Kilimo cha Maharage: Mbinu za kulima, Ushauri na Masoko yake

Unaweza kulima kwa greenhouse na makisio ya gharama ya greenhouse ya hekari 2 ni tshs ngapi na unaweza kupata ngunia ngapi kipindi cha mavuno?
Ni heka siyo hekari.......Ekari moja ni kilo 600 mpk 1200 mavuno......heka moja ni sawa na Ekari 2.5 sasa hapo jipigie mahesabu mwenyewe.
 
Ni heka siyo hekari.......Ekari moja ni kilo 600 mpk 1200 mavuno......heka moja ni sawa na Ekari 2.5 sasa hapo jipigie mahesabu mwenyewe.
Hecter na acre.hecter 1 ni acre 2.5 kama ndivyo basi maharage hayana dili hecter 1 kilo 600 kuna faida hapo?
 
KILIMO BORA CHA MAHARAGE (Phaseolus vulgaris)

UTANGULIZI

Maharage ni zao jamii ya mikunde ambalo hulimwa kwa ajili ya kuliwa kama mboga au futari.linaweza kama maharage mabichi au maharage makavu.Pia majani yake mni chakula cha mifugo na yanatumika pia kama mboga kwa binadamu.katika ekari moja unaweza kupata Kg 600 hadi 1200 za maharage.

HALI YA HEWA IFAAYO
Hustawi vizuri maeneo yenye mwinuko wa mita 1000 hadi 2000 kutoka katika usawa wa bahari .Pia yanaweza kulimwa pungufu ya mita 1000 au zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari.Maharage huitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya maharage.Huitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua na ukavu kipindi cha kukomaa na kukauka vitumba.Maharage hulimwa kwa wingi MBEYA,IRINGA,KIGOMA,ARUSHA,MOSHI,morogoro n.k

UDONGO
Hustawi vizuri katika udongo usiotuamisha maji na ambao ni mfinyanzi kichanga ambao una mboji ya kutosha wenye pH 5.5 - 7.Pia unaweza kulima katika udongo wa aina tofauti tofauti.

MBEGU BORA ZA MAHARAGE
Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za maharage kama vile canadian wonder,Tengeru,Uyole,SUA,Ilonga na Lyamungo.

UPANDAJI
Maharage hupandwa mwishoni mwa msimu wa www.kilimofaida.blogspot.commvua kuepusha kunyeshewa kipindi cha uekaji maua.Yanawezwa kupandwa mwezi Februari,machi,aprili inategemea mvua katika eneo lako zinaisha mwezi gani,hivyo hakikisha angalau yanapata mwezi mmoja wa mvua ya kutosha.Fukia mbegu zako katika kona cha sm2.5 hadi 4 katika ardhi kutegemea na aina ya udongo shambani kwako.

Maharage hupandwa kwa kutumia mbegu ambazo ni safi na hazijaharibika kwa kuvunjika au kuliwa na wadudu.Kabla ya kupanda maharage yako unaweza kuyatibu kwa kutumia Rhizobia bacteria ambapo itakupunguzia matumizi makubwa ya mbolea za nitrojeni.

NAFASI YA UPANDAJI
Maharage yapandwe kwa nafasi ya sentimeta 40-60 mstari hadi mstari na sentimeta 8 -15 shina hadi shina.

MBOLEA
Unaweza kupanda katika shamba lililotawanywa mbolea ya samadi.
Pia uanweza kwa uzuri zaidi kupandia mbolea za viwandani kama vile TSP au MInjingu mazao au minjingu kwa kiasi cha kg 50 -100 kwa ekari.

Wakati wa mmea kuanza kuweka maua unaweza kutumia mbolea ya N.P.K au SA au Kwa Kiasi Kidogo CAN au UREA Angalizo Mbolea hizi zikizidi maharage huwa na majani mengi kuliko maua na kusababisha mavuno kuwa machache.

UPALILIAJI
Upaliliaji inabidi ufanyike mapema mara tuu maharage yanapoota na kshamba kuwa na magugu.Palizi ya kwanza inaweza kufanyika Kati ya siku 8-12 baada ya mmea kuota na yapili ifanyike siku ya 20- 30 baada ya palizi ya kwanza.ILi kuyarinda maua ya maharage yako yasipukutike wakati wa palizi hakikisha unaepuka palizi kipindi cha uwekaji maua.

WADUDU
Funza wa maharage ni wadudu wanaoshambulia mimea michanga ya maharage. Funza wa maharage hawa huweza kusababisha uharibifu hadi kufikia asilimia 100 kufuatana na hali ya hewa-unyevu kidogo, rutuba kidogo, kuwepo kwa maotea ya aina ya maharage na magonjwa kwenye udongo, kurudia kupanda zao la maharage kila msimu na aina ya naharage.

Njia nzuri ya kudhibiti funza wa maharage ni:-
1. Kupanda mapema
2. Kupakaza mbegu dawa kama endosufan, Acephate, Murtano (mchanganyiko wa dawa ya fungas na wadudu) nasaidia kuzuia funza wa maharage na visababishi vya kuozesha mizizi.
TAHADHALI: Dawa ya Murtano ni sumu kali hivyo mbegu zenye dawa hii zisitumike kwa chakula.
3. Kunyunyizia dawa mfano DUDUBA au DUDUALL Karate 5EC au Actellic 50EC ndani ya siku 4 hadi 5 baada ya maharage kuota.
4. Kupanda mbegu zenye afya kwenye udongo wenye rutuba.
5. Kupanda mbegu zenye ukinzani wa funza wa maharage.
6. Kuweka matandazo kama pumba ya mpunga husaidia kuotesha mizizi mipya n kurudisha afya ya mmea wa maharage

Pia maharage yanaweza kushambuliwa na wadudu mbalimbali kama vile nzi weupe wa maharage na wengineo ambao wanweza kuzuiwa kwa kutumia dawa mbalimbali za wadudu.

MAGONJWA
Magonjwa maarufu ni ndui ya maharage, madoa pembe, kutu, magonjwa yanayosababishwa na bacteria na virusi. Mbegu iliyoambukizwa, udongo na takataka za maharage ni vyanzo vikubwa vya uambukizaji kwa magonjwa yote isipokuwa ugonjwa wa kutu ya majani.
1. Punguza athari kwa kupanda mbegu safi, zenye afya zisizo na vidonda/ magonjwa, aina zinazovumilia na kutunza shamba.
2. Panda kwa mzunguko wa mazao ya jamii nyingine.
3. Ondoa na kuchoma yaliyougua.
4. Tumia dawa zilizopendekezwa kama Kocide, Funguran, Bayleton n.k kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na bacteria.

UVUNAJI
Maharage huvunwa mara tuu yanaponza kukauka na kabla vitumba havijapasuka.Ng'oa mashina ya maharage na na upigepige kuyaondoa katika vitumba vyake.

KUHIFADHI
Baada ya kuyapiga na kupeta kuondoa uchafu yaanike juani kwa siku kazaa kuhakikisha yamekauka na hayana unyevu unaoweza kusababisha yapate fangasi.yahifadhi katika magunia,kama yatakaa muda mrefu bila kuliwa basi hakikisha unayahifadhi kwa kutumia dawa za kuulia wadudu kama vile Shumba, Kama vile ACTELLIC DUST au MALATHION. au Tumia mifuko maalum ya kuhifadhia nafaka.
Kilimo cha magazetini kitamu sana ila utamu wa ngoma anajua mchezaji
 
Habari za saa wakuu wangu?

Bila kupoteza muda niende katika jambo husika kwenu wahenga na wasamaria mnisaidie maarifa...

Wakuu kama mhitimu bila kupoteza muda ktk kutafuta na kusubiri kupata ajira mwaka huu nilifanya maamuzi ya kuwekeza fedha yangu ya akiba ktk kilimo cha maharage huko Gairo Morogoro, namshukuru Mungu pamoja na changamoto za ukosefu wa mvua nimefanikiwa kupata mavuno yakuridhisha kiasi chake, nililima maharage ya njano na soya... Ktk hali ya ugeni ktk sekta hii na changamoto katika kumuuguza mama ambae kwa mapenzi ya Mungu aliona mama apumzike sikufanikiwa kufanya tafiti za kutosha juu ya soko la maharage

Sasa nimevuna na ninao mzigo kubwa wastani wa tani 5 na bado sijamaliza kuvuna ni maharage ya soya na njano, kwa yeyote mwenye kujua soko lake kwa wafanyabiashara ama taasisi yoyote tafadhali niunganishe nao, natanguliza shukrani za dhati

1 kg ni 1400 bei yaweza kupungua kulingana na ukubwa wa mzigo pia tutaweza fanya kazi endelevu hata baada ya msimu kupita, gharama za usafiri kwa asilimia kubwa zitakuwa kwangu, karibu pm mkuu
 
Habari za saa wakuu wangu?

Bila kupoteza muda niende katika jambo husika kwenu wahenga na wasamaria mnisaidie maarifa...

Wakuu kama mhitimu bila kupoteza muda ktk kutafuta na kusubiri kupata ajira mwaka huu nilifanya maamuzi ya kuwekeza fedha yangu ya akiba ktk kilimo cha maharage huko Gairo Morogoro, namshukuru Mungu pamoja na changamoto za ukosefu wa mvua nimefanikiwa kupata mavuno yakuridhisha kiasi chake, nililima maharage ya njano na soya... Ktk hali ya ugeni ktk sekta hii na changamoto katika kumuuguza mama ambae kwa mapenzi ya Mungu aliona mama apumzike sikufanikiwa kufanya tafiti za kutosha juu ya soko la maharage

Sasa nimevuna na ninao mzigo kubwa wastani wa tani 5 na bado sijamaliza kuvuna ni maharage ya soya na njano, kwa yeyote mwenye kujua soko lake kwa wafanyabiashara ama taasisi yoyote tafadhali niunganishe nao, natanguliza shukrani za dhati

1 kg ni 1400 bei yaweza kupungua kulingana na ukubwa wa mzigo pia tutaweza fanya kazi endelevu hata baada ya msimu kupita, gharama za usafiri kwa asilimia kubwa zitakuwa kwangu, karibu pm mkuu
Nenda sokoni kwa uhakika zaidi
 
Duhh Tani 5 halafu unasema kuwa hapo ndio ulilima kwa changamoto!

Mkuu si mihela hiyo?

Uko mkoa gani mkuu? Jaribu kwenda katika masoko makuu ya mkoa ambao upo kisha watafute madalali Bila Shaka wataweza kutatua Tija yako
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom