Biashara ya ngozi na mazao yake hapa Tanzania na ngambo

Mshawa

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
776
306
Wasalaam wana Jf,

Ndugu zangu nina ombi kwenu hasa kwa anayefahamu uwepo ama (Viability) ya hii biashara ya ngozi, nimehamasika sana
kusindika ngozi ikiwa ni njia moja wapo ya kuiongezea dhamani ngozi za wanyama kama ngombe, mbuzi, n.k ila sina mwongozo ama uelewa wowote wa wapi nitapata soko hasa hapa Tanzania, nilipo ngozi huwa zinatupwa ama kuuzwa kwa bei nafuu, isipokua sina uelewa wa soko na namna ya kuwapata wateja wa ngozi iliyokamilika (leather).
regards Mshawa.
 
Naiamini sana Jf bado nina matumaini inawezekana wewe ama yoyote aliye na ufahamu wa hii biashara atatushauri ......
 
Masoko mazuri ya ngozi yako nje ya nchi, ukiangalia kwenye net, wapo wanunuzi wengi wananunua kwa bei nzuri.
unachotakiwa kufanya ni kutafuta vibali vya serikali ili uweze kupeleka nje. usikubali kabsa kutumia njia za panya kwani ni
hatari kwako. kupeleka nje ngozi ni gharama sana hivyo kama una mtaji tafuta watu mfanye pamoja usitake kufanya peke yako. mimi nina milioni tano kama utakuwa tayari tunaweza kushirikiana na kufanya pamoja. ubarikiwa na Bwana
 
mwanangu, fungua kiwanda hapa bongo cha leather tanning, tengeneza viatu, mikoba and the like.. and export finished goods only.
bonge la business idea.
Hivi Bata bado wako sokoni?
 
Hata mimi ninafikiria sana kufanya biashara ya aina hiyo lakini sina uelewa juu ya biashara ya nje bwana felix naomba uni pm ili tuongee biashara coz mimi nina mtaji wa kama milioni kumi
 
Naona watu kadhaa hapo mko na mtaji sio haba, nami niko na 4m, kwa nini tusikutane pamoja, then tukatafuta consultancy kuhusu hii biz, au hata tukaungana kama yawezekana
 
na mi niwekwe kwa kuongeza mil 5 ninazo. kwa kuanzia tufanye case study ya wakenya wanafanyaje maana wananunua ngoz kwa bei ya juu ambazo hazijasindikwa.
 
mwanangu, fungua kiwanda hapa bongo cha leather tanning, tengeneza viatu, mikoba and the like.. and export finished goods only.
bonge la business idea.
Hivi Bata bado wako sokoni?
Hawezi fungua wakati hana huo ujuzi au mtaji

A Philanthropist|£conomist|Business Consultant|Agricultural&Natural Resources Economics Analyst.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom