Biashara ya Mtandao inavyoathiriwa Na Umeme

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Kwa sasa kampuni nyingi zinazotangaza bidhaa zao kwa njia ya mtandao zinaangalia zaidi uwingi wa watu wanaotembelea tovuti au blogu husika toka maeneo Fulani , wanaangalia tabia za watu hao wanapenda kutazama nini kwenye mtandao na kabla ya kwenda tovuti au blogu Fulani huwa wanatoka blogu gani na pia jinsi wanavyotafuta vitu kwenye mtandao ili waweze kuweka matangazo yao vizuri kwenye majibu ya kile kinachotafutwa .


Ninaposema wingi wa watu wanaotembelea tovuti Fulani au blogu Fulani toka eneo Fulani namaanisha watu hao wawe kwenye mtandao kwenye tovuti Fulani kwa ajili ya kutafuta kitu Fulani idadi iongezeke au kuwa na watembeleaji wapya angalau 300 kila siku ya mungu toka maeneo yanayofafana na hayo .


Kwa wale wanaomiliki blogu au tovuti zenye matangazo Fulani ambayo malipo yake inategemea watu wa eneo Fulani mfano Tanzania kwa kipindi cha siku 7 sasa wamekuwa wahanga wa biashara zao za mitandao kushuka kwa kiasi kikubwa kutokana na tatizo la umeme kwamba watu wengi sasa hawatumii komputa zao zilizounganishwa kwenye mtandao kama wanatumia wengine hawana huduma ya mtandao kwa sababu hizo hizo za umeme .
Kwa wengine kama sisi tulishaona hili kwa kipindi kirefu kwahiyo target yetu ya matangazo kwa kiasi kikubwa kimekuwa kwa watu wa mataifa mengine ambao wana uhakika na vitu hivi kama umeme na komputa zilizounganishwa kwenye mtandaoa au wanatumia simu za mikononi na wana uhakika wa kutembelea tovuti na blogu hizi .


Kwa wale wenzangu wenye blogu walioweka matangazo ya kugonga ( click) kama adsense , infolinks , blackads na nyingine nyingi huu ni wakati wenu wa kuangalia masoko ya nje ya blogu zenu na tovuti zenu kwa ajili ya kukuza vipato vyetu na biashara zenu mitandaoni sio siri kukatika kwa umeme vijana wengi wanaotegemea blogu zao kwa ajili ya maisha yao ya kila siku wameathirika serikali imekosa mapato kutokana na cheki ambazo zingeingizwa kwenye mabenki ya kitanzania mwisho wa mwezi huu .


Huu sio utani kuna blogu zilizokuwa zinazalisha kiwango cha euro 15 kwa siku moja leo hii inakuwa na chini ya euro 5 kwa siku moja na kiwango kinaendelea kushuka kwa sababu watu hawatembelei blogu hizo kwa sababu haziwi updated kwa taarifa pia watangazaji hawatangazi bidhaa zao huko .
Kwa wale wengine wenye uwezo wa kujenga ushawishi kwa kampuni zingine kutangaza kwa njia za kawaida wanaweza kufanya hivyo hata hivyo wengi haswa hapa nyumbani hawaangalii idadi ya wanaotembelea blogu au tovuti na kutafuta taarifa zingine zingine kuhusu blogu au tovuti .
Kama kampuni zetu zingekuwa zinalipa gharama za matangazo kwenye tovuti kutokana na idadi ya watu waliogusa matangazo hayo naamini faida ingekuwa kwa watu wengi na ingeonyesha takwimu sahihi za biashara hizi za mitandao .
Kama unaswali , mapendekezo na maoni tunaweza kuwasiliana
Weekend Njema
YONA F MARO
WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
 
Back
Top Bottom