Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ureni, Aug 1, 2011.

1. u

ureni JF-Expert Member

#1
Aug 1, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160
Wana JF wataalamu wa biashara na wale walioshawahi kuifanya biashara ya mashine ya kusaga naomba mnijuze inalipa?au itakua ni kupaka hewa rangi?na mashine ya kusaga na kukoboa zinapatikana wapi na bei yake ni shilingi ngapi?Na umeme wake ni wa phase ngapi?
Nina kasehemu kangu Goba nimejenga fremu za biashara kwa mbele nataka niweke mashine ya kusaga nyuma,naomba mnijuze kwa mwenye experience au idea.Natanguliza thanks.

2. MamaEE

MamaEE Senior Member

#2
Aug 2, 2011
Joined: Jun 2, 2011
Messages: 103
Likes Received: 5
Trophy Points: 0
Mimi sina experience illa nafikiria something similar huko mkoani. So far ninajua costs of the machines at University of Dar es Salaam Technology Development and Transfer Center (TDTC) ni as follows:
A) MAIZE MILLER
Model mm 500/18.5
Capacity (kg/hr) 500
Power Input 18.5 kW 3 phases
Dimension (mm) 1400*1000*900
Weight (kg) 290
Price: Tshs.2,100,000/=B). MORTAR HP 25 USED FROM UK.
Price: Tshs.1,500,000/=
TOTAL TSHS. 3,600,000/=
C). MAIZE HULLER/DE-HUSKING MAIZE
Model HL 500
Capacity (kg/hr) 500
Power Input 11 kW 3 phases
Price: Tshs.1,560,000/=
D). MORTAR HP 15-20 USED FROM UK.
Price: Tshs. 900,000/=
TOTAL TSHS.2,460,000/=
GRAND TOTAL FOR A, B, C, AND D: TSHS. 6,060,000/=

Kila ka kheri... I would also like to hear from others wenye experience na hili zoezi.

3. Dr wa ukweli

Dr wa ukweli JF-Expert Member

#3
Aug 2, 2011
Joined: Feb 28, 2011
Messages: 892
Likes Received: 27
Trophy Points: 45
hapo knye rangi sijakupata ndio bness gani hiyo??

4. M

MIGNON JF-Expert Member

#4
Aug 2, 2011
Joined: Nov 23, 2009
Messages: 2,587
Likes Received: 1,563
Trophy Points: 280
Nina uzoefu kidogo na ninazo mbili katika location tofauti vijijini na si mjini.
Nakuomba uchunguze sana upatikanaji wa mahindi katika sehemu unayotaka kuweka.Ikiwa upatikanaji sio reliable nakushauri uachane na mradi huo na uweke mashine ya kuranda mbao,construction industry inakuwa kwa kasi mijini.
Kuhusu upatikanaji,maduka yako mengi sana na mojawapo maarufu lipo Morogoro road karibu na jengo moja jipya (sikumbuki jina) ambapo wanauza vifaa vya umeme (tronic).Motor ya hp 20 ex China ni around 70000/- na kinu cha kusaga na kukoboa ni almost same price,500000/- kila kimoja ingawa kila baada ya miaka miwili itabidi ubadili,sio imara kabisa!!!
Naamini itakusaidia na achana na huyo mchangiaji ambaye anwaza naniiiiiiiiiiiiiiiiiii
Mashine zangu zinaleta at least shillings mia nane kwa unit moja ya umeme na umeme unaohitajika ni three phase.

5. Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu JF-Expert Member

#5
Aug 2, 2011
Joined: Oct 12, 2010
Messages: 4,986
Likes Received: 427
Trophy Points: 180
Kwanza wewe unaye tafuta kuwekeza kwenye mashine ya kusaga, hiyo lugha ya kupaka rangi upepo itakukosesha watu wa kukusaidia. Labda niseme hivi mimi ninao uzoefu wa mashine ya kusaga.
Kusema ina faida ni kweli ina faida saana tu!!!!!!!! Maelekezo ya msaada:-
1. Jenga banda imara na store ya kuweka mahindi na pumba, safe storege kwa mazao ya mud mrefu.
2. Funga umeme wa three phase watu wa umeme watakuelewesha.
3. Nunua mashine yaani kinu cha kusaga size 75 kama uwezo ndogo anza na size 50.
4. Nunua motor size HP 25 au HP30 iwe china siemens Germany au Borch au England bora matunzo mazuri.
5. Nunua kinu cha kukoboa size 50 na motor HP 15.
Tangaza biashara yako kwa majirani na watu wa mbali.
Pata kijana au vijana waaminifu wa kufanya kazi vinginevyo utafanyia upepo kama ulivyo tangulia kusema, uwajalibu kwanza.
Faida kubwa ya machine iko kwenye pumba.Jiandae ubarikiwe.

6. Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu JF-Expert Member

#6
Aug 2, 2011
Joined: Oct 12, 2010
Messages: 4,986
Likes Received: 427
Trophy Points: 180
Huyu jamaa ureni yupo au alipitia tuu, ana mambo yake???????????

7. BONGOLALA

BONGOLALA JF-Expert Member

#7
Aug 2, 2011
Joined: Sep 14, 2009
Messages: 13,785
Likes Received: 2,395
Trophy Points: 280
usijaribu kununua kinu cha udsm,nunua kwa mafundi wazoefu mtaani!pia jiandae kuchakachua umeme bila kufanya hivyo faida yote wataila tanesco

8. Dr wa ukweli

Dr wa ukweli JF-Expert Member

#8
Aug 2, 2011
Joined: Feb 28, 2011
Messages: 892
Likes Received: 27
Trophy Points: 45
mkuu umeelezea vizuri sana naona hii bness haihitaji mtaji mkubwa ukiwa na M4 unaweza kuanza natakanifungue yangu maeneo ya Manzese ya kusaga na kukoboa pale bness ipo!

9. L

Lutifya JF-Expert Member

#9
Aug 2, 2011
Joined: Jan 6, 2011
Messages: 253
Likes Received: 174
Trophy Points: 60
Nina uzoefu kiasi na biashara hiyo. Pia nimewahi kufanya kazi SIDO kwa muda mrefu kama Mhandisi na nimetengeneza sana mashine za kusaga na kukoboa. Basically ni biashara nzuri kama una capital ya kutosha kwa maana kwamba uwe na storage facility ya mahindi. usisubira mahindi toka kwa madalali. Uwe na wazo la packaging na sio usubiri watu wanye kusaga kwenye viroba. Nakushauri pia nunua mashine toka Workshop ya SIDO moshi au Arusha wana mashine imara sana. UDSM mashine zao sio nzuri sana!!!!!. Nunua kinu cha kusaga namba 75 au 100 na cha kukoboa rola 3 na funga Mota za Horse power 25 au 30. Muhimu pia ni kuwa uaminifu wa wasagaji ni asset kubwa sana ingawa unaweza kuntrol wizi kwa kulinganisha unit zilizotumika na kiasi cha mifuko kilichozalishwa. Kwa matumiza mazuri gunia moja kusaga na kukoboa usitumia umeme zaidi ya unit 7(kwh) kwa mota ya Hoers power 25.It is a good and lucrative business if you have capital and markeing strategy. Try now.

10. Dr wa ukweli

Dr wa ukweli JF-Expert Member

#10
Aug 2, 2011
Joined: Feb 28, 2011
Messages: 892
Likes Received: 27
Trophy Points: 45
mkuu maeleo mazuri ntapata mchanganuo wa makadirio ya bei! ubarikiwe sana nataka nitie maguu kyenye hii bness

11. u

ureni JF-Expert Member

#11
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

Asante sana kwa ushauri mamaEE lakini naona inatumia umeme mkubwa sijui kama italipa.

12. u

ureni JF-Expert Member

#12
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

MIGNON nimepata mawazo hapa nafikiri itakua bora ni nunue hii mashine ya bei poa itakayodumu kwa two years nisikilizie biashara itakuaje kwanza,ndipo baada ya miaka miwili nikiona mwelekeo unalipa niupgrade,lakini mia 8 kwa unit ya umeme imenitisha tena manake inaonekana kama nitakua nafanyia kazi umeme tu,bila faida.

13. u

ureni JF-Expert Member

#13
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

Asante sana kwa ushauri hapo nimekuelewa vizuri kwa maana nyingine kwenye hii biashara kupata hasara sio rahisi,mie kitu ambacho nawasiwasi nacho hapa sasa hivi ni umeme,labda garama za umeme zinaweza kuwa kubwa sana.

14. u

ureni JF-Expert Member

#14
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

Kweli JF nimeikubali kuna wataalamu,hapo kwenye packaging nimeipenda sana,kwa idea hiyo naweza kupata sana manake naweza kusaga nikaweka kwenye package nikasambaza,mambo yakawa safi,asante sana mkuu,nikishaanza hii biashara nitarudi kuwapa feedback ya progress.Nashukuru sana,Je mambo ya leseni yanakuaje? Na ni kiasi gani?

15. Mtumishi Wetu

Mtumishi Wetu JF-Expert Member

#15
Aug 2, 2011
Joined: Oct 12, 2010
Messages: 4,986
Likes Received: 427
Trophy Points: 180
TANESCO watakufungia mita mpya ambayo readings zake ni kule HQ yao, hivyo you will get the bills from HQ no kuchakachua, ni kama LUKU. Ongea na TANESCO!!!!!!!!!

16. Candid Scope

Candid Scope JF-Expert Member

#16
Aug 2, 2011
Joined: Nov 8, 2010
Messages: 11,896
Likes Received: 119
Trophy Points: 160
Pamoja na kutokuwa na uzoefu wa biashara aina hiyo, lakini nimeshuhudia uendeshwaji wa biashara hii nikiwa katika kampuni inafaa sana tu.l
Jaribu kubadili kidogo mtazamo na matarajio ya biashara yakio na geukia upande wa pili kwa kujenga dhamira ya kujiamini zaidi ili ufanye makubwa.
Usifikirie watu wakuletee mahindi ili ukoboe na kusaga, ila hilo liwe second target.
• Kwanza fikiria kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata mahindi na ikiwezekana kulima shamba lako mwenyewe na ya kununua iwe nyongeza tu.
• Pili fungua macho yako kwenye taasisi na vyuo na fanya utafiti utaona wanaweza kuwa soko lako ya uhakika ukiingia mkataba nao
• Tatu buni packaging ambayo itakuwa labeled na shirika la viwango ili kurudufu ubora wa bidhaa yako unaweza kuwa na soko hata kwenye supermarkets
• Nne wateja wengine wawe extra income baada ya kujiridhisha kuwa na uhakika wa kuendesha biashara yako hata kama unakuwa na upungufu wa wanaokuja kutumia vinu vyako.
Nikuhakikishie tena jiamini na jenga moyo wa kufanya makubwa, Kama Mungu yuko upande wako hakuna lisilowezekana, ila uwe tayari kuruka vihunzi kabla hujafikia mafanikio.

Penye nia pana njia

17. N

Ninaweza JF-Expert Member

#17
Aug 2, 2011
Joined: Dec 14, 2010
Messages: 7,176
Likes Received: 1,177
Trophy Points: 280
Zingatia kuna mgao wa umeme mkuu au goba haujafika

18. u

ureni JF-Expert Member

#18
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

Na kuchakachua ni nzuri lakini ubaya wake wakikustukia faini yake ni kubwa sana kuna mama mmoja boss wa Tanesco nilimgusiaga kuhusu kuchakachua akaniambia niachane nayo manake wakishtukua faini ni kubwa,inaweza fikia milioni tano.

19. u

ureni JF-Expert Member

#19
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

Kuhusu mgao wa umeme najua utakuja kuisha tu siku moja hauta dumu milele

20. u

ureni JF-Expert Member

#20
Aug 2, 2011
Joined: Jun 14, 2011
Messages: 1,272
Likes Received: 232
Trophy Points: 160

Asante sana wana JF nazidi kupata mawazo mazuri sana la kampuni ni lamaana sana,kwa hiyo nitaweza kuwa na packaging zenye nembo ya kampuni yangu na kusambaza sehemu mbalimbali mjini,hapo nimekupata.Suala la kutafuta masoko kwenye taasisi na mavyuo nalikubali na kushukuru kwa ushauri mzuri sana ntaufanyia kazi.Lakini kwenye kulima naogopa sana manake kuna mjomba wangu mmoja alikopaga fedha nyingi benk kwa ajili ya kilimo,akachukua hecta kama 100 kwa ajili ya kilimo alikua anajiitaga mkulima bora,akalima mahindi shamba lote kwa kweli majirani wote walimkubali wakawa wanamwita investor,ikaja kitu moja inaitwa mvua ya alninyo mbona alikuwa mdogo kama piriton na pressure juu hakupata hata ya ushaidi,kwa hiyo toka enzi hizo ukiniambia suala la kulima linaniwia gumu.

Loading...