Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

1. Mashine ya kusaga unga wako wewe ili uweke kwenye mifuko uuze au unasagia watu wanalipia huduma hiyo?!!

2. Angalia soko na wanunuzi endelevu au hapo unapoiweka tabia ya watu unaoishi nao je ni wa kipato cha kati au vipi, watu wengi kwa sasa wananunua unga dukani kuliko kubeba mahindi kwenda kusaga,angalia sehemu unayokaa na wateja unaowalenga.

3. Kukutoa au kutokukutoa inategemea na malengo yako, mtaji, mipango kazi, uelewa wako wa soko, timu yako utayofanya nayo kazi, aina za mashine utazotumia, usimamizi wako n.k. . . .Biashara inataka nidhamu ya hali ya juu sana nabkubadilika kutokana na soko na washindani wako.

4. Umeamua kuweka chumba katika nyumba hiyo hiyo au unapoishi umejenga vhumba pembeni maalum kwa kazi hiyo??!!. Kusaga ni kazi ya vumbi na ina kelele, sio salama sana kuweka katika nyumba hiyohiyo nadhani hata maandalizi ya msingi wa mashine ni tofauti na nyumba ya kuishi

Kila la kheri. . .
 
Habari za jioni wakuu

Ninaombeni mawazo yenu. Niko kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda rasmi cha kusaga na kufungangasha unga wa nafaka mbalimbali. Nina mashine ya kusaga mahindi mkoani Dodoma na nilikua nafunga na kuuza unga kienyeji vijijini. Sasa nimeamua kuifanya iwe rasmi kabisa na Mungu akisaidia January 2016 bidhaa zangu zitakua sokoni. Niliyofanya mpaka sasa?
1. Mashine ya kukoboa na kusaga
Tayari ninayo na inatoa huduma

2. Mashine ya kupima, kufungasha na kufunga niliagiza kutoka China na iko kwenye hatua za mwisho za kuwa installed

3.Nimeshaanza mchakato wa kupata vifungashio kwenye kiwanda kimoja Bagamoyo. Mifuko ya kilo 5, 10 na 25 yenye nembo.

4.Stock ya mahindi ninayo karibia tani 10

5.Niko kwenye hatua za mwisho za kupata kibali cha tbs.

Kwa wazoefu wa biashara hii naomba kama kuna mwenye mchango wa ziada tushauriane mpaka hapo nilipofikia. Na kama kuna kitu kingine chochote kinahitajika.Tunaweza wasiliana hapa kwa michango au anymore business ideas/patnership na masoko zaidi.Au hata kwa PM

Shukran.
Mjasiriamali
 
hongera mpaka hapo ulipofika umeshinda NAIPENDA HIYO BIASHARA naomba nijuze hizo mashine umezinunua bei gani hasa hiyo ya kukoboa na mpaka kuifikisha TZ IMEKUGHARIMU SHILINGI NGAPI
 
hongera mpaka hapo ulipofika umeshinda NAIPENDA HIYO BIASHARA naomba nijuze hizo mashine umezinunua bei gani hasa hiyo ya kukoboa na mpaka kuifikisha TZ IMEKUGHARIMU SHILINGI NGAPI

Mkuu mashine ya kusaga na kukoboa sijaagiza kutoka nje. Hii niliinunua kutoka kwa mstaafu mmoja wa Relwe(TRC) mwaka 2010 nikiwa chuo. Nilinunua kinu cha kukoboa na kinu cha kusaga na mota moja niliyoifunga katikati kwa vinu vyote. Mota yangu ni ya 20hp nilinunua kwa sh.700,000.Hivyo vitu vingine nilinunua kwa milion 2 wakat huo.

Kwa sasa niliagiza mashine ya kupima uzito,kujaza na kufunga mifuko(VFFS) kutoka China. Hii ilinicost mil 4.5 mpk kufika Bongo.Hapo ondoa gharama za shipping kwakua nilipakia katika kontena la mtu.

Natumai nimekujibu.
 
Mi nakuona we ndo mzoefu na ungetoa ushauri ili na wengine tukiweza tufanye hiyo biashara

Hamna uzoefu katika maisha. Na hamna uzoefu kwenye biashara pia na siku utakayojiona we ndio mzoefu ujue ndio siku utakayoanguka. Nimeiweka hapa hii ili niendelee kujifunza zaidi haswa katika masoko na pia mbinu mpya.

Hapa wanapita watu mbalimbali mkuu.

Natumai umenielewa. Mwenye kutaka ushauri ntamjibu pia katika yale ambayo nayafahamu
 
Big up sana... I am inspired..

Get angry get insipired. Kuwa mvumilivu,na cha muhimu kuliko vyote penda unachofanya. Mimi nimeipenda hii kazi tayari na hata ukiniambia nikaajiriwe BOT ntatosa. Sema kuna changamoto nyingi na ndio nataka tuelezane changamoto kwa wazoefu. Sema hawaji na mimi sijioni km mzoefu bado. Nataka kujifunza zaidi
 
aisee kaka, nimekua nikiwazia sana biashara kama yako, sema ndo kupata taarifa ni ngumu, thanks nimepata insights kidogo kupitia post yako.
 
Mkuu mashine ya kusaga na kukoboa sijaagiza kutoka nje. Hii niliinunua kutoka kwa mstaafu mmoja wa Relwe(TRC) mwaka 2010 nikiwa chuo. Nilinunua kinu cha kukoboa na kinu cha kusaga na mota moja niliyoifunga katikati kwa vinu vyote. Mota yangu ni ya 20hp nilinunua kwa sh.700,000.Hivyo vitu vingine nilinunua kwa milion 2 wakat huo.

Kwa sasa niliagiza mashine ya kupima uzito,kujaza na kufunga mifuko(VFFS) kutoka China. Hii ilinicost mil 4.5 mpk kufika Bongo.Hapo ondoa gharama za shipping kwakua nilipakia katika kontena la mtu.

Natumai nimekujibu.

Asante nashukuru sana ninaomba unisaidie kwenye mahitaji ya vibali je nako ni leseni ya biashara na tin number au mpaka uwe umefungua kampuni? na je hiyo mota ina maana kama unasaga huwezi kukoboa? NILIWAHI ULIZIA SABA SABA niliambiwa kinu cha kusaga milion mbili na cha kukoboa ilikuwa tatu HAPO SIJAJUA MOTA IPO NJE AU naomba msaada wako mkuu au hata ushauri cost za kuiset mpaka mashine ianze kufanya kazi
 
Asante sana mkuu. Ndo hivo matatizo yanakukomaza sio kukaa kulia lia. Unapambana. Asante sana

Ila nashangaa thread za huku hamna wachangiaji

watu wengi wabinafsi KUNA JAMAA YUPO HAPA MBEZI BEACH ANAPIGA HELA KWELI KWELI HII BUSSINESS INA FAIDA ENDAPO UNAZALISHA UNGA WAKO MWENYEWE kama mkuu anavotaka demand ni kubwa sana
 
watu wengi wabinafsi KUNA JAMAA YUPO HAPA MBEZI BEACH ANAPIGA HELA KWELI KWELI HII BUSSINESS INA FAIDA ENDAPO UNAZALISHA UNGA WAKO MWENYEWE kama mkuu anavotaka demand ni kubwa sana

Hivi Kwa Sasa mashine ya kusaga na kukoboa original nzuri na vifaa vyake kama kinu motor n.k itakua kama sh ngapi??? Na je zinaweza kupatikana moter Za kutumia fuel energy kama diesel n.k au zote n Za umeme
 
Habari za jioni wakuu

Ninaombeni mawazo yenu. Niko kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda rasmi cha kusaga na kufungangasha unga wa nafaka mbalimbali. Nina mashine ya kusaga mahindi mkoani Dodoma na nilikua nafunga na kuuza unga kienyeji vijijini. Sasa nimeamua kuifanya iwe rasmi kabisa na Mungu akisaidia January 2016 bidhaa zangu zitakua sokoni. Niliyofanya mpaka sasa?
1. Mashine ya kukoboa na kusaga
Tayari ninayo na inatoa huduma

2. Mashine ya kupima,kufungasha na kufunga niliagiza kutoka China na iko kwenye hatua za mwisho za kuwa installed

3.Nimeshaanza mchakato wa kupata vifungashio kwenye kiwanda kimoja bagamoyo. Mifuko ya kilo5,10 na 25 yenye nembo.

4.Stock ya mahindi ninayo karibia tani 10

5.Niko kwenye hatua za mwisho za kupata kibali cha tbs.

Kwa wazoefu wa biashara hii naomba kama kuna mwenye mchango wa ziada tushauriane mpaka hapo nilipofikia. Na kama kuna kitu kingine chochote kinahitajika.Tunaweza wasiliana hapa kwa michango au anymore business ideas/patnership na masoko zaidi.Au hata kwa PM

Shukran.
Mjasiriamali

Hakikisha unakuwa na soko la uhakika. Na ikiwezekana muajiri mtu wa 'marketing' kazi yake ni kila siku akuletee mteja wa uhakika wa bidhaa zako.

Hakikisha una 'maintain' ubora wa bidhaa zako, ikiwa ni kupokea 'customers feedback' juu ya kile unachozalisha. Hakikisha na usafi pia.

Hakikisha unakuwa na varieties za bidhaa unazozalisha, usiishie kwenye sembe tu, unaweza kuongeza dona, unga wa dengu, ung wa mihogo, mahindi ya kukoboa nk.

Hakikisha pia unapanua soko nje ya mkoa. Huko ndiko biashara yako inakuwa na kujulikana.
 
Back
Top Bottom