Biashara ya kuuza na kununua biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,529
Leo nataka tujadili kidogo kuhusu biashara ya kuuza na kununua biashara.Sio bidhaa wala sio huduma bala ni biashara ndo inauzwa na kununuliwa.

Kwa wengin wanaweza kufikiri kwamba hili ni jambo jipya lakini hili jambo lipo sana na katika mfumo mkubwa basi tunauza na kununu kitu kinaitwa HISA.Leo sizungumzii hisa bali nazungumzia hasa uuzaji na ununuaji wa biashara ndogo ndogo.

Kuna sababu nyingi sana zinaweza mfanya mtu kutaka kuuza au kununua biashara ikiwamo,madeni,gharama za uendeshaji,kukosa mtaji wa kutosha,kukosa utaalamu na hata kukosa nia ya kutaka kuendelea na biashara na wakati mwingine ni kutaka kutafuta fursa nyingine.

Kwa kawaida,uuzaji na ununuaji wa biashara unaangalia mambo mengi ikiwamo kiwango cha ukwasi na madeni,idadi ya wateja/soko,gharama za uendeshaji,Umaarufu wa jina la biashara,Location ya biashara ilipo na vigezo vingine vingi vinavowezesha biashara kufanikiwa.

Kwa kawaida mchakato wa kuuza na kununua biashara unaweza kuwamrefu au mfupi kwa kutegemea aina ya biashara na mahali biashara ilipo,kiwango cha mauzo,muundo wa kiundeshaji,idadi ya wafanyakazi.n.k.Kwa maana hio basi ni muhimu mtu kutambua kwamba unapotaka kuanzisha biashara/kununua/kuuza ni lazima uwe na taarifa sahihi kuhusu soko na biashara husika.

Tujadili leo kwa pamoja juu ya Faida na Hasara za kuuza ama kununua biashara ambayo iko hai na namna bora ya kuweza kupata matokeo mazuri katika ununuaji na uuzaji wa biashara.

Karibuni.
 
Mimi siuzi ila nahitaji watu wa kushirikiana nao kuendesha NGO...ambayo tayari in assets za maana ila wanachama hawako active...kama upo interested uje PM
wanachama wa part-time wanaruhusiwa? Au participation inahitaji full time participation?
 
Back
Top Bottom