Biashara ya nguo kwa mtaji wa Tsh. milioni 1

Disaba

Member
Jun 16, 2015
34
17
Habari za humu ndani ndugu zangu.

Katika hali ya kuchakarika na kutafuta maisha hatimaye leo nimekuja na wazo langu ambalo nahitaji msaada toka kwenu wadau au kama kuna wazo zuri zaidi ya hili unaweza pia nishauri.

Nilikuwa na wazo la kufanya biashara ya nguo za wadada na watoto, kwa mzoefu au mwenye uono zaidi. Je mtaji wa Tsh. milioni 1 unatosha? Kama unatosha nini kifanyike hadi kufikia step ya kuweka mzigo sokoni?

Location niliiona iwe Mbagala Rangi 3 (ila Rangi 3 na huu ujenzi wa barabara panachangamoto sana) au hata K\Koo.

NAOMBA KUWASILISHA
 
Watu hawajaja hapa kwa kuwa nawe si mchangiaji.
ID yako ya 2015 lakin unaonekana c wa kujichanganya.

Hata nyuzi zako zina wachangiaji wachache sana.

Tembelea nyuzi zinazohusu biashara.
Ulichoandika tayari kishajadiliwa sana.
Nilikua cjui kumbe kama huwa huchangii kwenye maada yoyote kuhusu wenzio naww ukitoa uzi wako hawachangii!! Kama kijijini kwetu kama huwa huendi msiban naww cku ukifiwa hawaji
 
Watu hawajaja hapa kwa kuwa nawe si mchangiaji.
ID yako ya 2015 lakin unaonekana c wa kujichanganya.

Hata nyuzi zako zina wachangiaji wachache sana.

Tembelea nyuzi zinazohusu biashara.
Ulichoandika tayari kishajadiliwa sana.
Kush nikuambie kitu, watu hutofautiana

Kuna akina sisi Karucee ni headache tangu wadogo.... Darasani ni noisemakers tangu nursery school.

Ila kuna wengine who are comfortable in their solitude. Hawajichanganyi not because hawataki but it's because of their nature.

Some are shy, some just can't interact with others.

So please tumuelewe. And sometimes it is better to just read and mute rather than offend people or insult them.

If you can assist her please do... It you can send her a link, go ahead. The good you do will come back to you in one way or the other.
 
Habari za humu ndani ndugu zangu.

Katika hali ya kuchakarika na kutafuta maisha hatimaye leo nimekuja na wazo langu ambalo nahitaji msaada toka kwenu wadau au kama kuna wazo zuri zaidi ya hili unaweza pia nishauri.

Nilikuwa na wazo la kufanya biashara ya nguo za wadada na watoto, kwa mzoefu au mwenye uono zaidi. Je mtaji wa Tsh. milioni 1 unatosha? Kama unatosha nini kifanyike hadi kufikia step ya kuweka mzigo sokoni?

Location niliiona iwe Mbagala Rangi 3 (ila rangi 3 na huu ujenzi wa barabara panachangamoto sana) au hata K\Koo.

NAOMBA KUWASILISHA
Huu mwandiko wa kike kabisaa. Mkuu hongera KWA kupata mtaji wengine tunasubiri tujitolee kwanza
 
B
niliwish za dukan ila kama kwa uzoef wako unaona mtaji huo hazitosh pia unaweza nishaur niingie kwa za mtumba. frem kulipia kwa huo mtaji niliona ni ngumu. hivyo nilitaka kujua kama kuna mwenye uzoef kwa wale wanaopanga bidhaa kwenye meza utaratibu nao unakuaje!
Binafsi nipo Mbagala rangi 3.nakomaa na vifuniko vya asali..hapa mbagala kuna matabaka..kama za dukani nenda kule biasi...kama mtumba mkali njoo hapa akiba bank...kwa huo mtaji kodi meza
 
Niliwish za dukan ila kama kwa uzoef wako unaona mtaji huo hazitosh pia unaweza nishaur niingie kwa za mtumba. frem kulipia kwa huo mtaji niliona ni ngumu. hivyo nilitaka kujua kama kuna mwenye uzoef kwa wale wanaopanga bidhaa kwenye meza utaratibu nao unakuaje!
Sorry for late reply.....za dukani utapata ila utapata mzigo mdogo...... Za mtumba zinauzika sana hasa za kina dada tena unaweza anza na za mtumba za laki 3 tu alafu laki 3 nyingine wekea viati vya kina dada.....vingi vinauzika kwa elfu 5 yani kariakoo unanunua 2500 unakuja uza 5000......

Laki 4 ibaki pembeni kama akiba na nguo ufanye pointing kuliko kununua belo, sehemu za kufanyia pointing kwa dar ni ilalaboma na karume huko nguvu yako ya kuchagua ndio itafanya upate nguo nzuri kwa bei ya kuanzia 1000 - 4000 kwa ilalaboma kama ukiwahi alfajiri....

Utaratibu wa kupata meza, unategemeana na mkoa, ila sehemu nyingi ni nguvu ya kuwahi na kujuana na majirani zako kibiashara na tozo wanalipa 2000 kwa siku hiyo ni Moro.....kwa iringa huku ni bure kabisa kwa machinga......

Ukiwa smart utatoka mapema, kupitia nguo zakike na viatu kulaza 50 itakuwa kawaida na ninauhakika katika hili....

nimekushauri upoint ili usipate maronya mengi pia uzoee deals zinaendaje ili ukizoeana na unaeona anapata mabelo mazuri na muaminifu akushike mkono ..... Changamoto zipo ila zinasolvika na ni ndogondogo sana.....

Mfano kipindi cha baridi hiki mikoako ukipeleka trench coats almaarufu kama koti za kikorea utauza sana kwa bei ya 5000 na zile ndefu mzuri 7000 hadi 8000.....
 
Niliwish za dukan ila kama kwa uzoef wako unaona mtaji huo hazitosh pia unaweza nishaur niingie kwa za mtumba. frem kulipia kwa huo mtaji niliona ni ngumu. hivyo nilitaka kujua kama kuna mwenye uzoef kwa wale wanaopanga bidhaa kwenye meza utaratibu nao unakuaje!
Pia za mtumba zinauza na kutoka kwa uharaka hasa za akina dada kuliko za dukani......pia nilichosahau ni rika...yani Nguo za mtumba angalia sana unataka uwauzie wa rika gani usiwele nguo nyingi za wanafunzi wa sekondari utakosa pesa...wewe weka nguo za wanachuo na wadada wakubwa kiasi pesa ipo pale mkuu.....

my testimony: kipindi cha corona nilikuwa nyumbani office ilifungwa basi nikaenda dar nikapoint nguo ilala boma nilienda saa 9 usiku wakafungua saa 11 hivi nikapoint nguo nzuri sana za kike kwa 1500, 2000 skin jeans 3000 wanapofungua mabelo zingine hadi 500 blouse nzuri tu......skin jeans nlinunua kama 20 tu sikuwa na uhakika nazo ila ajabu niliuza skin jeans hadi sio vizuri kwa bei ya 6500 nikajilaumu kwanini sikuchukua skin tu....

so Skin kwa wanachuo zinauzika sana na zile track zao kama wanazovaa wasanii kama Nandy wewe ziweke humo utanishukuru badae.....

Nilishindwa endelea sababu ofisi ilifunguliwa na nikashindwa kumanage muda vizuri wa biashara na kazi. Nilitumia mtaji wa laki 330 tu including nauli
 
Back
Top Bottom