Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

Wazoefu wa hii biashara tafadhalini tupeni mchanganuo wa gharama za uendeshaji na faida.
Najua faida si kubwa kiviile ila si mbaya mkatupatia maelezo yakinifu ili tusiwe tunabahatisha.
Chonde chonde.....🙏🙏🙏
 
Naomba nikuelekeze gharama za uendeshaji, gharama si kubwa maana gharama zote zinaingia kwa mlaji mfano umeme,usafiri,mifuko,maji n.k

Unachotakiwa kuzingatia ni mahindi
Mahindi mazuri yatatoa wastan mzuri yakitoa wastani mzuri ndio yayakupa faida nzuri
Mahindi mazuri yanayotoa wastani mzuri ni ya Kibaigwa haya yanatoa wastani kuanzia 68 mpk 75
Maana yake asilimia 75 ni makande(unga) alisimia 25 ni pumba
Ukipata mahindi ambayo ni chini ya wastani wa 65 achana nayo vinginevyo ununue bei ya chini sana ili isikukate ukala hasara
Maana hapo utapanda pumba nyingi kuliko unga
Pia kuna swala la bei inabidi ucheze nalo sana kama unavyoona kwenye maduka ya kubadilisha pesa na soko la mahindi liko hivyo hivyo
Tena hapa ndio kuna kasheshe kwelikweli maana unaweza ukanunua mzigo wako Leo kwa bei ya sh 450 (mfano) kesho ukasikia bei ni 430 Mara nyingine huwa inapanda kwahiyo ikipanda faida kwako ikishuka itakupa stress maana ww utauza unga wako kwa bei ya juu kidogo kuliko wenzako ambao wamenunua kwa bei ya chini hivyo bei yao itakuwa chin kidogo
Kwamaana hiyo tahadhar ni muhimu sana kwa nunua mahindi kwa bei ya chin kidogo ili hata yakipanda usiathirike
Na hapa pia itategemea sana usukumaji wako was mzigo sokoni (hapa kuna mambo mengi ya kujua)
Utatengeneza faida nzuri sana ukienda kununua mzigo mwenyewe mkoani badala ya kununua kwa madalali manzese.

Niishie hapa kwanza
 
Habari wana JF

Nahitaji kuanzisha kiwanda kidogo cha sembe na dona je ninahitajika vibali gani au niweke kwanza majengo na mashine.

Je mtaji kiasi gani?

Location ni Kibaha msaada zaidi sifahamu chochote nabje raw materials nitapata wapi?
Hii ni biashara nzuri sana na ina ela, kama unataka kuifanya usianze kwa kununua mashine na vitu vingine gharama ni kubwa mno na hutaweza kuifanya na kuona faida kama unavyodhan hii biashara ina mambo mengi kama zilivyo biashara nyingine
Nikushauri kitu tafuta mashine itakayoweza kusaga na kukoboa bidhaa yako alafu ingiza sokoni
Manzese zipo mashine unanunua mzigo wanakukobolea na kukusagia then unaingiza sokoni mzigo
Ila kuna mahesabu yake
 
Aisee!
 
Biashara kichaa watu hawaijui tu. Utahitaji vibali si chini ya 7 kuanzia halmashari mpaka TFDA
 
Samahani mkuu... una uzoefu na hii biashara? Na ni biashara kichaa kivipi? Tujuze kidogo kabla hatujajiingiza huko
Kuna urasimu mwingi sana. Mimi vibali tu kulipia na kodi halmashauri ilikuwa naripa kama 4m. Hii ni faida ya mwezi mzima. Jamaa wa sijui mazingira wakikuibukia ndo utajuta, hawajaja jamaa wa TFDA. Niliamua kustopisha uzalishaji mashine nikapeleka kijijini iwasaidiage wazee.
 
Poleni na majukumu ya ujenzi wa taifa ndugu wasakatonge wenzangu:

Nina mpango wa kufungua mashine ya kusaga na kukoboa nafaka. Hivyo ninahitaji kujua ni vitu gani muhimu vya kuzingatia kabla sijaanza process yaani

1. Bei za vifaa kama motor; wiring nk

2. Mtaji wa kuanzia ili nione kiasi nilichonacho kama kinatosha

Kwa wenye ufahamu na hii biashara karibuni mnidadavulie. Pia kama wewe ni mfanyabiashara wa vifaa hivyo tutawasiliana nije nikuungishe.

Shukrani.
4mil complete kwa mota na mashine ya hp kubwa

Luckman1
 
Habari zenu wadau.

Ninataka kuanzisha biashara ya kusaga nafaka, na kuuza unga kwa kuweka kwenye vifungashio.

Ninaomba kufahamu bei ya mashine za kusaga mahindi size 100 na size 75 ninaweza kupata kwa kiasi gani.

Pia nipate na bei za mashine za kukoboa roller 3 au roller 2.

Ahsanteni sana.
 
Back
Top Bottom