Biashara ya Radio: Uliza swali lolote linalohusiana upate jibu.

Radio Producer

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
724
295
Wadau,

Leo naomba kwa wale wenye maswali kuhusu biashara ya radio watupie hapa tutakuwa nao pamoja.
Mfano kuhusu:-
- Vipindi
- Vifaa
- Gharama za kuansiah radio yako
- Human Resource
- Mitambo
- Ufundi
- Soko n.k


Radio Producer.
 
Ina gharimu kiasi gani kuanzisha radio yenye mafasa umbali wa kilomita 100?
 
Mkuu Logo, inategemeana na mazingira uliyopo na jinsi ulivyojipanga mpaka sasa. Mfano unaweza kuwa tayari una majengo ya studio yanahitaji uboreshaji mdogo tu, vifaa vya studio havizidi Tshs 8,000,000.00 vikitoka nje tukikutengenezea package kutoka hapahapa bongo kwenye Tshs 3,000,000. na Trnsmitter ya Watts 1000 ndo utahitaji kuwa nayo ambayo itacost $5,995/=

Karibu.
 
Gharama za TCRA zenyewe zinategemeana na aina ya radio unayotaka kuanzisha.

•Kwani kuna aina ngapi za radio ukiacha AM na FM?
•hyo Transmitter ya Watts 1000 inaweza kurusha ndani ya km100 kutoka center(station) pasipo kua na repeater hapo kati? Je ukiondoa mnara wa center,je kuna minara mingine ya kuweka kwa ajili ya transmission of signals?
•Je kuna gharama nyingine unalipa TCRA ukiondoa license? Hapa nauliza coz nasikia kurun 24hrs radio ni tofauti na wale wanaozima saa sita usiku.
•Gharama za matangazo/udhamin yapo vipi?
 
•Kwani kuna aina ngapi za radio ukiacha AM na FM? Tunaposema aina za radio zipo kuu tatu "1. commercial radio 2. Public Radio (Zinamilikiwa na mashirika au makanisa) 3. Community radio (radio za jamii) Kwenye fee structure ya TCRA bei zake zinatofautiana kulingana na Aina za radio.
•hyo Transmitter ya Watts 1000 inaweza kurusha ndani ya km100 kutoka center(station) pasipo kua na repeater hapo kati? Je ukiondoa mnara wa center,je kuna minara mingine ya kuweka kwa ajili ya transmission of signals? (Kitaalamu huwa ni kwamba Watts 1000 huwa ni sawa KM 100 Ground level yaani maeneo radio inasikika bila bughudha ila hali hii inategemeana na miinuko ya milima katika eneo ulilopo kama upo kwenye milima mingi inakukinga unaweza usifike 100KM lakini kwa Watts 1000 unafika km 100 bila shida na bila booster yoyote ni kutoka center.
•Je kuna gharama nyingine unalipa TCRA ukiondoa license? Hapa nauliza coz nasikia kurun 24hrs radio ni tofauti na wale wanaozima saa sita usiku. (Gharama zingine zipo ndogo ndogo sana kama za application kama 15,000/= na suala la kuwa hewani masaa 24 na zile zinazozimwa lenyewe lina misingi yake mingine siyo ada kuongezeka hapa)
•Gharama za matangazo/udhamin yapo vipi? Inategemeana na mkoa uliopo, mfano mkoa kama wa Mtwara tangazo kuruka mara moja ni kati ya Tshs 40,000-100,000, lakini kwa mikoa ya Mbeya hiyo psa unaweza kurusha kwa wiki nzima kila siku mara tatu, Udhamini inategemeana na makampuni pia yapo mengine yanalipa mpaka milion 5 kwa mwezi nakuaendelea.


Karibu
 
Mkuu nimekuwa nafuatilia mada zako za redio na hatimaye naanza kupata interest. Nitakujia na maswali muda mchache ujao. Natoka kidogo. Thanks a lot.
 
Mkuu Safi sana ...nahitaji Kuwa Fundi Mitambo wa Redio Stations...Nipo Tabora huwezi kunifundisha hata kwa njia ya INTERNET?
 
ina hitaji vifaa gani na inaghalimu kiasi gani ili radio isikike online??
 
Mkuu Safi sana ...nahitaji Kuwa Fundi Mitambo wa Redio Stations...Nipo Tabora huwezi kunifundisha hata kwa njia ya INTERNET?

Ufundi Mitambo wa radio ndugu yangu ni kitu simple lakini vitu kama hivi ni vigumu sana kujifunza kwa internet si kwamba haiwezekani inawezekana lakini itagharimu sana na pia huwezi kupata ujuzi mapema na itakuwia ugumu sana wakati mwingine. Karibu ututembelee Radio Consult Company Limited
 
mkuu nlikua nikitafuta msaada kwa wataram kama nyie sasakwangu najua itakua rahisi mm nimetengeneza internet radio shida kuubwa internet sijui nitumienini au kifaa gani napia naitaji niwatembelee najifunze ujuzi zaidi
 
mkuu nlikua nikitafuta msaada kwa wataram kama nyie sasakwangu najua itakua rahisi mm nimetengeneza internet radio shida kuubwa internet sijui nitumienini au kifaa gani napia naitaji niwatembelee najifunze ujuzi zaidi
 
Back
Top Bottom