Biashara ya nafaka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya nafaka.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bhbm, Nov 12, 2011.

 1. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 717
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ninaomba kujuzwa wanajf wenzangu, je ni nafaka aina gani zinaweza kuwa na soko zuri hapa mjini Dar? Na je ni mtaji kiasi gani naweza kuanzia nao? Natanguliza thanks.
   
 2. E

  Enny JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 948
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Maharage
   
 3. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 717
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu kwa mchango wako wa maana.
   
 4. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mkuu biashara ya nafaka inalipa. unaweza jikita na mazao kama maharagwe, kunde, njegere, mbaazi nk. mtaji unategemea na uhitaji, anza hata kidogo kwa gunia kama 3 kwa kila zao ila fanya utafiti wa soko ili utakapotaka kujitanua isikupe tabu.
  goodluck
   
 5. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 717
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Asante sana mkuu kwa ushauri wako mzuri, God bless you.
   
 6. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,277
  Likes Received: 550
  Trophy Points: 280
  mkuu mimi c pingani na wewe but nataka kukushauri jambo moja,

  - katika swala zima la biashara ya nafaka ni bora ukajikita katika ku ad value au kuongeza thamani ya hizo nafaka.

  1. Ni bora ukawa na ofisi yako mjini na jaribu kuyaongezea thamani hayo mazo kama vile kugred na kupark kabisa. Hapo utakuwa umeongeza thamani na utauza kwa bei ya juu, na unaweza tafuta hata supermaket tano tu za kuwa sambazia.

  2. Hili la kununua mchele kutoka mbeya na kuja kuuza dar kama ulivyo hakuna cha maana sana mtu nacho pata zaidi ya ujanja ujanja wa kuchanganya. Mtu anachukua mchele wa mbeya na kuchanganya na mchele wa morogoro
  - hii biashara ya nafaka c kwa mba inalipa sana ila ni ujanja ujanja unao fanywa na wauzaji kwa kuchanganya changanya. Anaweza chukua gunia la maharage safi akachanganya na nusu gunia la maharage mabovu ndo business inaenda.

  - ila hili la ujanja ujanja ni la muda sana na si endelevu.


  So jitajidi upate hata mashine ya kupaki kwenye mifuko, mfano ukipata mashine moja inayo itwa heavy duty sealing machine ni nzuri sana unaweza ukawa na vibarua wako wa kugred na wewe ukawa unapaki na kuuzia watu wa supermarket.
  Hiyo mashine niliyo kuambia ni ambayo ina silidi kama vile totopark zinavyo kuwa zimefungwa kwenye vile viloba.

  Kuna kampuni moja ya kenya ina tengeneza vifungashio vizuri sana unweza cheki huko
   
 7. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 717
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu Komandoo nakushukuru sana kwa ushauri wako wa maana, tajitahidi kuufanyia kazi. Ila naomba tu unifahamishe hiyo mashine naweza kupata wapi? Hapa Dar ama Nairobi? Na bei zake zikoje?
  Natanguliza shukurani.
   
Loading...