Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
34,982
70,142
Sijui nyie hii biashara mnaifanyaje,,, kama mnunuaji lazima kila leo uwe na update ya bei ya siku kila leo isipokuwa jumapili lazima ujue bei sokoni ikoje, na uweze kulisoma soko linaenda kupanda ama kushuka, we utanunuaje bila kujua unaenda kuuzaje???

Dhahabu kupungua uzito inategemeana mfano hizi za kukamatisha na mercury unapaswa uichome haswaa tena kwa mkaa wenye nguvu uhakikishe mercury yote imeisha ukiitoa dhahabu ikiwa njano iliyokolea ile kama inaenda kuwa red ama brown hivi hiyo imeiva vzr japo wachimbaji wanakuwa wakali ila inabidi ukomae nao mana wao wanataka ubabue ili mercury iwabebe ila ukichoma vzr hata kama ni dungu la gram 40 halitopungua zaidi ya point 5 au chini zaidi, zile zisizokamatishwa zinapungua kama mtu hukupuliza vzr yaan umenunua zikiwa na uchafu mwingi hivyo zikichomwa ule uchafu ukitoka ndio zinapungua kulingana na uchafu uliokuwepo au kuzidi hapo ila ukizipuliza vzr huwa hazipungui sana

Hahaah tunaandika tunachopractc dogo. Unanunua Leo mzigo tuseme mwingi wa 2m! Umebakiza tuseme laki7 tu, kesho kitu unaona kimedrop. Kesho yake Tena kimedrop, wanauza kwa faida ndogo mradi aende Tena kukusanyia mzigo eish bye! Nini apps!tajiri anapanha Bei hutak kwenda.
 

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
625
1,023
Samahani..hapo ulisposema uzidishe 1000 sio wizi, au?
Hpn sio wizi mfano sasa ukidhamini gram unalipa laki na 10 yaani elfu 11 kwa kila point ila ww ambae hudhamini hutaki kurisk hela yako inabidi ununue laki na 20 yaan elfu 12 kwa point, ndio iliyokuwa mantiki yangu lazima uzidishe bei ili upate mzigo.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
34,982
70,142
Hpn sio wizi mfano sasa ukidhamini gram unalipa laki na 10 yaani elfu 11 kwa kila point ila ww ambae hudhamini hutaki kurisk hela yako inabidi ununue laki na 20 yaan elfu 12 kwa point, ndio iliyokuwa mantiki yangu lazima uzidishe bei ili upate mzigo

Conclusion hapa biashara ya dhahabu ni very risky. Bora kukimbiza mwalo au ununue vifusi uwe mtaalam wa kujua Kama Kuna kanjanja. ..Tena techniques zako za kizaman. Unampa mtu mtaji anakuletea kidhahabu kichafuuu. Anakuletea point 2! Na hapo umempa hela ya gram nzima mtaanza zungushana weee!

Ukitaka upate faida nunua dhahabu kubwa kubwa hivyo vipoint ndo vby balaa! Na ukitaka uchukue hizo ndogondogo ukubali..kumuibia. mie naongelea wauzaji dhahabu wewe unaleta habar za wapiga fonka.
 

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
625
1,023
Hahaah tunaandika tunachopractc dogo. ..unanunua Leo mzigo tuseme mwingi wa 2m! Umebakiza tuseme laki7 tu...kesho kitu unaona kimedrop...kesho yake Tena kimedrop...wanauza kwa faida ndogo mradi aende Tena kukusanyia mzigo eish bye! Nini apps!tajiri anapanha Bei hutak kwenda

Yaani ww ni mbishi mjuaji bila sababu ....ukishaona mgodi dhahabu zake chache percentage za kufeli ni100/-%. Yaan kwa siku unashundia gram 7! Faida hapo si ya kula tu. Lol.tembeaga uone. Kuna machaka purity had 68%>>sema umekuja kubishana nakuangalia tu

Mpaka hapa meshaona tofauti ilipo na hivyo sistahili kubishana na ww wala haikuwa lengo langu hope yupo aliyejifunza kitu and let me end this by saying your right.
 

Phanwonderz

Member
Oct 4, 2018
54
29
JAMANI MALINYI MISEGESE KUMEHILA,(KUMELIPUKA DHAHABU)
wale wenye kusimika Gest mpooo...
Wenye mpesa..
Kuweka plant..
Makota
Mama lishe. ! Huu ndo wakati wa kutengeneza pesa wakati mgodi wa motomoto...! Mie soon nafika huko ntawapa mrejesho...lols!

Kumelipuka lini bro?? pia naitaji ushauri wako naona pm kuna bomba la ... br naitji kujua ni kipi nifanye mgodini nina kam 300k naweza fanya issue gn nikatoboa,,vipi pia kuhusu fello zinafaidaa?? msaada wako mkuu.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
34,982
70,142
kumelipuka lini bro?? pia naitaji ushauri wako naona pm kuna bomba la br naitji kujua ni kipi nifanye mgodini nina kam 300k naweza fanya issue gn nikatoboa, vipi pia kuhusu fello zinafaidaa? Msaada wako mkuu.
Yaani nakushauri ni bora ukaenda kwanza kuchek Kuna fursa gan huko unaweza ifanya. Malinyi ni mwezi huu huu! Bado oya oya Sana haujasettle.
 
Jun 15, 2020
24
89
Kuna alienda Malinyi atupe update? Na wale walioko Dar ambao wangependa twende tukaangalie fursa zilizopo na kujifunza kuhusu Mishe zoote za huko mgodini! Mm n mpenzi wa kujifunza kwa vitendo hvyo kupoteza hela za nauli kwenda kujifunza sio shida afu weng humu wanaume tunalala popote mbona tushapoteza pesa kibao kutafta elimu ambayo imeishia kutupa cheti na bado tunahangaika na ajira?

Aliyetayr anipm tupange safar tusepe ila nasubir mrejesho wa alieko huko! Na naomba ushauri nkitoka malinyi niende mgodi gan nzuri kwa kujifunza ujanja wote wa madini na kupiga pesa.
 

opondo

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
467
1,081
Doh huko malinyi hiko mkoa gani aisee nikawapelekee nguo na viatu? Nagraduate mwaka huu nipe mchongo kabla hii hela ambayo nimeisave aijaishaa..
Yaani nakushauri ni bora ukaenda kwanza kuchek Kuna fursa gan huko unaweza ifanya...malinyi ni mwezi huu huu! Bado oya oya Sana haujasettle.
 

mcrounmj

JF-Expert Member
Feb 26, 2016
370
846
Kk kama una mtaji tafuta eneo ambapo dhahabu inatoka kwa wingi nenda jenga kakibanda tega scale yako lipa bei nzuri wachimbaji watakuletea dhahabu bila kuhangaika na hela yako haitakata hata nukta

Angalizo:-

A. Ulizia kwa mtu unaemwamini dhahabu ya eneo husika ni safi kiasi gani/ purity % yake, hiyo itakupa muongozo wa bei ya kununulia + bei zinazotamba mtaani

B. Usimdhamini mchimbaji kbs we mwambie unanunua dhahabu tu na uzidishe kama 1000 toka bei ya kawaida

C. Uwe na mtu atakaekusaidia kuchoma na kupuliza madini yasiyokamatishwa na mercury hadi utakapozoea...

NB: Naongea kwa uzoefu wangu, 1 kuhusu return za karasha na risks zake 2, ni mnunuaji wa muda na faida yake naijua ila nakushauri kama una hela za mawazo achana na karasha uncertainty zake ni kubwa mno
Yes mzee baba. Mi nafikiri kuanza kununua dhahabu is better kuliko kuanza kuwa na Karasha. Karasha demands large capital na upo uwezekano ukashindwa kuliendesha kutokana na uzoefu zero au ukakuza mlima ambao hausomi au sampo ipo chini mno.

Kwahiyo kuanza na Karasha wakati hauna uzoefu ni kurisk pesa ndefu mno zaidi ya ten M, kitu ambacho bora ungeanza kununua dhahabu mtaji hata ukianza na two M, watakuwa wanakuliza humohumo wakati ukigeini experience, na kama uko makini haichukui muda kuelewa kila kitu na mwisho wa siku utaweza kuukuza mtaji wako plus uzoefu.

Baada ya kuwa papa katika ununuzi wa dhahabu tanua mawanda, nunua Karasha. Hii itakuwa na faida lukuki kwako kiuendeshaji, kwanza pesa ya kuendeshea Karasha utakuwa unatoa kwenye faida ya dhahabu, pili upataji wa mawe yenye sampo utakuwa umeshaelewa kulingana na kwamba wachimbaji uko nao kuliko ukiwa mgeni kabisa. Tatu sampo ya mawe ya kusaga utakuwa ushafahamu na hivyo kuepuka kukuza mlima ambao hauna sampo. Yangu ni hayo, "let meet at high chairs"
 

Almendezz

Member
Aug 17, 2020
47
48
Mimi nataka kujua zaidi kuhusu hiyo ya kuuza vilipuzi, compressors na madawa. Mtaji, changamoto na faida zake.

Na hiyo ya umiliki wa elution plant.
Vilipuzi na compressor mara nyingi huwa vinaenda sambamba. Mfano kuchoronga mwamba tundu moja bei yake average ni tsh 10,000. Ukimuwekea mtu na mlipuko ni 15,000. Hvyo kuchoronga na kulipua tundu moja inakuwa 25,000. Ila kumbuka mtu wako anayelipua lazma awe na certificate. Thats y sikushauri kuuza milipuko kama milipuko usije ukashikana mashati na mamlaka.
 

Almendezz

Member
Aug 17, 2020
47
48
Ungekua na picha mkuu tuwekee make wengine hawajawahi ona crusher yenyewe na mwalo ahsante sana

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG_20201126_020601.jpg


Hiyo ni aina mojawapo ya karasha kitaalamu inaitwa hammermill. Tofauti na nyingi zilizozoeleka hii inasaga mawe pamoja na maji na final product inatoa slurry (tope) ambalo linapita kwenye gunia kwa ajili ya kukamata dhahabu. Makarasha mengi yaliyozoeleka ni yale yanayotumia gololi na moja ya disadvantage zake ni kuwa udongo unapokuwa na maji inakuwa ngumu kdg kusaga mpaka ukaushwe.
 

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
8,114
13,150
Vilipuzi na compressor mara nyingi huwa vinaenda sambamba. Mfano kuchoronga mwamba tundu moja bei yake average ni tsh 10,000. Ukimuwekea mtu na mlipuko ni 15,000. Hvyo kuchoronga na kulipua tundu moja inakuwa 25,000. Ila kumbuka mtu wako anayelipua lazma awe na certificate. Thats y sikushauri kuuza milipuko kama milipuko usije ukashikana mashati na mamlaka.

Shukrani. Vp madawa ya uchenjuaji?
 

Almendezz

Member
Aug 17, 2020
47
48
Shukrani. Vp madawa ya uchenjuaji?
Nikirefer wachimbaji wadogo wengi wanashindwa kupeleka plant kufanya leaching kwa sababu ya cost kama chemicals, kumlipa mkemia na kukodi plant. Ndio maana mwisho wa siku wanaamua kuuza marudio yao.

Njia rahisi ya kupata faida kutoka kwenye chemicals baada ya kujiridhisha na report ya maabara ni kumkopesha mchimbaji then kugawana naye percentage. Though hata kama report ipo vzuri, mkemia naye anaplay role kubwa kufanikisha zoezi zima la uozeshaji.
 

Mb-one

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
847
1,120
View attachment 1634832

Hiyo ni aina mojawapo ya karasha kitaalamu inaitwa hammermill. Tofauti na nyingi zilizozoeleka hii inasaga mawe pamoja na maji na final product inatoa slurry (tope) ambalo linapita kwenye gunia kwa ajili ya kukamata dhahabu. Makarasha mengi yaliyozoeleka ni yale yanayotumia gololi na moja ya disadvantage zake ni kuwa udongo unapokuwa na maji inakuwa ngumu kdg kusaga mpaka ukaushwe.
Ulishawahi kusagia na maji kwenye karasha hizi za kawaida,faida yake na hasara yake ikojee.
 

Almendezz

Member
Aug 17, 2020
47
48
Ulishawahi kusagia na maji kwenye karasha hizi za kawaida,faida yake na hasara yake ikojee.
Hapana sijawahi kutumia karasha za kawaida. Ila wanaotumia ndio nimewaskia kuwa wanapata tabu kdg mawe yakiwa na maji. Labda walio na experience nazo humu watatupa details
 

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
3,157
4,408
Haya yote mnayojadili Bwana Dotto Biteko akijua... Maana sasa hivi wapo kasi sana kufukuzana nakuwekana ndani
 
2 Reactions
Reply
Top Bottom