Kilimo cha Maharage: Mbinu za kulima, Ushauri na Masoko yake

Duhh Tani 5 halafu unasema kuwa hapo ndio ulilima kwa changamoto! !!


Mkuu si mihela hiyo? ...

Uko mkoa gani mkuu ? Jaribu kwenda katika masoko makuu ya mkoa ambao upo kisha watafute madalali Bila Shaka wataweza kutatua Tija yako
nafikiri kuna wakati unakurupuka kukomenti bila kusoma uzi. hivi juaoona kasema amelima Gairo ?
 
Habari za saa wakuu wangu?

Bila kupoteza muda niende katika jambo husika kwenu wahenga na wasamaria mnisaidie maarifa...

Wakuu kama mhitimu bila kupoteza muda ktk kutafuta na kusubiri kupata ajira mwaka huu nilifanya maamuzi ya kuwekeza fedha yangu ya akiba ktk kilimo cha maharage huko Gairo Morogoro, namshukuru Mungu pamoja na changamoto za ukosefu wa mvua nimefanikiwa kupata mavuno yakuridhisha kiasi chake, nililima maharage ya njano na soya... Ktk hali ya ugeni ktk sekta hii na changamoto katika kumuuguza mama ambae kwa mapenzi ya Mungu aliona mama apumzike sikufanikiwa kufanya tafiti za kutosha juu ya soko la maharage

Sasa nimevuna na ninao mzigo kubwa wastani wa tani 5 na bado sijamaliza kuvuna ni maharage ya soya na njano, kwa yeyote mwenye kujua soko lake kwa wafanyabiashara ama taasisi yoyote tafadhali niunganishe nao, natanguliza shukrani za dhati

1 kg ni 1400 bei yaweza kupungua kulingana na ukubwa wa mzigo pia tutaweza fanya kazi endelevu hata baada ya msimu kupita, gharama za usafiri kwa asilimia kubwa zitakuwa kwangu, karibu pm mkuu
Hayo maharage ya njano....ni yale manene-mafupi au membamba-marefu?

Njoo pm nitakupa contacts tuwasiliane.
 
Salaam kwenu wadau wa kilimo cha maharage ya njano.Ninaomba ushauri na mchanganuo nasaha kuhusu kilimo cha umwagiliaji wa maharage ya njano.
.
1)Mbegu zapandwa kg ngapi kwenye ekari1
(2)Tuta liwe na urefu/upana wa inch ngapi?
(3)Aina ya mbolea zinazofaa.
(4)Ekari1, kwa makisio ya chini,wawezapata magunia mangapi?
5)Mbinu zakutumia zinazoweza kunihakikishia mavuno mazuri ni zipi?

Natanguliza ahsante
Wenu,
INVESTPHILE
Usa River,Arusha
 
Ndugu zangu wanajamvi nimepata eneo ekari 2 nataka kulima Maharage shida ni makisio ya. mbegu kiasi gani ninunue? Je ni hatua zipi (spacing) zinashauriwa kitaalamu?
 
Habari ya leo ndugu wakulima,naomba kujuzwa kuhusu kilimo hichi hasa kwa mikoa ya iringa na mbeya
-upatikanaji wa mashamba na gharama za kukodi kwa ekari
-gharama zake mpaka kuvuna
-msimu wa kilimo icho kwa mkoa husika


Asanteni.
 
Kupata usaidizi kwenye mambo kama haya ni ngumu kwa sana kwa sasa.

Hebu 'search' kilimo husika kwenye hili jukwaa uone kama utaweza kupata dondoo mbili tatu.

Watu wako MMU.
 
Habari zenu wakuu nilikua naomba kuuliza kwa wadau mliopo ndani ya mkoa wa njombe kuhusu kilimo cha maharage ya njano....

Je...
Maharage hayo yanastawi vizuri huko njombe.!?
Vipi soko lake!?
Gharama za kuuza maharage ya njano kwa gunia lenye debe sita...?
Gharama za uendeshaji!?
Gharama za kukodi shamba!? Na ni eneo gani linafaa kwa kilimo hicho!?

Natanguliza shukran za dhati.
 
Habari zenu wakuu nilikua naomba kuuliza kwa wadau mliopo ndani ya mkoa wa njombe kuhusu kilimo cha maharage ya njano....

Je...
Maharage hayo yanastawi vizuri huko njombe.!?
Vipi soko lake!?
Gharama za kuuza maharage ya njano kwa gunia lenye debe sita...?
Gharama za uendeshaji!?
Gharama za kukodi shamba!? Na ni eneo gani linafaa kwa kilimo hicho!?

Natanguliza shukran za dhati.
Mkuu, binafsi nataka kutinga kwenye hiki kilimo, japo sijapata taarifa zaidi kuhusu njombe. Nataka kulima Arusha, labda kama kuna wadau wanajua zaidi kuhusu hii mishe kwa pande za njombe tunaomba msaada watujuze tujifunze zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom