Biashara ya maziwa mtindi na fresh

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Kuna wimbi kubwa sana la wauza maziwa mtindi na fresh limezukia maeneo ya ubungo river side (mandela road) wale wafanya biashara yale maziwa ni mengi sana na kila siku yapo sijui yanatolewa wapi.

Kinachoniumiza ninefanya resech hao jamaa yale maziwa wanaletewa kutoka vijijini na hawa wanaoleta hayo maziwa hawataki hao wanunuzi wajue soko (huko yanakotolewa) wao wanaleta maziwa na ndoo na ( hapa inategemea wewe mteja unataka ndoo ngapi)wanakuachia ndoo au wanakumiminia wanadudi na ndoo zao wee unatoa hela.

Ndoo kubwa mtindi ni 38 hadi 40 elfu ndoo ndogo ni 18 hadi 22 elfu.hao wauzaji hawana cha kibali cha afya wala leseni mamlaka ya dawa na chakula (TFDA) wa leseni ya serikali ya kulioa kodi TRA hapa sijui siku itatokea maafa au watu kuumwa matumbo serikali sijui itaanzia wapi na serikali yenyewe inakosa maoato maana hii biashara mzigo unaoshushwa pale ni zaidi ya ndoo 2000 kwa siku na ndani ya masaa 4 mzigo umeisha maana hawa wanunuzi wadogo wadogo wanatoka sehemu mbali mbali.

Maziwa yanaletwa alfajiri saa tisa mpaka saa moja kasoro maziwa yameisha.
Mamlaka husika fuatilieni hili hiki ni chanzo kingine cha mapato mnakipoteza.
 
Hapo ulipomalizia hadi asubuhi yameisha umeonyesha wivu wakizamani sana .Unataka maziwa yalipiwe kodi ??? Acha
Kujifanya una hasira na hii nchi .
 
Mtoa mada,
Achana na kodi au TRA una point kubwa sana kwenye afya ya mlaji maziwa ni kitu sensitive sana hasa maziwa ya mgando uandaaji ukiwa mbovu unaweza kuzua janga hadi mkashangaaa......

Kwa wingi wa ndoo hizo na muda wa kuisha (kama ni kweli) ni bora udhibiti ukafanyika au mamlaka zikaangalia namna ili kuilinda afya ya mlaji....

Mwisho wa siku tutafute Hela na hiyo ni njia moja wapo.
 
Back
Top Bottom