nitafanya hivyo hadi kuku wafikishe miezi miwili ambapo nitawatoa kwenye hilo banda na kama kuna vifaranga wengine nimezalisha basi wanakuwa wanaachiana mabanda .

sasa hapo kuku wangu wanakuwa na umri wa miezi miwili wenye afya nzuri na ukuaji mzuri.Hapo huwa na machaguo miwili kuna wakati huwa naamua kuwaachia wajitafutie chakula na kuku wazazi isipokuwa watakula chakula cha ziada na kuku wazazi ambacho ni pumba tu.kuku hawa naweza kuwauza wakiwa na umri wa miezi 5 na kuendelea

Lakini kunawakati nawafungia kwenye uzio nilio eleza awali.kwenye huo uzio watashinda mchana usiku wataingia kwenye banda, ili asubuhi iwe rahisi kuku kuingia kwenye uzio bila kuku wengine kuingia nao. nilicho fanya kwenye Banda la kuku nimeweka mpaka ambao hauruhusu kuku kuchanganyika pia kuku hawa wanakuwa wa mwisho kuingia na wa kwanza kufunguliwa.

humo ndani ya uzio naweka vyombo vya maji na chakula,chakula hapa huwa nawapa kwa utaratibu na formula kama awali kule bandani lakini nitaongeza kipimo kwa siku, kuku mmoja atakula gm 6 kwa wiki tatu za mwanzo wiki ya nne gm 7 kwa siku.kuku hawa ninaweza nikawauza baada ya kutimiza miezi 3 hadi 3.5.

chanjo ya ndui inatolewa baada ya kuku kutimiza miezi miwili.mimi ninacho fanya kama nitakuwa na lengo la kuwauza kuanzia miezi mitatu basi siwachanji ili kupinguza gharama na kama nitawaacha hadi miezi mitano wajitafutie chakula hapo huwa nawachanja.
 
Kama unasoko la hao kuku fanya uende vijijini kusanya idadi unayotaka uuze but kufuga kuku wakienyeji uwauze kwa ajili ya nyama ndani ya wiki 6 inabidi utumie muujiza
 
Wiki ya tano hadi ya sita au kutegemea na hali ya hewa kama ni ya baridi sana na hawajaota manyoya unaweza waacha hadi week 8!
 
Habari ndugu zangu, ninaomba kufaham kama suala la kufuga kuku wa kienyeji kwa muda mfupi kama wanavyofugwa kuku wa kisasa wa nyama linawezekana?. Nahitaji kufuga kuku wa kienyeji kuanzia wakiwa wana siku moja na wakifika wiki 6 au 8 nianze kuwauza. Tafadhali kwa yoyote mwenye uwelewa naomba anisaidie
Nenda vijijini kusanya ila itachukua muda maana inabidi ufatilie minada.
Utatunza kwa muda ili uuze.
Je una soko tuwasiliane tufanye biashara.
 
Nashukuru nyote kwa ushauri wenu na mawazo yenu. Nadhani sasa ni muda muafaka wa kubadili mbinu na kuelekeza katika mawazo mapya.
Ahsanteni!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom