Biashara ya mifugo ng'ombe, toka mikoani kuja Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya mifugo ng'ombe, toka mikoani kuja Dar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by DATOGA, Jan 20, 2012.

 1. D

  DATOGA Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ndg wana jf hope sote tu wa afya njema baada ya hekaheka za wiki nzima.

  Naomba mwenye EXPERIENCE ya kutosha na hii biashara ya Mifugo hasahasa Ng'ombe kuwaleta Dar kutoka Mikoani kama inalipa
  coz nimewahi enda pale PUGU Mnadani wakati wa Christmas angalau nijitafutie Mbuzi wa kumtafuna na nikafurahishwa sana na ile
  biashara, ati muuzaji anakwambia BEI ya mnyama kwa kukadiria bila kupima ktk kilo.

  Kilicho nihamasisha zaidi ni ndg yangu nilie kuwa nae pembeni aliniambia unaweza kuta huyo mbuzi anaemuuza Tsh 50,000/-
  amemnunua Tsh 25,000/- huko mikoani!!! Au ng'ombe wa 600,000/- unaweza kuta kanunua 300,000/-

  Please NAOMBA mwenye maujanja na hiyo business anipashe hapa, aniambie ma-requirements na mikoa gani nitapata
  hawa mifugo esp ng'ombe kwa wingi?


  With Thanx
   
 2. DullyM

  DullyM Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mkuu, mara nyingi, mtu anafanya biashara ili kupata faida, na hizo bei wanazouza ni kutokana na gharama walizonazo pamoja na maslahi flani. kwa hiyo sidhani kama kuna mtu atanunua mbuzi 25,000 kisha auze kwa 10,000[​IMG]
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu mimi ningekushauri ufanye jambomoja.

  - Umefika wakati tuwe tunafanyabiashara zenye tija, biashara zenye faida na biashara ambzao hazina usanii.

  - Biashara kama hizi zina usaniimwingi sana
  1. Kununua mazao na kwenda kuyauzasehemu nyingine

  2. Kununa kuku na kwenda kuziuzasehemu nyingine

  3. Kununua ng'ombe na kwenda kuziuzasehemu nyingine

  HIZI BIASHARA LAZIMA UWE MSANII WAHALI YA JUU KUWEZA KUZIFANYA NA SI KWAMBA ZINAHITAJI AKILI BALI ZINAHITAJIUSANII.


  MFANO:


  1. KUNUNUA KUKU NA KUJA KUZIUZA SEHEMUNYINGINE- HAPA HAKUNA ULICHO ONGEZA ZAIDI YA KUWALILIA WANAO KUZIA WAKUZIE BEIYA CHINI NA WEWE UKAUZE BEI YA JUU. HAUJAONGEZA THAMANI YOYOTE ILE KWENYE HAWAKUKU

  2. UNANUNUA MAGUNIA YA MAHINDI KUTOKADODOMA NA KUPELEKA DAR- HAPA HAKUNA CHA MAANA ULICHO FANYA ILA USANIIUTAFANYIKA WAKATI WA KUNUNUA UTUMIE NDOO KUBWA ILIYO FANYIWA MODFICATION, NAWEWE WAKATI WA KUUZA LAZIMA UCHANGANYE MAHINDI MAZURI NA MABAYA ULIO NUNUA KWABEI YA CHINI. BILA KUCHANGANYA HAYA MAHINDI HUWEZI PATA FAIDA
  - Hapa unakuwa hujaongezea hayamahindi thamani yoyute ile

  3. Kwenye swala la ng'ombe nalolinahitaji usanii tu, ukawalilie wanao kuzia il wakupunguzie na wewe upatekafaida.

  UMEFIKA WAKATI WA KUFANYA BIASHARA ZAKUONGEZA THANANI

  1. Nunua ng'ombe chinja na supplynyama hapa unakuwa umeongeza thamani
  -Au fungua kiwanda cha kupaki kabisana kuuzia watu wa supermarket, hapa unakuwa umefanya biashara ya maana sana

  2. Nunua mahindi saga na paki unga,hapa unakuwa umeyaongezea hayo mahindi thamani kubwa mno na utapata faida

  3. Nunua kuku chinja, pack na uza-
  Hii ndo biashara ya kuad value, lakinihii ya kununua mchele kutoka morogoro na kuja kuuza dar inahitaji usanii wakuchanganya mchele wa morogoro na ule wa thailandla sivyo hakuna chachote kile utakacho faidi

  NDO MAANA HII BIASHARA HAIHITAJI AKILIBALI USANII WA KUIBIA WATEJA, NA SI ENDELEVU

   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Muhunze wilayani Kishapu kuna mnada wa ng'ombe pale very easy we kama unalo soko la kuuza hao ng'ombe zako, nenda zako pale kanunue kama bado hazijafikia idadi utakayo. kuna minada kibao ya ng.ombe mfano Sanga, Maswa n.k isipokuwa kipindi malisho mengi na bei iko juu, lakini kipindi cha ukame bei ubwete.

  Maelezo mengine kama wanafanyaje nini na nini niPM, hakuna mbinu chafu, hamna wa kukusumbua, hamna kibali wala nini.
   
 5. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa biashara ya usanii ni ipi?
  Hizi ulizozitzja wewe au?
  Mwenzio kaomba ushauri usimtishe mtie moyo,
  Hii biashara ya ng'ombe haina usanii wala nini ng'ombe unamuona kwa macho hakuna ng'ombe wa kichina, unanunua kitu roho inapenda.
   
 6. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280

  HUJANIELEWA, MIMI SIJASEMA HII BIASHARA NI YA KISANII, NIMESEMA LAZIMA UWE MSANII KUFANYA BIASHARA AMBAZO UNANUNUA KITU NA KUJA KUKIUZA KAMA KILIVYO.

  - MFANO:

  Biashara ya mchele mara nyingi ni usanii mtupu, mtu anachukua mchele wa mbeya anachanganya na wa morogoro ndo anaingiza sokoni, na anafanya hivyo kwa sababu akiuza kama ulivyo itakuwa ni hasara kwake hatapata faida.

  - Ndo maana nikasema ni bora tukaja na biashara za kuongeza thamani ambazo zinalipa sana, Ng'ombe unavyo mnunua na kuja kumuuza kama alivyo unakuwa hujamuongezea kitu na mara nyingi lazima huko unako nunua ulie sana ili wakupunguzie kwa sababu na wewe unakuja kumuuza kama alivyo.

  - NDO MAANA NIKASEMA BIASHARA NYINGI SANA HATA ZA KUKU WA KIENYEJI MARA NYINGINE HUWA WANA MIX NA ZA KISASA HUMOHUMO, NA HII NI KWA SABABU HAKUNA UTARATIBU WA KUZIONGEZEA THAMANI NDO AZIUZE,

  - BIASHARA YA NGOME

  1. Yule mchinjaji wa mwisho ndo anae faidi na wala si wewe unae uza ngo'ombe kama ng'ome.
  KAMA UNGEKUWA UNANUNUA NA KUZICHINJA NA KUPAKI AU KUUZA NYAMA UNGEPATA
  1. NGOZI- HII NI PESA
  2. KWATO HIZI NAZO NI DILI SANA
  3. PEMBE ZINASOKO LAKE
  4. MIFUPA, HII INASOKO LAKE PIA
  5. NYAMA NI PESA
  6. MENO YA NG'OMBE NI PESA
  7. MKIA WAKE, ZILE NYWELE ZA MKIA WAKE NAZO NI PESA
  HAPA UNGEWEZA PATA VITU ZAIDI YA 7

  SIJAJUA WAUZAJI WA PUGU KAMA WA CHUKULIA MAANANI NA HIZI PRODUCT ZINGINE
   
 7. D

  DATOGA Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Thanx guyz hasahasa Mr. Abdallah Hassan, i will pm u ma friend
   
 8. D

  DATOGA Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Thanx guyz hasahasa Mr. Abdallah Hassan, i will pm u ma friend
   
 9. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nyie mnataka kuingilia mabizines ya wakubwa. Tip; KUNA SOKO ZURI DUBAI, QATAR NA HATA SAUDIA. Lkini kumbuka kuna wakubwa ambao ndiyo wameshilia mabiz hayo.
   
 10. D

  DATOGA Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
   
 11. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani sisi hatuwezi kuwauzia Nyama? ni mpaka tuwauzi ng'ombe mzima? au tunawauzia ng'ombe wachinje wachukue ngozi theni watengeneze viatu waje kutuuzi kwa bei ya ng'ombe?

  Masoko ya ng'ombe yako mengi sana hapo kenya tu kuna soko la kufa mtu,

  Ila kule kenya wao wanafaidi zaidi kwenye ngozo na product zingine.


  HILI LA DUBAI NA QATAR SI LA MCHEZO WAKUU SI RAHISI KAMA MNAVYO FIKILIA, SI SWALA LA KUPAKIA NG'OMBE KWENYE MELI NA KUPELEKA KULE.

  HAWA MPAKA WAKUPE KIBALI CHA KUINGIZA NG'OMBE KWAO SI SWALA LA KITOTO NA SI SWALA LA MWAKA MMOJA
  WANAANGALIA VITU VINGI SANA, WANAJARI AFYA ZA WATU WAO SI HUKU BONGO TUNALETEWA SAMAKI WA NYUKILIA THEN TUNAAMBIWA NI SALAMA

  BAADHI YA VITU WANAVYO CHEKI

  1. MAHALI NG'OMBE WANAKO TOKA/SHAMBA/RUNCH
  2. UTUNZWAJI WAO
  3. MADAWA WANAYO PEWA/ AINA YA MADAWA WANAO TIBIWA NAYO KAMA HAYANA MADHARA
  4. CHAKULA WANACHO PEWA

  HUWEZI OKOTELEZA NG'OMBE KWENYE MINADA YA SHINYANGA HALAFU UTARAJIE KUWAPELEKA DUBAI, NI NDOTO MKUU, HAPA LAZIMA UWE NA SHAMBA LAKO NA UNAKUWA UNAWATUNZA MWENYEWE NA HAPO NDO UNAWEZA KU EXPORT
  NA KIBALI WANATOA WAO SI KWAMBA UNACHUKULIA HAPA DAR KIBALI

  WALE WANAANGALIA SANA QUALITY YA NG'OMBE, NA SANA SANA WENYE RUNCH NDO WANAO WEZA KU EPORT HUKO NA SI HAWA NG'OMBE WA KUSWAGA NA KUPIGWA NA FIMBO

  - HUWEZI BEBA NG'OMBE KUTOKA SHINYANGA NA TREN AU MALORI AU KWA KUWASWAGA UFIKISHE DAR UTARAJIE KUWAPAAKIA MELI UWAPELEKE DUBAI, UTARUDI NAO
   
 12. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,850
  Likes Received: 2,778
  Trophy Points: 280
  Komandoo acha kutisha watu. Soko la Waarabu siyo gumu kiasi hicho. Mara ngapi wameuziwa kondoo na mbuzi wa kutoka Shy na Ddm? Soko lenye masharti magumu ni la EU countries, huko asikwambie mtu. Hawa wana standards za kwao.
   
 13. b

  bagamoyo1 Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  samahani kama ni tawakwaza ndugu zangu , chonde chonde .> BIASHARA MSILIHARIBU bongo kila mtu ni mfanyabiashara hata muuza mchicha ukimuuliza anakuambia ni mfanya biashara , mchuuzi ni nani ?? ninachotaka kufahamisha biashara ni malezi huwezi kukurupuka na ukaaza biashara , na Tanzania tuna makabila 2 makubwa ya biashara wachaga na wapemba , na uchumi mzima wa tanzania unaendeshwa na makabila mawili pia waarabu na wahindi kwanini ?? hivi vizazi kila vikikuwa havijuwi shughuli yoyote zaidi ya bisashara tangu mtoto anazaliwa anafundishwa kujuwa thamani ya sh moja na ndiyo maana wakiachiwa urithi biashara zinakuwa , simemi kwamba hakuna kabila nyingine zisizo fanya biashara ikitokea kuwepo basi huyo mzee akifariki biashara inafilisika hii ni kutokana watoto hawapewi malezi ya kibiashara ,

  MADA HALISI > ILI KUFANIKIWA KIBIASHARA UNATAKIWA KUWA MCHESI , MTU WA WATU , UWEZE KUNUNUA KILICHO BORA KWA BEI YA CHINI , KUEPUKA WATU WOTE WAKATI , NA KUKIUZA KILICHOBORA KWA BEI YA USHINDANI NNDANI YA SOKO
   
 14. K

  KEEM New Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka lakini unasahau kua kuadd value kunahitaji mtaji mkubwa ... ukizingatia kwa sie ambao tunaanza biashara tukiwa na mtaji mdogo.. unatushauri vipi.. tuache tusubiri tukiwa na mtaji wa kutosha kuadd value kwnye hzo biashara zetu..? mimi pia ni mmoja wa wanaofikiria kuanzisha biashra ya kuuza nafaka (mchele sana sana)... na nimefurahi kuona wenzangu mkijadili habari hizi.. naombeni mawazo zaidi ya kibiashara.. asanteni sana..
   
 15. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mkuu Biashara zote ni ghalama, na kuongeza thamani ndo mpango mzima, Ukinunua MCHELE KUTOKA MBEYA UKALETA DAR, ili upate faida ni lazima ufanye usanii wa kuchakachua MCHELE wa mbeya unachanganywa na wa Morogoro na hata saa zingine unachanganywa na MCHELE WA NJE YA NCHI KUTOKA PAKSATAN NA THAILAND,

  Bila kuongeza thamani huwezi fanya Biashara yenye Tija hata siku moja, na si lazima uanze na mitaji mikubwa mkuu, hii ya kuuza mchele au mahindi kama yalivyo ni unyonyaji na hakuna faida inayo patikana,

  Chukulia mfano Kahawa Ya Tanzania au Pamba, PAMBA INAPELEKWA NJE INATENGENEZA NGUO THEN TUNARUDISHIWA KUUZIWA KWA BEI GHALI,

  Ni uvivu wetu tu lakini hakuna kisicho wezekana ni kuweka mikakati
   
 16. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu KOMANDOO ushauri wako ni mzuri na unaweza kuwa mgumu kwa wengine kueleweka kwani wa TZ wengi tunapenda deal zitakazotuingizia pesa za haraka; kweli biashara nyingi za uchuuzi zimetawaliwa na usanii, kama mtu anafikiria kufanya biashara ya mifugo au mazao na unaona huna mtaji wa kutosha katika kuongeza thamani ni bora kufikiria kuanza kulima hiyo bidhaa au kama ni mifugo basi kufikiria kuanza kufuga na baadae hatua kwa hatua unakuza uzalishaji wako mpaka unaweza kuongeza thamani, Vinginevyo kama unakwenda kununua mazao kwa wakulima ujiandae kwenda kuwanyonya (kuwazulumu) wakulima kutokana na uelewa wao mdogo au shida wanazokabiliana nazo. Nimeshawahi kwenda kijiji fulani kuna wafanyabiashara hupita wakati ambapo wanakijiji wana njaa (wameishiwa mazao), huwakopesha fedha kwa ahadi ya kuja kulipa mazao, hutoa dhamani ya fedha kwa mazao kwa kiwango kidogo sana, mfano gunia la mahindi kwa Ts. 10000, wakati msimu ukifika gunia la mahindi ni Tsh 30000. Nilishuhudia baadhi ya wakulima wakivuna mahindi yao yote na kuwapelekea wafanyabiashara kama malipo ya mkopo waliopata, kwa kweli ni unyonyaji wa hali ya juu.
   
 17. M

  Malila JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Naomba nikushauri kijasiriamali ndugu yangu,

  Kama unataka kufanya biashara hiyo kwa kumaanisha, basi nunua eneo kubwa nje ya mji wo wote uliko,kisha jenga terminal ya mifugo hiyo unayotaka. Baada ya kujenga terminal yako anza kununua mifugo sawa na soko la msimu huo,kisha unawaboresha/nenepesha tayari kwa kuuza moja kwa moja au indirect, yaani watu wakijua kuwa kuna terminal ya mifugo iliyoboreshwa watakufuata wenyewe. Ni kama shamba/ranch, lakini lenyewe wanyama wanakaa muda mfupi na kuuzwa.
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Chasha aka KOMANDOO na Mgombezi ni kweli kabisa hii biashara ya mifugo si rahisi kama watu wanavyofikiria ni usanii kwa kwenda mbele na kuwakandamiza wafugaji na wakulima, kinachofanywa ni kuzitumia shida zao kujinufaisha wewe mwenyewe. Kiukweli unaponunua ng'ombe mikoani mpaka kuja kumuuza dar faida yake ni ndogo sana.. utakapotoa gharama za kumtunza kabla ya kumsafirisha, usafirishaji, mahali pa kumfikisha, udalali, urasimu,...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mkuu salama, za siku.

  Siku moja nilikuwa Kibakwe Ddm, debe la mahindi linabadirishwa na ndama wa ng`ombe, na jamaa yuko na gunia mia moja alizonunua wakati wa mavuno pale pale kibakwe, kila gunia wakati huo alinunua kwa Tsh 15,000/. kwa hiyo utaona kwamba gunia moja lilimpa ndama sita au saba hivi ( debe analopimia yy ni lile modified sio alilonunulia mahindi). Kibaya zaidi, anawaacha wale ndama pale pale kwa makubaliano na mkulima mmoja kuwatunza kwa kumpa gunia moja la mahindi kwa miezi sita ndio aje kuwachukua.
   
 20. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mkuu salama kabisa mambo yamebana sana kwa sasa,
  hela za laana mimi huwa sizitaki kabisa ndio maana tunajaribu kumuelewesha ndugu yetu hapa kuhusu hizi biashara za kitapeli, huko kongwa, mpwapwa vijijini kuna wahuni huwa wanapeleka mafuta ya taa kubadili na mahindi daaa yani lita moja inabadilishwa kwa debe la mahindi. Wenye matractor nao huwa wanayapeleka huko kipindi cha kilimo then hekari moja inalimwa kwa gunia kadhaa za mahindi au maharage na wanakijiji hawana 30,000 ya kulimia hk 1 so inawabidi tu wakubali... itatuchukua muda sana kuja kuibadili tz yetu kwa mitindo ya namna hii
   
Loading...