Kubota
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 532
- 1,089
hivi mama hawadonoi vifaranga ambavyo si wake kweli!!
Swali lako lilishaulizwa na mdau huko nyuma, ni kwamba kuna baadhi ya kuku ni wakali sana na huwa hawakubali kabisa kupokea kuku wa wengine, huwadonoa vifaranga wasiokuwa wakwake na kuwaua kabisa, lakini si kwamba anawatambua kuku wake bali ukichelewa kuweka vifaranga vya nyongeza tena ukiweka anashuhudia huwashitukia pengine kwa harufu yao na hapo hufanya maangamizi. Unapomuongezea kuku vifaranga vya ziada unashauriwa umwekee usiku.
Kwa hiyo ni wajibu wako kuwatambua kuku wakali usiwape kamwe jukumu la kulea vifaranga. Kuna kuku ambao ni wapole sana, inabidi uwatambue na uwatumie kwa kazi hiyo ya kulea vifaranga bila kubagua. Kwa hiyo kuku wakali hao ni budi wabakie kutaga tu wala wasipewe fursa ya kuatamia.