.
Ufugaji wa kuku
 
samahan wakuu, bei ya kifaranga cha layers sasahivi ni kiasi gani, kwa kifaranga kimoja
thanks.
 
Habari naomba kusaidiwa namna yakuanza kufuga kuku kuanzia kifaranga mpaka hatua ya mayai au kuuzwa...na list ya madawa na chakula
 
Kama hujawahi kuwafuga usiongee maana unaweza amka ukawakuta wote wamekufa
Acha tu mkuuu mimi nina kuku na nguruwe ...mvua ili nyesha ukuta uka anguka nguruwe nikawala hifadh banda zur jiran na banda la kuku bwana eheeee...waka vunja banda lao kuvamia la kuku waka bomoa mabati na skia makelwleee vimejikusanya eneo moja nguruwe akipitisha mdomo ana toka na kuku wa tatu nilitaman kulia nikawa na jikuta na zungumza mwenyewe tu,nika bakisha kuku 80 kat kat ukiamka ukikuta kuku ameanguka swla la kawaida Mungu mwema wamebaki 80
 
Mimi kuku wangu hawalei vfaranga manake nawachukuwa mara tu baada ya kutotolewa... Nilicheka sana pale rafiki yangu alipoona nachukua vfaranga toka kwa mama kuku ingali yupo kwenye kiota chake akasema niwaache wanyonye japo kwa wiki moja...
 
Back
Top Bottom