Biashara ya Kuuza Nyama (Butcher's Shop): Mambo Mbalimbali ya Kujifunza

Mkuu hiyo biashara ni nzuri sana tatizo linokuja kudhoofisha biashara ni suala la Parking ya nyama

Changamoto kubwa hiko hapo bado wa Tz hatuwezi ku design parking nzuri ya product kama ya nyama ndio maana katika Supermarket zetu wanauza sana nyama ya Nje kwasababu ina kidhi viwango vya kimataifa

Ushauri wangu

1 Jenga banda sehemu yenye ardhi ya kutosha ambayo pia kuwe na Majani ya kutosha ( ranch kidogo hivi unakipiga na fensi)

2 Jenga Machinjio madogo ya kisasa

3 Tafuta alternative source of energy usitegemee umeme wa tanesco kwa sababu bucha za kisasa zinatumia mashine kukatia nyama na sio vigogo na hizo mashine zinatumia umeme kwaiyo ukitegemea umeme wa Tanesco unaweza ukakaa siku bila kufanya kazi

4 Kuusu Parking nenda TFDA kuna wataalam watakupa ushauri wa jinsi gani unaweza kufanya parking ya International standard

5 Usikope hela bank kwaajili ya kuanzisha biashara hii inaweza ikakugharimu biashara ikawa ngumu mwanzoni alafu jamaa wakaanza kukuchachamalia mwishowe ukamwaga manyanga

6 Fanya Study tour nakushauri nenda pale SUA ( Moro) yuko Professor mmoja Ana mradi mkubwa wa hii kitu na anapiga hela ndefu sana atakupa muongozo wa kila kitu usitegemee ushauri wa hapa Jf tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ushauri mzuri sana, nakufuata pm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama unaweza kufanya kila kitu kinachohitajika kwenye biashara hii kikamilifu, ni biashara nzuri. Unapaswa kuwa na mabucha yako, machinjio, maduka au wateja kama supermarkets. Pia unapaswa kuweza kukata nyama kitaalamu kwa kutumia machine na kuzipaki vizuri. Pia usisahau kwamba utahitaji freezers kubwa kuweza kuhifadhi nyama kabla ya kuuza.

Biashara hii inahitaji uwe na gari/magari yako, moja la kubeba ng'ombe na jingine kusafirisha nyama kwa wateja. Vyote hivi vinahitaji uwekezaji mkubwa.

Sikushauri uanze na ng'ombe 60 ni wengi mno kama huna miundombinu na nyenzo nyingine utapata shida na pengine hasara.
Ahsante kaka, ni miundo mbinu ipi ya ziada inayohitajika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom