Biashara ya kuchezesha pool table inalipa?

Sunshow

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
1,140
391
Nimewaza biashara ya kufanya nikapata wazo la kununua pool table mbili ambazo nitaziweka sehemu mbili tofauti. Mwenye kujua bei ya pull table nzuri na imara anijuze na pia mwenye kuijua biashara hii vizuri msaada tafadhali.
 
Ushauri wangu hyo biashara sio nzuri kwa sasa hasahasa hapa dar, na kwa uchunguz wangu wa harakaharaka imeathiriwa na uanzishwaji wa mfumo wa usafiri wa bodaboda ambao umeajiri vijana wengi sana, tena wale wacheza kamari a.k.a kamongo
 
Ushauri wangu hyo biashara sio nzuri kwa sasa hasahasa hapa dar, na kwa uchunguz wangu wa harakaharaka imeathiriwa na uanzishwaji wa mfumo wa usafiri wa bodaboda ambao umeajiri vijana wengi sana, tena wale wacheza kamari a.k.a kamongo
Asante, ngoja tusikie pia maoni ya wadau wengine.
 
Wadau,sina details za kina sana juu ya hii biashara,ila wengi wanaisifia kuwa inalipa,nataka niifanyie Iringa mjini,kwa wanaojua tafadhali mnijuze mtaji wa hii biashara,changamoto zake hasa usimamizi na manufaa yake,nawasilisha
 
Sehemu nyingi tu hizi pooltables zinatenezwa hapa dar...
Kuna sehemu takikati ya riverside na mabibo hostel, pia maeneo flani karibu na ubungo kibangu...
Niliulizia bei wakaanza na 1.2 M lkn kuna maelewano...

ahsante mkuu nilikuwa sijui
sasa kwa wazoefu wa hii biashara minimum ya mauzo kwao ni bei gani
 
ahsante mkuu nilikuwa sijui
sasa kwa wazoefu wa hii biashara minimum ya mauzo kwao ni bei gani


Mkuu Majigo , sina uzoefu sana katika hii biashara, lkn kuna kipindi niliongea na dogo flani ambae alikua msimamizi wa hiyo pooltable, alidai kwa siku za kawaida anachezesha Token 70-100...
Tokea 1 ina-worth around 200, so on dairly basis the minimum amount ni 14'000/=
 
Last edited by a moderator:
JE unatamani kuwa tajiri na hujui ni BIASHARA gani ufanye nipigie sim namba 0715 416464 nikupe mchanganuo na uanze kupata pesa za kukutajirisha
 
Heshima mbele mkuu,

Mkuu ni kwa muda sasa natamani kufanya biashara hii ya pool tables, kwa kifupi ninajamaa yangu ana bar nje kidogo ya mji, na vijana wengi wa eneo hilo hawana shughuli maalum (jobless na day workers) mara nyingi wako kwenye bar yake wanakunywa na wengine wanaangalia TV tu, ni bar yenye watu wengi kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 usiku na kwa kifupi ilianza kama duka tu, kutokana na watu kuongezeka ikabidi aanzishe ka bar kwa pembeni, ili vijana wapate huduma ya vinywaji na kuangalia Tv ili kupoteza muda na kubadilishana mawazo, kama tunavyojua nchi zetu maskini hazina sehemu za mapumziko, sasa hii ndiyo sehemu ya makutano.

Sasa hebu nifahamishe kuhusiana na hii biashara ili nijue nini cha kufanya.

Asante
 
Hivi nyie mmekuja Dar lini?
Hakuna kitu hapo mtaibiwa mjini.

Hata Samaki ukivmua unamuonyesha kwanza chambo kabla ya kumvua.
Namna ya kumpika anajua mpishi mwenyewe

Nyie mngekuwa mnataka maelezo zaidi ya biashara hizi,wasiliana na KENICE POOL Company.
Watakupeni kila kitu,sio kila kitu kuangalia kwenye upande ambao mtu ana personal interest zake.

Halafu heading eti Tajirika,we umeona nani duniani katajirika na Pool table zaidi ya kupata pesa ya kula na kuendesha familia kwa kiwango cha chini.

Na declare interest kwamba mie ninayo hapa mtaani,na unapata pesa ya kawaida tu ya kupunguza ukali wa maisha.
Na pia kuwa makini maana wapo vijana wanatabia ya kucheza kamari kwa kuwekeana pesa katika mchezo huo,mwisho wa siku ni laana kwa mwenyepool table na wachezaji.
Inalipa zaidi ikiwa nje ya Bar,siku hizi vijana wengi bar wanaenda kuangalia tu bar gani inamadem wazuri basi.Na ukiangalia vijana wengie wanaishia kwenye viroba juu kwa juu,na wenye nazo muda wa kupindisha viuno kwenye pool table sio kivile wengi kama vile wameisha uchoka.
Ilikuwa zamani wakati mchezo unaingia na hakuna pa kuchezea zaidi ya bara ndio maana watu wakaona kwamba lazima uweke bar.
Ila ukweli ni kwamba hata mazingira ya kawaida unalipa vizuri sana.We muuliza mtu wa Bar akuambie mapato ya miaka ya 2004 hadi 2007 na sasa ni tofauti baada ya mchozo kuzagaa hadi mitaani.
Muhim ni kuangalia sehem yenye utulivu.
Na bora zaidi kuweka sehem ya wazi,mie nilikodi kiwanja cha mtu kwa mkataba kwamba akitaka kujenga naodoka.
Sasa niliweka sakafu chini na bati juu,kisha chini nikaweka tiles za vipande,halafu nikafanya kuigeuza iwe kijiwe cha biashara.
Yaani nauza chipsi,juices,supu,maji bites kibao na mambo mengine.Ili niwe naokota mia mia.
Ila mwanzo ni gharama kidogo ila inalipa kiasi kwa kushirikisha biashara zaidi ya moja.
Naamini sie wote wengi kila mmoja mtaani kuna kiwanja cha mtu hakijajengwa au sehem ya mtu ipo wazi.
Sasa unaweza kumuomba uibadilishe iwe kibiashara zaidi,sio kuweka turubali juu kama uwanja wa fisi.

Sasa ukimuomba mwenye uwanja na ukamuambia dhamira yako basi hakukatalii kabisa,muhim heshim ya mchezo huu ni jinsi unavyoiweka na kuiandaa kwa ujumla.ukiweka kihuni basi wateja wako watakuwa wahuni na ukiiweka kiheshima kidogo basi hata wale wahuni watakuwa wapole na kufuata utaratibu kutokana na mazingira.
 
Wadau Mimi ni graduate mhanga wa ajira serikalini,lakini nilifanya kazi na kampuni moja na mkataba kufikia ukomo.

Ivi karibuni nategemea kupata mafao yangu.Nimewaza biashara ya kufanya ambayo haina risk kubwa nikaona pool Kama inafaa

Wadau nlikuwa naomba mwenye uzoefu na hii biashara anisaidie kunielekeza Bei ya pool mpya, iliyotumika pamoja na wastani wa mapato.

Natanguliza shukrani zangu za dhati..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom