Biashara ya ngono dar

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
Habari wakuu:

Sijajua mikoa mingine, lakini kwa ninachokiona dar es salaam kinatia kichefuchefu,imekuwa kama kazi nyingine za kuingiza kipato hazipo kwa mabinti zetu lakini sio tu mabinti wadogo lakini majimama mazima hayaoni haya kujidharirisha..

Unakuta katoto kadogo ka miaka 15 kanaenda na jamama la miaka arobaini na kitu ili mradi bwana mdogo awe na 2000/=

mida ya saa 2 usiku utakuta sehemu nyingi za vichochoroni hasa karibu na nyumba za wageni wadaDa wamejianika kujiuza..

Jamani jamii tunaridhika na hili,,hivi tunapambana na ushezi na ukimwi au ndio umetushinda nguvu na kutulazimisha tuukumbatie..

Na serikali iko wapi katika hili,,,ooh mungu wangu unakuta mama anauza mihogo au mahindi ya kuchemsha anapigwa virungu eti anauzia barabani,,lakini machangudoa hawa wanaOdharirisha ubinadamu,wanaosambaza ukimwi kana kwamba ni kitu cha thamani sana katika jamii na wanaoharibu maadili ya watoto ambao ni taifa letu la kesho wanaachwa wajinafasi kwa raha zao...

Aisee huwa napata hasira sana,,mama anajiuzia karanga anavyonyanyaswa,,unataka akale nini??? Unataka awasomeshe vipi watoto??? Unataka afanye kazi gani??? AU UNATAKA AKAJIUZE???Jamani watanzania kama hatutaamua kubadirika,mabadiriko hayawezi kuja....maadili yanapolomoka kwa kasi kupita kiasi,,,jamani viongozi wetu ni vipofu au??? Hawayaoni haya???? Najua penye nia pana njia...LAKINI PASIPO NA NIA PANA GIZA..

Nawasilisha masikitiko yangu,,,naomba mawazo yenu pia wakuu,,,natanguliza shukurani zangu wakubwa..
 
Unakuta katoto kadogo ka miaka 15 kanaenda na jamama la miaka arobaini na kitu ili mradi bwana mdogo awe na 2000/=

Siku hizi na madogo nao wanabanwa na ukakasi! si mchezo
Lakini na midingi nayo inapenda tusichana twa miaka 12,13,14....
 
Wateja wao ni akina nani?

biashara ikikosa wateja matokeo yakle huwa nini
 
Wateja wao ndo haohao walipewa mamlaka ya kuwakamata sasa shida ni kuwa watawakamataje?>??
 
Mi nashangaa hii kampeni ya Fataki na watoto wa chini ya miaka 18, sasa sijui wanalenga watoto wa ainagani maana hii biashara ya ngono inafanywa zaidi na watoto miaka 13 hadi 18 walio wengi.
Achilia mbali hawa wa mitaani hata wanafunzi wa shule za msingi na secondary nao hivyo hivyo wanauza, hizi simu nazo zinachangia sana watoto hawa kutafutwa kwa urahisi - inatia kinyaa unapita na mgeni wa heshima matembezini then vitoto vipo nusu uchi barabarani jamani - ndiyo hali ya uchumi mbaya hiyo?

Arusha, Dar na Mwanza ndiyo waziwazi kabisaa. aibu kubwa kwa nchi yetu.
 
Kutoka kwa Shigongo hii......

Na Waandishi Wetu

Wakati Waislam duniani kote wakiendelea na mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, baadhi ya ‘madada poa' wanaofanya ‘biashara' ya kuuza miili wametoa kali yenye kujaa kufuru ya Mungu wakiweka bayana kuwa, mchana wanafunga, usiku wanajiuza, Ijumaa Wikienda limebeba ushuhuda wa kutosha.



Patroo ya nguvu iliyofanywa na ‘skwadi' ya gazeti hili usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita maeneo mbalimbali ya jiji la Dar ilifanikiwa kuwanasa makahaba hao ambao walionesha ‘kukomaa' katika vilinge vyao wakisubiri wateja ambao kwa dhahiri ni wanaume.

Makahaba hao walinaswa na kamera maeneo ya New Maisha Club (Oysterbay), Jolly Club (Upanga), Leaders Club (Kinondoni) na Kinondoni Makaburini ambako walikuwa ‘wa kumwaga'.



Miongoni mwa makahaba hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao, walipobanwa sawasawa na Mapaparazi Wetu kwamba, hawaoni kuwa wanafanya kufuru kubwa kuuza mwili Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, walijigamba kwamba hata wao wanafunga.

Walisema kuwa, kutokana na kukosa kipato, wameamua kufunga mchana, lakini usiku wanaingia ‘kibaruani' kuuza miili ili wapate pesa ya kujikimu.



"Tunakufuru nini, hata sisi tunafunga. Tunafunga mchana, usiku tunaingia kazini," alisema kahaba mmoja huku akiikimbia kamera ya Ijumaa Wikienda.

Aidha, kahaba mwingine alihoji: "Kama tusipokuja kuuza miili yetu mnadhani pesa ya futari itatoka wapi?"
Baadhi ya makahaba wengine waliwarushia vijembe wenzao hao na kudai kuwa, kama wao wangekuwa kwenye imani ya kufunga wasingekuwa wanaingia ‘kazini, Mwezi Mtukufu huu.



Hata hivyo, kwa mujibu wa maandiko matakatifu ya Quran, swaumu ina baraka na kupokelewa kwa Mungu kwa wale walio katika usafi wa kiroho na kimwili.

Aidha, muislamu ambaye hayupo katika ndoa lakini anajamiiana (anazini kama wafanyavyo makahaba hawa) na kudai anafunga, swaumu yake haiwezi kukubaliwa na Mungu.



Mbali na kufuru ya kuuza miili Mwezi Mtukufu, hata miezi mingine, kitendo cha kufanya ukahaha ni machukizo mbele za Mungu.

Gazeti hili linailaani vikali biashara hiyo haramu na linawataka wanaojihusisha nayo kuiacha mara moja kwani madhara yake ni makubwa tofauti na wanavyofikiria.
 
Kwa kweli hii serikali yetu inaelekea pabaya, tena pa kutisha!!
Utashangaa wamachinga na wauza vitu vingine vidogovidogo wanatiwa virungu na kunyang'anywa mali zao eti wanachafua miji, sasa na hao wanaojiuza hawachafui miji na maadili ya kitanzania piA????? Huku kwe2 uchagani nawashangaa sana migambo wa mji wa Moshi wanakimbizana na wakinamama wauza viatu na nguo mjini na wakiwakamata tu mali zote zinachukuliwa sasa wale wanAojiuza kule mitaa ya Kiusa hamuwaoni mkaenda kuwakamata???
Na kule kwa mjomba Tanga wamejipa mpaka majina ya club za mpira za huko ulaya, utasikia Madrid, Barcelona n.k
ASTAKAFIRULLAH
 
Back
Top Bottom