Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

mpushi

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
280
76
Loli.jpg

Salam Wakuu,

Ninapenda kujua ni mtaji kiasi gani unaweza kutosha kuanzisha biashara ya kutengeneza na kuuza icecream.

Mchanganuo huo uhusishe gharama za kununua mashine ya utengenezaji, mashine ya kuhifadhia pamoja na mali ghafi.

Asante kwa msaada.

WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUFAHAMU BIASHARA HII
Habarini za muda huu ndugu zangu

Mimi ni ni kijana mwenye umri wa miaka 25, Katika kujikwamua na umasikini na tatizo la ajira Niko na wazo kwa muda mrefu la kuanzisha biashara ya Icecream, nimekuja kwenu kuomba mawazo yenu kwa anaeifahamu biashara hii anipe ufafanuzi kidogo.

Ufafanuzi ninaoomba ni huu;-

i) Changamoto za biashara hii ni zipi
ii) Mtaji wake (malighafi pamoja na mashine vinagharimu kiasi gani)
iii) Kipi kizuri Kati ya kumpa mtu awe anatembeza mtaani kwa kuweka kwenye ndoo kama wanavofanya wengi ama kununua kibaiskeli kama cha Azam
iv) Ili biashara iende ni population ipi niitargert Kati ya wanafunzi wa secondary, primary ama chuoni.

Na mengine niliyosahau unaweza kunisaidia ukawa mzoefu wa hii biashara

Mahali nilipo ni Mwanza , na nimekuja kwenu baada ya kujaribu kufuatilia kwa wanaofanya hii biashara ila ushirikiano wao ulikua ni zero, nilienda pale Salma cone maana ndio sehemu pekee nayoifahamu kwa Mwanza wanaofanya biashara hii.

Nitashukuru Sana kwa atakaenisaidia kwa haya niliyouliza.

Ahasanteni!
Hellow wana JF,

Mimi napenda kuuliza mtaji unaofaa kwa biashara ya kuuza ice cream, naomba mwenye uwelewa anisaidie.

Siku njema wote
Habari zenu! Nauza askirimu hizi za mitaani za watoto (wakubwa pia)

Nina viajana wawili wanatembeza mashuleni.

Nahitaji kukuza biashara yangu napendelea niuze jumla na rejareja pia. Ila changamoto niliyonayo ni machine kwaajili ya kutengenezea hizo askirimu. Kwa sasa natumia impulse sealer. Nahitaji nitengeneze kwa wingi na kwa muda mchache.

Ni mashine gani ambayo naweza kutumia?

Na kingine naombeni ushauri wenu wakitaalam namna ya kufanya biashara ikuwe. Nahitaji mawazo yenu na ushauri wenu!

Ahsanteni
Habarini za muda huu ndugu zangu

Mimi ni ni kijana mwenye umri wa miaka 25, Katika kujikwamua na umasikini na tatizo la ajira Niko na wazo kwa muda mrefu la kuanzisha biashara ya Icecream, nimekuja kwenu kuomba mawazo yenu kwa anaeifahamu biashara hii anipe ufafanuzi kidogo.

Ufafanuzi ninaoomba ni huu;-

i) Changamoto za biashara hii ni zipi

ii) Mtaji wake (malighafi pamoja na mashine vinagharimu kiasi gani)

iii) Kipi kizuri Kati ya kumpa mtu awe anatembeza mtaani kwa kuweka kwenye ndoo kama wanavofanya wengi ama kununua kibaiskeli kama cha Azam

iv) Ili biashara iende ni population ipi niitargert Kati ya wanafunzi wa secondary, primary ama chuoni.

Na mengine niliyosahau unaweza kunisaidia ukawa mzoefu wa hii biashara

Mahali nilipo ni Mwanza , na nimekuja kwenu baada ya kujaribu kufuatilia kwa wanaofanya hii biashara ila ushirikiano wao ulikua ni zero, nilienda pale Salma cone maana ndio sehemu pekee nayoifahamu kwa Mwanza wanaofanya biashara hii.

Nitashukuru Sana kwa atakaenisaidia kwa haya niliyouliza. Ahasanteni!
Habari wana JF,

Mimi naitwa Dennis. Jana nimeanza biashara hii ya aisikrimu za vifuko za shilingi mia mtaani.changamoto niliyoipata ni hii;kuna mteja alivyoanza kuila alilalamika kuwa ni ngumu na anapata shida kuitafuna na akanishauri nitafute ujuzi unaotumika na wengine kutengeneza kwani wapo wanaotengeneza laini kabisa na wakati huohuo zinakuwa zimeganda.

Sasa naomba mwenye ujuzi anisaidie hapa,z8natengenezwaje laini, vitu gani vinawekwa na kwa utaratibu gani.aisikrimu ninazotengeneza ni za ubuyu.

Ahsanteni kwa elimu wakuu

MICHANGO NA MAONI YA WADAU
NAMNA YA KUZITENGENEZA

Hello friends,

Naomba nijibu maswali yenu hapa. Kama nilivosema mwanzo kuna aina nyingi za icecream ila pendwa sana ni za maziwa. Mie hutengeneza za maziwa na za ubuyu, nianze na za maziwa.

MAHITAJI

1. Maziwa ya unga
2. Sukari
3. Maji
4. Ladha (vanila)
5. Rangi ya chakula ( mie hutumia yellow)
6. Kilainishi(optional)
7. Vifungashio

Sasa hapa unakua na vipimo vyako mwenyewe mfano kwa mahitaji ya icecream 70 za maziwa

Maji lita tano( yalochemshwa au weka water guard kurahisisha)

2. Maziwa ya unga robo kilo (tsh 3250)
3. Sukari robo kilo (tsh 650)
4. Ladha ya vanila (tsh1,000) hii utatumia vifuniko viwili tu au vitatu vya kichupa....
5. Kilainishi(tsh 500) kijiko kimoja cha chakula changanya material yako hayo namba moja hadi nne, kisha weka rangi yako (tsh 100 tu) kidogo tu. Baada ya hapo kilainishi unakiweka kwenye blenda unachanganya maji nusu kikombe ule uji wake weka kwenye mchanganyiko wako. Congratulations bidhaa yako ipo tayari funga ktk vifungashio (tsh 500) vyako kisha weka kwa fridge yako tayari kupokea pesa.

Mahitaji 3250+1000+650+500+500+100 =600
Mapato 70@200 =14,000

14,000-6,000= 8,000

Net profit 6,000

Mahitaji kama ladha, rangi, vifungashio na kilainishi utatumia hadi mara 5 bila kununua tena imagn unaweza kuuza icecream 100 tu kwa siku.

100 x200=20,000 kwa siku mara siku 30 sawa na 600,000 kwa mwezi toa gharama za uendeshaji unacheza kwenye laki nne. Fikiria sasa kutanuà soko lako. Ni zaidi ya mshahara wa degree holder.

Ubuyu ndo cheaper zaidi. Oh I love this biz nakushawishi ufikirie. Mkihitaji ya ubuyu nitaelekeza pia.
ZINGATIA SUALA LA ENEO NA MASOKO

Kwa haraka haraka mtu anaweza kukuona kama mjinga au mtu aliyeshindwa maisha lakini una akili sana na inshaalah mungu atakufanyia wepesi. Napenda kukushauri kwenye swala la MARKETING ambapo ukicheza vizuri unaweza kuishi maisha ya kutembelea gari hata kwa hiyo biashara yako ya Ice cream.

Kwenye marketing kuna P's na mojawapo ni Place yaani sehemu ambayo bidhaa inaweza kuuzwa au sehemu ya kufanyia biashara husika. Hapa kwenye place kuna maajabu makubwa sana tena ni miongoni mwa maajabu makubwa sana katika dunia ya biashara, ukiwa mbunifu katika biashara yako hiyo ya ice cream na ukaitumia Place kwa makini nakuhakikishia utakua unakaa na remote mkononi unatizama TV nyumbani halafu hela ya kutosha inaingia kiulaiiiiiiini.

Swala la ugumu au ulaini linatokana na Ratio au wastani wa maji na hicho unachochanganyia kwenye ice cream zako, nakupa ushauri wa sisi magenius kama ifuatavyo; kama unatumia ukwaju nunua kilo moja halafu igawe mara nne yaani uwe na robo nne kila moja uiweke kivyake, halafu baada ya hapo robo moja changanya na maji robo lita, ya pili changanya na maji nusu lita, ya tatu changanya na maji nusu na robo ya lita halafu robo ya mwisho ya ukwaju changanya na lita nzima moja ya maji na ukimaliza kufanya haya gandisha zote kwakuzitenganisha kwa alama ambayo itatofautisha kiwango cha maji ulichoweka.

Baada ya kuganda chukua ice cream moja kila upande ili upime menyewe ugumu na ulaini, nafikiri kwakufanya hivi utapata ice cream laini na ngumu katika hizo ulizozigandisha. Pia katika vipimo hivyo vya maji bila kuongeza wala kupunguza unaweza kuongezea moja katika aina za biskuti zinazouzwa madukani au matunda fulani ambayo hayawezi kuiathiri radha husika unayoitaka kwa kiasi kulingana na bei ambayo unauza hizo ice cream zako.

NB: Kila biashara inaweza kukupatia kipato kizuri katika maisha lakini inategemea unaifanya vipi na katika mazingira yapi.
MBINU YA KUTENGENEZA

MAHITAJI
(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ X 10)
Maji lita 7
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote)
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza)
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)

HATUA:
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu.

Kwa hisani ya Numbisa Jinsi ya kutengeneza barafu za kula, ice crem
NI BIASHARA NYPESI, INAYOLIPA NA INAWEZA KUKUTOA
Je, wajua utengenezaji wa icecream unaweza kubadili maisha yako? Utashangaa right? Ndio ice cream hizi hizi unazozijua za kutengeneza kwa mikono yako. Kutokana na wingi wa vijana wengi kua mtaani na kuwa tegemezi kwa madai kwamba hawana cha kufanya nimeona nifanye ku share hapa.

Ice cream ni biashara nyepesi na yenye pesa ukijua tu jinsi ya kuitengeneza kiutaalam can u imagine 20k a day? Just kwa kuanzia before hujajitanua zaidi? Mimi nimekua nikifanya hii biashara kwa miezi sita sasa kwakweli inanilipa. Kuna ice cream za aina nyingi na cha muhimu zaidi ni package yako, usinielewe vibaya; hapa naongelea "home made " ice cream ambayo nauza moja kwa 200/300, trust me it pays.

Vijana wenzangu tusio na ajira mimi na elimu yangu ya degree nimjasiliamali ambaye nafanya vitu tofauti tofauti vya kujiajiri. Nakushawishi pia uanze kufikiria kujiajiri si lazima uwe na pesa nyingi ndio uanze safari ya ujasiliamali. Ice cream zinahitaji raw material kidogo na nirahisi kupatikana. Let's think out of the box. If you are interested ask me how.
BEI YAKO INATEGEMEA UBUNIFU WAKO

Mahitaji
1. Ubuyu(tsh 2000 kisado)
2. Maji
3. Rangi(tsh100)
4. Ladha(tsh1000)
5. Sukari (tsh1300 nusu)
6. Vifungashio (tsh 500)

Kwa kipimo cha sado moja ya ubuyu utapata icecream nyingi zaidi ndio maana sukari itakua nusu. Sasa hapa ili upate bidhaa nzuri unafanya hivi chukua maji weka kwenye sufuria yenye ukubwa wa kutosha weka ubuyu wako kisha bandika jikoni (ubuyu ukibandikwa jikoni icecream yako itakua haibakizi kile kijiwe cha mwishoni ambacho hakina ladha ila inakua laini kabisa, japo unaweza kuloweka tu bila kuchemsha)

Funika sufuria yako utakua unafunua kukoroga ili ubuyu na mbegu viachane. Ikifikia hatua ubuyu unachemka tayari mbegu na ubuyu wa nje vitakua vimeachana epua subiri vipoe. Sasa chuja mbegu na uji uji wa ubuyu weka uji wako kwenye chombo kingine sasa ongeza maji taratibu huku ukikoroga ili kupata uzito wa uji ubaotaka usiweke maji mengi sana ikawa maji kabisa. Baada ya hapo malizia kuweka sukari, rangi na ladha unayotaka mie hutumia passion. Funga bidhaa yako gandisha, kazi imeisha unasubiri mkwanja tu.

Kwa mnaosema icecrean ni 100 tu, you are very wrong. Hata maandazi kuna jingine huwezi uza zaidi ya 100 lakini andazi hilo hilo duka la pili linauzwa 500. What matters ni ubunifu katika kazi yako; mimi huuza 200 na nikiitwa sehemu napeleka kwa 300.

Pia icecream sio spesho kwa watoto tu. Ukitengeneza vizuri hata watu wazima watanunua tu mbona (ukwaju wa Bakhresa unaliwa na kila rika?) Ile ni icecream tu kama hizi za kawaida sema kaboresha package na ubunifu. Mie siwauzii watoto tu, napata oda hadi za maeneo yenye mikutano japo I'm m still growing. Hivyo, kama unahisi upo kwenye nafasi ya kufanya hii kitu usiichukulie poa its a deal.

Kuhusu fridge, labda niseme hivi: ukiamua kweli kweli na ukiona unaweza kufanya hii kitu basi tafuta hata ki freezer used ufanyie kazi ama kama home kuna fridge basi ifanye iwe ni kama asset sio kuweka nyanya tu. Tuamke vijana wenzangu tusisubiri ajira tufanye yaliyopo kwenye uwezo wetu wakati tunasubiri hayo mambo mengine.
 
Nataka nianzishe biashara ya kuuza icecream kama za bakhresa na juice fresh wadau nani keshawahi kuifanya hii biashara?

Nahitaji nini na nini/vifaa?

Mtaji ni kama shilingi ngapi?

lol:israel:
 
Kiwanda cha kuzalisha ice cream kama za bakhresa ni dola 400,000.

Lambalamba ni laki 4. Hizi za kunyonya kwenye vifuko vya plastic mtaji elfu 40. Wewe unataka kipi fafanua. Mfano Ice cream ngapi per day? ni aina ngapi za ice cream unataka kuzitengeneza? Malighafi zako ni zipi? Distribution network yako. Je, una mtaji kiasi gani? umeipangaje? Please fafanua tukupe majibu unayotaka.
 
Kiwanda cha kuzalisha ice cream kama za bakhresa ni dola 400,000.

Lambalamba ni laki 4. Hizi za kunyonya kwenye vifuko vya plastic mtaji elfu 40. Wewe unataka kipi fafanua..Mfano Ice cream ngapi per day?,ni aina ngapi za ice cream unataka kuzitengeneza?malighafi zako ni zipi? Distribution network yako Je una mtaji kiasi gani? umeipangaje? Please fafanua tukupe majibu unayotaka

Hapo nilipo bold, ndio hela/mtaji alioanzia? Embu changanua, vitu gani vinahitajika vyenye gharama hio. Mtu mwenye mtaji mdogo hawezi kuanza hio business baadae akapanua?
 
sarah6, hongera sana kwa nia yako.

Sijawahi fanya hii biashara ila nimeifikiria sana na bado ipo kwenye mikakati yangu. Nina imani ukiwa na tshs 5m - 10m unaweza kuanza. afrika kusini zipo mashine za ice cream (ukiwa na usd 2500 unawezapata mashine nzuri tu).

Kama mfanya biashara mdogo basi eneo la biashara ni muhimu sana. Ukipata karibu na kituo kikubwa cha mabasi, karibu na shule za sekondari au chuo itakusaidia sana.

Aidha ukifungua hiyo biashara mikoa yenye joto mwaka mzima ni bora kuliko mikoa ambayo kuna miezi kuna baridi kali mfano Mbeya, Arusha, Iringa n.k. (miezi ya baridi utapoteza biashara).

Nakutakia mafanikio mema. mimi nipo njiani.
 
Habari zenu wakuu,

Nilikua naomba msaada wa kununua/upatikanaji wa vitu vifuatavyo:-

1-Guta/Toyo (Honda ya maringi matatu)

BEI GANI: Mpya na Used?

MAHALA: Wapi naweza kuzipata (maduka) katika sehem hizi- Dar na Zenji?

2-Ice cream machine (ya kibiashara) {{km ya apo chini}}

BEI GANI: Mpya na Used?

MAHALA: Wapi naweza kuzipata (maduka) katika sehem hizi- Dar na Zenji?

NB: Kama kuna importers pia sio mbaya

ice cream.jpg
 
Habari wana JF,

Mimi naitwa Dennis. Jana nimeanza biashara hii ya aisikrimu za vifuko za shilingi mia mtaani. Changamoto niliyoipata ni hii; kuna mteja alivyoanza kuila alilalamika kuwa ni ngumu na anapata shida kuitafuna na akanishauri nitafute ujuzi unaotumika na wengine kutengeneza kwani wapo wanaotengeneza laini kabisa na wakati huohuo zinakuwa zimeganda.

Sasa naomba mwenye ujuzi anisaidie hapa, zinatengenezwaje laini, vitu gani vinawekwa na kwa utaratibu gani. Aisikrimu ninazotengeneza ni za ubuyu.

Ahsanteni kwa elimu wakuu
 
Nasikia wanawekaga ngano, ila sina huo utaalam
Wajuzi mjuzeni..

Kaka nashukuru kwa idea nitaifuatilia zaidi ila ukiweza kuja na maelezo ya kina jinsi gani inachanganywa na ice cream ya ubuyu itakuwa msaada mkubwa sana. Nasikia wapemba wataalamu wa hivi vitu ila sina friend mpemba anayefanya hii bness.
 
Please wadau kwawale ambao wameshawahi au wanao fanya biashara ya ice cream za Azam nahitaji kujua taratibu zake namna ya kuwa wakala.

Je, ina faida na ni zipi changamoto zake?
 
Mie nafanya kwa huku kwenye Duka langu.
Nitakupa kwa ninavyojua mie.
Kwanza unaenda kwao wanakupa Bei ya Jumla.
Faida sio kubwa sana ila lazima duka lako liwe na vitu vya ziada na sio kutegemea Ice cream peke yake unless uwe na flow kubwa.

-Fridges:-
Kwanza hakikisha una Fridges zenye uweo mkubwa,chukua kopo la Azam na usome na kujua inatakiwa iwe kwenye Baridi ya degree ngapi.Jaribu kuwauliza wao kuna kipindi walikuwa wanayauza yale ya kwao.Kama upo Dar nasikia bado utaratibu huo upo.Yale yao ni makuubwa sana na ni Heavy duty na pia ni dhamana kwa kazi hii.Ila lazima ununue na bei yake sio ya kitoto.Milioni na kitu kama sikosei.

Angalizo,Ice cream zina contents ambazo zinafanya usichanganye na kitu chochote katika uhifadhi,kuwa makini sana na hili.Huwa hazipendi kabisa kuwekwa ndani na kitu kingine,la sivyo utaona kila kitu kina ganda ila zenyewe hazigandi,fundi atakula hela hapo mpaka basi.So,Fridge ukiweka Ice cream zile basi weka zenyewe tu au pamoja na chockstik.Na umeme ukikatika muda mfupi tu basi zinayeyuka kulingana na vitu vingine vilivyomo humo.
Kama utakosa kwao basi nakushauri nunu Fridge Jipya kwa ajili ya Ice cream.
-Umeme
Umeme ukikatika,hapa itabidi iwe tatizo sana,hasa kwenye baadhi ya bidhaa,sasa lazima uwe mjanja kwenye upangaji wake,ili usiwe unalifungua muda muda mrefu kutafuta size ya Ice cream anayoitaka mteja,maana hewa ya nje ni ya mvuke wa joto,sasa hufanya kuyeyuka haraka sana pindi umeme ukiwa hakuna.Lakini ukipanga vizuri itakusaidi kwamba kama umeme haupo basi unafungua tu na ku pick anachotaka mteja.Tatizo kubwa ni pale itakapofika masaa kuanzi 6 - 8 bila umeme ndio issue.Hasa kwenye chocksick.
-Bidhaa:
Mbali na Ice ceam jaribu pia kuuza chockstik kwa jina maarufu,huwa zinatoka vizuri kwenye biashara,mie kwangu ndio zinaoongoza kwenye mauzo,maana nipo karibu na shule International School

Nikikumbuka jingine nitakuja.Ila kwa ufupi ukipata sehem nzui ni biashara nzuri.
Mie nimeweka,Ice cream,chockstic,nauza Fruits,Juices,Coffee maana nina coffee maker,na pia Maji.Na Vitafunwa mbalimbali.
Na katika vitafunwaa mbalimbali imenifanya nipate mpaka order za maharusi mbali mbali na shughuli mbali mbali,yaani bila kutarajia nayo imekuwa biashara kubwa.Mfano upande wa orders nyingi ni Sambusa,Katless,chapati za maziwa,bagia,Cakes nk,na pia huwa baadhi ya siku navamia dayoutings za watu na kuwashauri niwafanyie picnic lunches,maana biashara nyingine lazima ujifanye hamnazo ili yako yaende.
Ni biashara nzui,zingatia sana usafi.
Mie mwakani natarajia kufungua kama hii huko Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom