ukiwa unarudi njoo na PICHA za hayo mabanda
Ngoja nisubir umalizie ndo niuulize yangu pia USHAURI
 
kaka safi,lakini hayo yote umefanya kwa mtaji wa shilingi ngap?

gharama ambazo nilitumia kununua baadhi material ya awali, chakula na madawa kuanzia kwa uzalishaji wa mwanzo ambao niliingia kama kujifunza ili nipate picha halisi ya ufugaji ni sh.k5 hata hivyo vitu vingine nilitumia nguvu zangu vingine nilitengeneza kutokana na local available material badala ya kununua.
 
ningeomba wanajamvi mnoti pembeni maswali yenu kisha baada ya kumaliza niulizeni nitajibu.nahitaji kuwasilisha mbinu zote leo leo inshaallah .
 
Me baada ya kuona napoteza vifaranga vingi sana kwa mwewe nimeamua kuwafungia mama na mtoto kwenye mabanda sasa nawauliza wadau inachukua muda gani hawa kuku kutokuweza kudhulika na baridi nimtoe mama yao ili aanze kutaga tena? Kinachonipa faraja sasa ni takribani week tatu vifaranga 25 hakuna kilichokufa hata kimoja naombeni uzoefu.
 
Me baada ya kuona napoteza vifaranga vingi sana kwa mwewe nimeamua kuwafungia mama na mtoto kwenye mabanda sasa nawauliza wadau inachukua muda gani hawa kuku kutokuweza kudhulika na baridi nimtoe mama yao ili aanze kutaga tena? Kinachonipa faraja sasa ni takribani week tatu vifaranga 25 hakuna kilichokufa hata kimoja naombeni uzoefu.
unaweza ukawatoa hata siku ya kutotolewa tu ila ukawa unawawekea joto mbadala kwa taa ya umeme au au mkaa kwenye kigai
 
aya tuendelee..baada ya kuku wazazi kutaga mayai huwa nayakusanya na kila yai naandika tarehe ambayo limetagwa kwa kutumia penseli au peni.

kuna kuku ambao watakuwa wametaga siku nyingi kuliko wengine hivyo watakua wanaanza kulalia ninachofanya ni kuchagua mayai ambayo ayajavuka siku kumi tangu kutagwa kisha nitawachukua hao kuku na kuwatenga chumba kisicho na usumbufu nitawawekea kila mmoja mayai yasiyozidi kumi na mbili.

chumba ambacho natumia nikile cha vifaranga wa wiki nne ambacho muda wote kinakuwa na chakula na maji ya kutosha pia akina usumbufu wa kuku wengine ambao wangetaka kutaga kwenye viota ambavyo vinamayai yanayo lalaliwa.Idadi ya kuku wanao lalia inategemea na bajeti yangu ya mwezi huo .

kwakuwa kuku wote nitawawekea mayai siku moja hivyo baada ya siku 21 hadi 22 mayai ya kuku wote yataanguliwa.

katika chumba cha kulelea vifaranga wadogo nimeweka box ambalo huwa linatumika kusafirishia pikipiki mpya,ndani ya hilo box na weka matandiko ya pumba mpunga kiasi ,vyombo vya maji na chakula pia na bulb ya w100 au w60 inategemea na msimu.

vifaranga hao nawaweka humo kwa muda wa wiki nne katika hizo wiki wiki ya kwanza nawapa chanjo ya kideli na wiki ya pili chanjo ya gumbolo.Chakula ambacho huwa na wapa hawa vifaranga wa umri huu ni chakununua ambacho nanunua sh1000/kg.

baada ya vifaranga kumaliza mwezi nawahamisha kwenda banda lingine nililisema awali ambalo ni kubwa kidogo na halina taa za joto lengo nikuwapa nafasi na kuruhusu vifaranga wengine watumie hilo box.

chakula kwa muda ambao watakaa humo huwa nachanganya mwenyewe kutokana na local materials kwa kufuata formula ya uchanganyaji. nitatuma formula hiyo baadae.
 
Ukumbuke kueleza jinsi ya kumtambua kuku wa kuhatamia mayai na atafanya hivyo mara ngapi kabla ya kumpa uhuru naye aanze kutaga!
 
Habari wanajamvi na poleni kwa uchovu wa pasaka. bila kuchelewa turudi tena kwenye mada yetu.

kipomo cha chakula cha hao kuku wanao tafuta umri wa miezi miwili kwa siku huwa nawapa gm4/kuku kwa wiki ya kwanza na pili kwa wiki ya tatu na ya nne na wapa gm4.5/kuku.mfano nina kuku labda 20 kama ni wiki ya kwanza nita wapa gm80 kwa siku.

Ulishaji wa hawa kuku huwa nitofauti kidogo na vifaranga wadogo.vifaranga wadogo nawawekea chakula wanakula muda wote usiku na mchana ila kwa hawa wakubwa nagawa share ya chakula ya siku hiyo katika nusu mbili,nusu moja nawapa wale asubuhi wakimaliza hicho chakula siwapi iliyobaki kwa muda huo pia siwaachi wakae bila kula ninacho fanya nachukua chakula chochote nafuu nawaning'inizia waendelee kudonoa taratibu hadi mida ya saa tisa hapo nawawekea nusu nyingine wamalizie mgao wa siku.chakula cha kuning'iniza kinaweza kikawa kabichi nzima,mboga za majani,majani mf.michunga,matikiti pori yaliyo katwa vipande nk.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom