Jamani msaada kwenye tuta....

Nina kuku wa kienyeji kama 20 hivi, tatizo ninalopata kwa sasa ni ugonjwa wa kuku kuvimba macho, na mwishowe anapofuka. Wameshakufa wawili.
Nimepata dawa chanjo ya kuweka kwenye maji na pia dawa ya macho (eye drops) lakini naona haiko effective.

Anayefahamu chanzo na tiba please saidia
 
Habari wadau wote wa kuku wa kienyeji, nilipotea kidogo weekend. Poleni kwa magonjwa na vifo ila kwa michango ya Kubota kwenye matibabu nadhani ametutia nguvu wengi sana,kifupi mie sijawahi kufuga hawa wa kienyeji kibiashara hivyo najifunza mengi sana hapa kwa michango yenu. Nami nina sijui ni vinyoya wako wiki ya 4 sasa hivyo najifunza mengi sana hapa. Napenda kuongezea kwenye magonjwa huo wa macho inawezekana kweli ni ukosefu wa vitamin A maana hata binadamu ukosefu wa vitamini A huathiri macho...kumbe pia unatibika sikujua Kubota unatufaa sana.
Mimi miti ya muarobani iko mingi eneo letu na sasa ivi inatoa mbegu nyingi ila bado mbichi nitaanza kufanya zoezi la kusiokota nilikuwa nawapa majani tu au kuwachemshia wadogo kwenye maji. Niatjitahidi kufuata ushauri wako kwani na mie nilianza kuwaza kufuga kwa wazo la Gazeti ingawa nimenunua tu vifaranga, mbinu zako zitatufaa wengi.
 
msome Kubota hapa ujasiriamali anaelezea hilo tatizo
 
Mama Joe bila shaka hapa utakuwa umechukua elimu tosha,,,,,,,,tumia ipasavyo na hakika utarudi jukwaa hili na majibu mazuri sana na nikutakie kila la Kheri Mama Joe

Habari wadau wote wa kuku wa kienyeji, nilipotea kidogo weekend. Poleni kwa magonjwa na vifo ila kwa michango ya Kubota kwenye matibabu nadhani ametutia nguvu wengi sana,kifupi mie sijawahi kufuga hawa wa kienyeji kibiashara hivyo najifunza mengi sana hapa kwa michango yenu. Nami nina sijui ni vinyoya wako wiki ya 4 sasa hivyo najifunza mengi sana hapa. Napenda kuongezea kwenye magonjwa huo wa macho inawezekana kweli ni ukosefu wa vitamin A maana hata binadamu ukosefu wa vitamini A huathiri macho...kumbe pia unatibika sikujua Kubota unatufaa sana.
Mimi miti ya muarobani iko mingi eneo letu na sasa ivi inatoa mbegu nyingi ila bado mbichi nitaanza kufanya zoezi la kusiokota nilikuwa nawapa majani tu au kuwachemshia wadogo kwenye maji. Niatjitahidi kufuata ushauri wako kwani na mie nilianza kuwaza kufuga kwa wazo la Gazeti ingawa nimenunua tu vifaranga, mbinu zako zitatufaa wengi.
 
Last edited by a moderator:
Kubota
Mama Joe
guta
Mama timmy

Hebu litazameni hili lililonipata jana baada ya Mi nikiwa Safari niliporudi nikakuta kuku mmoja mtetea amekufa ndani ya banda na hata hakuonyesha dalili yoyote na leo nikajaribu kutafuta watalaam nikakuta leo ni siku ya mapumziko na nipo nikachukua maamuzi ya kuzika.

Je? Kwenu haya yanatokeaga? Na hata nimejaribu kumpigia guta RETI na bila ya mafanikio baada ya simu zao kutopokelewa.

NAOMBENI USHAURI WENU WANDUGU!

Asanteni sana!

Pole mkuu @LiverpoolFC kwa kupoteza mtetea, kwa kweli sina jibu la moja kwa moja zingatia ushuri wa kubota .
 
Kubota pole na shughuli ya kila leo!
Hakika tu pamoja mwanzo mwisho na vifaranga wote wanaenenda vema kabisa sijaona mabadiliko mabaya kwao kwa kweli na ninaendelea kuwapa ile starter ndiyo lishe yao na mama yao ndani ya banda!

La zaidi ninaloomba ndugu zangu Kubota Mama Joe guta Mama timmy RETI jamani hakuna anayejua dawa ya kuwapatia kuku mara wanapoanza kuharisha choo kahawia?
Maana naona tangu juzi jana nawaona katika dalili hiyo sana!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa kweli kuwaweka na mama zao inasaidia joto ila kuna risk kupata magonjwa kubwa sana, kifupi hawa wakubwa wakifika umri fulani wanakuwa wamepata immunity ya magonjwa mengi ingawa wanakuwa na vijidudu kwenye damu, au choo ila hayawadhuru tatizo ikitokea hawa vifaranga wamekutana na vinyesi vya wakubwa tu uambukizo kwao unakuwa ni ugonjwa. Hii inatokea kwa hata kuchanganya vyombo vya maji, ku share banda au kwa miguu ya watunzaji toka nje au banda hili kwenda hili. Ndo maana kuhofia hilo kuna wengine wanashauri kuanzia wiki ya pili hata kama hawaumwi wapewe Amprolium dose ndogo huwakinga na ugonjwa wa coccidiosis, ingawa sina uzoefu na hawa wa kienyeji ila hii ni kwa wa kisasa tumekuwa tukifanya hivyo ukichelewa na hasa kama uambukizo ukitokea inabidi watibiwe. Kutokana na dalili zako naweka hapa dalili kutoka kitabuni lakini nakushauri jieleze vizuri pharmacy wataelewa ni ugonjwa gani
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Kuharisha damu (Coccidiosis)
Kuzubaa
Kushusha mabawa kama
mtu aliyevaa koti.
Kupoteza hamu ya kula.
Kuharisha kinyesi chenyerangi ya kahawia au kilichochanganyika na damu.
Kuharisha damu
Manyoya kutimka
Kupauka kwa upanga na ndevu
Kudhoofika na hatimaye huwezakufa.
Tiba:
Ugonjwa huo unawezakutibika kwa amprolium, salfa na ESb3 kama hatua
za kuudhibitizitachukuliwa mapema
Kinga kuepuka unyevunyevukatika matandiko.
Kuwatenga kuku wanaoonyeshadalili za ugonjwa.
Kinga kwa kutumia coccidiostat.
Kutibu kwa kufuataushauri wa wataalam wa mifugo.
My take, wakati tunasubiri ushauri wa wengine nakushauri ondoa maranda au uchafu wowote bandani, ukitibu watibie kuku wote, kila yakilowa maranda ondoa weka mengine jitahidi kuwasogeza hata wagonjwa kwenye dawa, mwaka jana mie iliwapata broiler walichanganya vyombo vyao na hawa chotara wakubwa, ukijitahidi wanapona hasa vile hawa ni kienyeji wako strong. All the best

Pole sana mkuu LiverpoolFC , hii kazi ni ngumu sana lakini tutafika tu, matatizo yangu kama yako.
Nami nasikitika sana kuku wangu wametotoa vifaranga wachache sana mmoja katotoa vifaranga 2 kati ya mayai 12, wapili katotoa vifaranga 4 kati ya 12 watatu katotoa naye 4 kati ya 12, sijajua tatizo ni nini, maana niliwasubirisha ili waatamie mayai kwa wakati mmoja, lakini ilichukua muda wa siku 4 wote wakawa wanaatamia siku ya tano nikawawekea mayai 12 kila mmoja. Maotokeo ndo hayo, ila mmoja bado anaatamia nategeme week ijayo naye atotoe yeye sikumsubirisha na wala sikuyatoa mayai yake kama wale wengine , ngoja nisubiri matokeo.

Jambo jingine naona kuna ugonjwa bado unasumbua kuku, vinyoya vimepata ugonjwa kama vitatu vimeshakufa, na kimoja bado kinaendelea kuugua. nimevipa madawa mpaka navionea huruma. pia kuna mmoja kati ya hao wakubwa naye kinyesi chake ni cha kuharisha damu, huyu nimemuoana leo asubuhi, mpaka sasa niko njia panda yaani nafikiria niwamalize kuku wote nianze upya kabisa. Inaweza kuwa ni sababu yakutotoa mayai machache.
Ngoja nijaribu kwanza dawa aliyopendekeza Mama Joe, au kama anaushauri mwingine atumwagie tafadhari.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa kweli kuwaweka na mama zao inasaidia joto ila kuna risk kupata magonjwa kubwa sana, kifupi hawa wakubwa wakifika umri fulani wanakuwa wamepata immunity ya magonjwa mengi ingawa wanakuwa na vijidudu kwenye damu, au choo ila hayawadhuru tatizo ikitokea hawa vifaranga wamekutana na vinyesi vya wakubwa tu uambukizo kwao unakuwa ni ugonjwa. Hii inatokea kwa hata kuchanganya vyombo vya maji, ku share banda au kwa miguu ya watunzaji toka nje au banda hili kwenda hili. Ndo maana kuhofia hilo kuna wengine wanashauri kuanzia wiki ya pili hata kama hawaumwi wapewe Amprolium dose ndogo huwakinga na ugonjwa wa coccidiosis, ingawa sina uzoefu na hawa wa kienyeji ila hii ni kwa wa kisasa tumekuwa tukifanya hivyo ukichelewa na hasa kama uambukizo ukitokea inabidi watibiwe. Kutokana na dalili zako naweka hapa dalili kutoka kitabuni lakini nakushauri jieleze vizuri pharmacy wataelewa ni ugonjwa gani
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Kuharisha damu (Coccidiosis)
Kuzubaa
Kushusha mabawa kama
mtu aliyevaa koti.
Kupoteza hamu ya kula.
Kuharisha kinyesi chenyerangi ya kahawia au kilichochanganyika na damu.
Kuharisha damu
Manyoya kutimka
Kupauka kwa upanga na ndevu
Kudhoofika na hatimaye huwezakufa.
Tiba:
Ugonjwa huo unawezakutibika kwa amprolium, salfa na ESb3 kama hatua
za kuudhibitizitachukuliwa mapema
Kinga kuepuka unyevunyevukatika matandiko.
Kuwatenga kuku wanaoonyeshadalili za ugonjwa.
Kinga kwa kutumia coccidiostat.
Kutibu kwa kufuataushauri wa wataalam wa mifugo.
My take, wakati tunasubiri ushauri wa wengine nakushauri ondoa maranda au uchafu wowote bandani, ukitibu watibie kuku wote, kila yakilowa maranda ondoa weka mengine jitahidi kuwasogeza hata wagonjwa kwenye dawa, mwaka jana mie iliwapata broiler walichanganya vyombo vyao na hawa chotara wakubwa, ukijitahidi wanapona hasa vile hawa ni kienyeji wako strong. All the best

Mama Joe:
I salute you kwa kulichambua tatizo la maambukizi toka kwa kuku wakubwa, pia kwa kutoa solution!
LiverpoolFC: Mama Joe kamaliza maelezo yafanyie kazi, na mimi nilishakusisitizia huko nyuma kuwa huwa inatolewa
preventive treatment kwa vifaranga kwa kutumia antibiotics, ndiyo hizo amezitaja Mama yetu. Take action!!
 
Mheshimiwa Guta pole kwa kuuguza na kupotelewa kinyoya. Naona tatizo lako linafanana na LiverpoolFC nadhani fanyia kazi kwanza ushauri wa Mama Joe, kuhusu tatizo la kutotoa inategemea lishe, jogoo, urefu wa muda unaohifadhi mayai, mazingira unayohifadhi mayai kabla hujawawekea kuku na pilika pilika za kwenye viota wakati wa kuatamia labda kuku hawatulii shauri ya kufukuzana kwenye viota au shauri ya chawa n.k. Je hali halisi ikoje, hebu dadavua.
 
Poleni sana wadau ila tusonge mbele, Kubota asante kwa pongezi. Niliona umetaja tiba mbadala nyingi je mafua ya kuku yanayo kinga au tiba unayoifahamu?
 
Back
Top Bottom