Biashara ya simu used, nifanye nini ili nisipatwe na hatari ya simu zilizoibwa

emmarki

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
682
918
Kwenu wajuvi wa sheria za biashara.

Ninafanya biashara ndogo ya kuuza na kununua simu used, zilizotumika hapahapa jijini Dar almaarufu simu za mkononi..

Changamoto kubwa kama mjuavyo huwa kuna simu za wizi, muuzaji hawezi kukuambia ni wizi na ni vigumu kutambua kwa sababu kiteknolojia hakuna namna ya kutambua labda kwa simu km iphone ambazo inaweza kuwa iPhone disabled. Ishu ni hizi za kawaida kama infinix, tecno, Samsung na nyinginezo.

Nataka nijiweke kwenye mikono salama kisheria. Nahitaji kuwa na vielelezo gani ili nisiangushiwe jumba bovu na wajanja zaidi yangu.
 
Omba risiti na taarifa za anaekuuzia ikibidi mrekodi.
Ili kesho ukibanwa na wazee wasiharibu mwili waambie aliyeniuzia ni huyu hapa lakini utoachiwa kirahisi hadi mwizi au muuaji apatikane ndipo utachomoka ukiwa shahid namba 2 wa tukio lolote la uhalifu.
Pana mtu alinunua simu used kwa mtu kwa laki moja ikamtoka milioni 3 plus kukaa ndani miezi 6 Ili kuua soo. Milioni 3 bora angenunua iphone.
Simu ilikuwa inakichwa cha mtu yeye ni mnunuzi na sio muhusika wa tukio
 
Kwenu wajuvi wa sheria za biashara.

Ninafanya biashara ndogo ya kuuza na kununua simu used, zilizotumika hapahapa jijini Dar almaarufu simu za mkononi..

Changamoto kubwa kama mjuavyo huwa kuna simu za wizi, muuzaji hawezi kukuambia ni wizi na ni vigumu kutambua kwa sababu kiteknolojia hakuna namna ya kutambua labda kwa simu km iphone ambazo inaweza kuwa iPhone disabled. Ishu ni hizi za kawaida kama infinix, tecno, Samsung na nyinginezo.

Nataka nijiweke kwenye mikono salama kisheria. Nahitaji kuwa na vielelezo gani ili nisiangushiwe jumba bovu na wajanja zaidi yangu.
Kwa Tanzania bado sana ila soon hili litamalizika, kila simu ina IMEI numbers hivyo kwa nchi za wenzetu simu zote zinakuwa linked na makampuni ya simu, hivyo ukiiba huwezi kuitumia nchi hiyo, hivyo soon na sisi tutafika huko.

Nimelipa 4.5 kumchomoa mtoto wangu kwenye msala wa simu ya wizi, iliibiwa Arusha.

Unagharimia kila kitu kuanzia polisi wa Arusha, tameka Dar 14 days, kisha polisi wana collude na aliyeibiwa aseme aliporwa millions ili kukukomoa na kugawana na polisi!. You have pay vinginevyo wanamng'ang'ania dogo waende nae Arusha!.

Kiukweli nilisikitika sana kwasababu dogo has everything, including a good phone, lakini he wanted more!.

Kiukweli mchuma janga hula na wakao!, hili jambo limetutesa kwa kutusumbua, mwisho wa siku niliongea na aliyedai kuibiwa nikamwambia nakubali kulipa hiyo 4.5 but I know it's not true, nililipa na yakaisha ila naamini na yeye karma itakuwa imeisha mtake care kushirikiana na polisi kuwakamua Innocent victims wa simu za wizi.
P
 
Pole pia baadhi ya mapoli upiga dili na watu wauze simu then wanaifatilia unapewa kesi,wanavuta,masimu mengi yamejaa ubaoni kwao
 
Kila Kazi Ina changamoto naamini njia nzuri ni kuwa na wateja wenye risiti yaani Mtu awe na risiti akuuzie then na wewe ndo utafte Mtu umuuzie , kwa hapa Daslama simu za wizi ni nyingi Sana.
 
Kwenu wajuvi wa sheria za biashara.

Ninafanya biashara ndogo ya kuuza na kununua simu used, zilizotumika hapahapa jijini Dar almaarufu simu za mkononi..

Changamoto kubwa kama mjuavyo huwa kuna simu za wizi, muuzaji hawezi kukuambia ni wizi na ni vigumu kutambua kwa sababu kiteknolojia hakuna namna ya kutambua labda kwa simu km iphone ambazo inaweza kuwa iPhone disabled. Ishu ni hizi za kawaida kama infinix, tecno, Samsung na nyinginezo.

Nataka nijiweke kwenye mikono salama kisheria. Nahitaji kuwa na vielelezo gani ili nisiangushiwe jumba bovu na wajanja zaidi yangu.
Siku ukiunganishwa kwenye lupatikana na simu iliyotumika kwenye mauji ndio utaelewa ukubwa wa hili jambo. Kuna watu wamesota sana.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom