opportunist2012
Member
- Feb 8, 2012
- 92
- 8
Kutokana na matokeo mabovu ya form IV mwaka 2011,shule za private zimekosa wanafunzi wa kidato cha tano mwaka huu (2012) kwa idadi wanayoihitaji.Baadhi ya shule imepokea mpaka wanafunzi watatu mpaka 10.Hali hii imetokana na matokeo yasiyoridhisha ya kidato cha tano ingawa serikali imejitapa kwamba kiwango cha ufaulu kimeongezeka.Kilichoongezeka hapa ni division IV na kupungua zero.Wamiliki wa shule hizo za private wameonekana kuchanganyikiwa kwani hata hao wanafunzi wachache wenye div1 mpaka III wanagombeana na shule za serikali.Kuna baadhi ya shule za serikali zimekosa kabisa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano,baadhi ya shule hizo zimeaghirisha kuchukua baadhi ya michepuo kutokana na matokeo mabovu ya kidato cha nne.Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2012 watatangazwa hivi karibuni.