Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
415
359
Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla payback period haijafika ni vyema unapotwambia imeingiza hasara uwe unatupa na pay back period ilikua ni miaka mingapi. Na je tayari ilishafikiwa. Ila kama hiyo hasara unaikokotoa bila kutwambia payback period ilikua ni miaka mingapi hapo watanzania utawachanganya.

Mimi nadhani tungepewa hesabu nzima, tusiandikiwe tu hasara.

Tupewe pesa iliyotumika kufanya investiment ni kiasi gani kwa ndege zote.

Alafu tuambiwe kila ndege zinaingiza kiasi gani kwa mwaka.

Hiyo ndio hesabu tunayoitaka, Mimi nacho kijua na kukielewa hiyo ni long term business ambayo inatumia higher investiment. Hivyo haiwezi kuleta faida kabla haijafikia payback period.

Twambie kwanza pay back period ilikua ni ya miaka mingapi ndipo uje na hiyo hesabu ya hasara.

Ukitwambia tu hasara hatuwezi kuelewa vizuri.

Maana bado siijui payaback period

Ipo miradi mingi mikubwa ambayo ikiianza usitegemee kupata faida ndani miaka minne, it's impossible. Tuna mradi wa LNG, huo mradi payback period yake ni ndefu sana. Tusitegemee kuja kuanza kupata faida ndani ya muda mfupi. Katika Biashara kubwa lazima uwe mvumilivu.

Mimi kiukweli ningependa kusikia tu return of investiment imefikia kiasi gani basi. Hapo ningechakachua kichwa na kujua wapi tunaelekea.
 
Weanzako wataka kuona faida tangia siku ya kwanza ndege kununuliwa wala hawataki kureason kisa ati hawakumpenda Magufuli.
Hapo ndipo wanapokosea hata biashara za kawaida hazipo hivyo. Sasa yeye hiyo hasara anaipataje ndani ya hii miaka minne. ilitakiwa tupewe hesabu zinazoeleweka. Tueleze return of investiment imefika kiasi gani.
 
Ni ule muda ambao biashara yako inakurudishia fedha na gharama zote ulizowekeza wakati unaanzisha hiyo biashara. Hapo kuna gharama nyingi tu. Gharama za kununua ndege, gharama za kununulia mafuta wakati unakwenda kuzichukua, gharama za kuwalipa wafanyakazi wakati unaanza, n.k
Ni hela uliyoweka kwenye biashara yako inayorudi bila faida?? Au na faida yako humo??, Kama bila faida. Je, faida inayorudi inaitwa kwenye uwekezaji huo?
 
Biashara ya ndege haiwezi kuleta faida kabla pay back period haijafika...

Ni kweli uwekezaji kwenye ATCL ni wa muda mrefu hivyo faida inaweza kuchukua muda mrefu. Shirika la ndege la Tanzania uwekezaji wake hasa wa ununuzi wa ndege kidogo haukufanyika kwa ufanisi. Hakukuwa na sababu kwanza kununua ndege cash na pia hakukuwa na sababu ya kununua ndege kubwa ya DREAMLINER kabla ya shirika kumudu soko la ndani [ DOMESTIC ROUTES} na soko la majirani zetu[ REGIONALROUTES].

Shirika lingefanya vizuri kama kungekuwa na strategic plan ambayo ingesisitiza kuwa na mpango wa jinsi ya kukidhi soko la ndani kwa muda mfupi na muda mrefu pia kuangalia jinsi ya kumudu ushindani ulionza kwa majirani zetu nao kuanzisha mashirika yao ya ndege!

Tuna wataalam wa mambo ya usafirishaji ambao wanatumiwa na hata taasisi kubwa Duniani lakini la kushangaza Serikali ya Magufuli ilikuwa haioni umuhimu wa kuwatumia; ikaona afadhali watu wa TANROADS KUWA WAKURUGENZI WA ATCL kwani inaelekea aliamini ndege biashara yake ni kama ya daladala!

Kuna mwalimu wa Transport Economics UDSM enzi hizo siku hizi mara nyingi ni consultant nje ya nchi lakini huwa namuona ona, Jina lake limenitoka lakini nakumbuka aliwafundisha wakina Haule wa TANROADS na marehemu Dr.Likwelile miaka hiyo!! Huyu angeweza kuwa na msaada mkubwa kwenye board ya ATCL.
 
Payback period refers to the time required to recoup the funds expended in an investment, or to reach the break-even point. For example, a $1000 investment made at the start of year 1 which returned $500 at the end of year 1 and year 2 respectively would have a two-year payback period
Elezea kwa kiswahili mkuu.
 
Mkuu mpaka CAG kafikia kusema limeendeshwa kwa hasara hayo yote ameyapigia hesabu
Ni kweli mkuu, sasa hapo anawaogopesha watanzania ni vyema angetuorozoshea kwanza zile fedha zilizowekezwa kama tayari zimesharudi then atupatie na kipindi cha Kurudisha kilikua ni miaka mingapi alafu atwambie sasa hizo ndege zinaingiza fedha kiasi gani kwa kila mwaka kabla ya kukokotoa hasara au faida.

Kwasababu kwa mtaji ulizowekezwa kwa kila ndege sitegemei shirika kuanza kupata faida haraka kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom