Biashara ya Sungura imejaa utapeli wa hali ya juu sana

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,235
Kinadharia ufugaji wa sungura kibiashara ni jambo lenye kuleta matumaini sana, lakini kiuhalisia ni biashara yenye utata mkubwa sana kwa hapa kwetu Tanzania.

Makampuni mengi yanayohamasisha ufugaji wa Sungura ni kama yale makampuni ya uuzaji bidhaa kimnyororo (Supply Chain companies) ambako faida inapatikana kwa kuongeza washiriki kwenye biashara husika.

Unapoingia kwenye ufugaji wa kibiashara wa sungura, Makampuni mengi yaliyoko hukuuzia sungura wa kuanzishia mradi, kukujengea banda, kukuuzia chakula cha sungura mengineyo utajijua mwenyewe, kwani ahadi nyingi za kutafutiwa soko la sungura huwa ni Uongo wa kupindukia ulipangiliwa kiakili sana

Nadhani wale wanaotaka kufuga sungura kibiashara wajaribu wenyewe kwanza kutengeneza soko la nyama ya sungura kabla ya kufuga sungura hao kwa wingi.

------------------

Soma maoni ya mdau juu ya jambo hili

Si kwamba ufugaji wa Sungura ni utapeli, no ni uwezo wetu wa kuwaza umeisha
 
Biashara zooote za wanyama wadogo kama kuku bata mende sungura ni mkakati wa kitapeli kuwavuta wengi waingie ili inspirational speakers wapate hela, wauza vyakula na madawa ya wanyama hawa wapate hela mengine wanakuachia wewe mwisho wa siku kama utabahatika utakuwa na wingi wa hao wanyama lakini huna pa kuuzia kurudishia hela.

Heti: kilo moja ya mende China ni laki tano??? Jamani muogopeni Mungu. Sasa ingia mkenge uanze kufuga hao mende utauziwa mende mmoja wa mbegu 15,000 nautaambiwa unatakiwa uanze na mende 10 kwa kiasi cha 150,000.

Hiyo semina ya jinsi ya kufuga mende unalipia kiingilio kwa mtu ni 50,000 wakipatikana 20 inspirational speakers kaishaula. Utauziwa chakula special cha mende kilo 35,000 na utaambiwa mpaka wakue unatakiwa ununue kilo 10.

Utaambiwa ununue madawa ya kufanya wazaliane, kuwakuza na kuwafanya wawe na uzito, n.k. Amaaa kweli nyakati hizi za mwisho watu wanapigwa na kubaki mafukara wa kutupwa
 
Utaingia mkenge ukibahatika kuwakuza changamoto huna pa kuwauza gharama ya matumizi mamillion utakuwa umeangukia pua!
Jamaa Sungura walipofika 50 ndipo kiswahili toka kwa ile kampuni iliyomuuzia sungura kwa ahadi ya kutafuta soko kilipoanza. Mpaka wanafika 200 hakuna soko na Kampuni ikawa imeshafunga shughuli zake hapa Iringa na kumwachia mzigo wa kuwasiliana na wafugaji wenzake mama mmoja ambaye naye walishamtapeli .
 
Jamaa Sungura walipofika 50 ndipo kiswahili toka kwa ile kampuni iliyomuuzia sungura kwa ahadi ya kutafuta soko kilipoanza. Mpaka wanafika 200 hakuna soko na Kampuni ikawa imeshafunga shughuli zake hapa Iringa na kumwachia mama mmoja ambaye naye walimtapeli mzigo wa kuwasiliana na wafugaji wenzake.
Umenifungua akili kwa kiwango cha hali ya juu kumbe ni utapeli huu, binafsi huwa sikosi vipindi vyako pale Ebony fm
 
Hatari sana. Ni mwendo wa kutengeneza fursa.
Kuna jamaa mwingine anasema ununue kuku 100 kwa laki sita, alafu baada ya siku 120 Ela yako utarudishiwa Mara mbili. Sijajua Kama Kuna ukweli hapa.
 
Dhuluma, " Huendi mbinguni " Hili songi liacheni tuuu kuna matapeli wasomi hawaendi mbinguni hakika.
Ni ujuha kupigwa kirahisi namna hiyo! Hivi utaambiwaje ufuge kitu ambacho hujui soko lake wala hujawahi kusikia soko lake hata siku moja? Mtanzania anaanguka kwa kukosa maarifa na kupenda mteremko.

Sasa kama sungura wana soko nchi za Ulaya wafugaji wake watashindwaje kuwafuga? Mbona wanafuga kuku, ngombe, nguruwe etc tena kwa wingi na bei zake ni rahisi kuliko hata huku kwetu?
 
umenifungua akili kwa kiwango cha hali ya juu kumbe ni utapeli huu,binafsi huwa sikosi vipindi vyako pale ebony fm
Da! Nimesikitika. Mbona wabongo mko warahisi sana kudanganyika jamani? Ni elimu, ni upeo wa kufikiri, ni kupenda vya bure au ni nini? Hili la kufuga sungura ukifikiria kidogo wala huwezi kukubali upuuzi kama huu.
 
Pia wanawadanganya mkojo wa Sungura deal!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimefuatilia sana kenya nikapata taarifa sahihi kwasababu wataalamu wetu kila ninapouliza nilikosa majibu yakueleweka. Hapa ni kweli kama unafanya kilimo hai au organic, una N,P na K ya kutosha sana na unaweza kuspray kwenye mmea wenye shida kuua wadudu.

Ni nzuri sana kwa wanaofanya kilimo cha mbogamboga, ni soil conditioner na rafiki mzuri sana wa udongo ila
Ukibugi kwenye uchanganyaji unaua mmea jumla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo tambarare ndugu yangu. Watu wanadanganywa kwa vitu vya kutumia logic ndogo tu...
Nakumbuka huku kwetu Iringa watu walilimishwa "Paprika" aina fulani hivi ya Pilipili mwisho wa siku hata leo hii ukiwakumbusha wanabaki kucheka tu. Mambo ya kupanda miti ya mlonge yalichukua hela za watu wengi sana.

Sijui ni kwa nini watu huwa hawaulizi mambo ya msingi kabla ya kushiriki kwenye kujitapeli.
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom