Biashara ya kusafirisha Dagaa kutoka Mwanza kuja Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Biashara ya kusafirisha Dagaa kutoka Mwanza kuja Dar

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Papizo, Jul 3, 2012.

 1. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,463
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wakuu nimesikia watu wanatengeneza hela kwa kufanya hii biashara, so nadhani na mimi nilikua nataka kujua deep zaidi inakuwaje hasa advantages and Disadvantages?? kwanza kabisa najuwa humu ndani wazoefu na kuna watu wa kila aina so sidhani kama itakuwa vibaya tukishauriana wakuu.

  1)Kwanza kabisa kiasi ambacho unaweza kuanzia kwa biashara kama hii kuanzia milioni ngapi ambapo utanunua mzigo wa kutosha??

  2)Sehemu ya kuuzia zikitoka Mwanza na kufika Dar, Je sehemu zipo ambapo zinaweza kuuzikana kwa ujumla I mean Soko???

  3)Je kuna faida gani na hasara gani katika kuzisafirisha na njia ipi ya usafiri ni njia nzuri zaidi

  Wakuu kwa haraka haraka nadhani hayo ni ya muhimu kwa sasa nadhani itakuwa vizuri zaidi wengine kama watakuja na idea au maswali mengine na tukapata majibu zaidi.

  Nawakilisha
   
 2. A

  Andre02150 JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Biashara ya dagaa inahitaji umakini mkubwa sana. Usipokuwa mwangalifu, kuna uwezekano mkubwa sana wa pesa zako (mtaji) kuuacha Mwanza! Madalali wa kuuza dagaa Mwanza sio waaminifu. Kwanza wanachakachua uzito wa kilo za dagaa kwa kuchanganya michanga. Vilevile soko lake huku Dar lina-fluctuate sana. Bei ya kilo ya dagaa inabadilika mara mbili au tatu ndani ya wiki moja. Hivyo ushauri wangu wa bure: tafuta biashara nyingine ya kufanya kuliko kuingia hasara kwenye dagaa. Unaweza kuni-inbox if u need more clarification....
  --dagaa mza zinanuliwa SOKO LA MWALONI, KIRUMBA
  --dagaa dar zinauzwa K'koo na ktk masoko mengineyo jijini japo madalali ndio wamekamata soko
  --endapo ni dagaa kwa ajili ya chakula cha kuku, wasiliana na FALCON, maeneo ya Tegeta; falcon ndio wasindikaji wakuu wa chakula cha kuku hapa Dar.

  Goodluck!
   
 3. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,463
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nashukuru sana mkuu wangu kwa msaada wako na mawazo yako mazuri na ya maana, yeah nitakucheck tuongee vizuri zaidi kaka wala hamna tatizo kabisaa.
   
 4. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama uko na mawazo ya kufanya biashara ni bora ukaifanya wala mtu asikuogopeshe na ww ukaacha kufanya mjasiliamali hatakiwi kuogopa kufanya kitu cha kufanya ni kuangalia hizo risks alizozisema mdau hapo juu kuna kipindi kama mwezi umepita,nilitembelea Kilosa nikataka kwenda porini hivyo ikanipasa kununua baadhi ya vyakula pale mjin,nilistaajabu kukuta bei ya kilo moja ya dagaa iko sawa na kilo moja ya nyama kwa Dar kwa huko nyama iko chini kidogo zaidi ya dagaa hao wa Mwz hivyo inaonekana soko lake ni zuri sehemu hizo ingawa sikufanya utafiti wa kutosha sana ila nilizunguka sokoni na nikakuta bei iko juu zaidi ya nyama hivyo kama kweli uko tayari unaweza ukafanya utafiti wako katika hiyo biashara ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko maeneo hayo sio kila bidhaa lazima iende k/koo mdau hata maeneo mengine kuna masoko mazuri tu cha msingi ni ujasiri na kutokata tamaa
   
 5. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,463
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Asante sana mkuu wangu na nashukuru sana kwa mawazo yako na kuwa open zaidi, yeah ni kweli kabisa na wala hujakosea biashara ni ujasiri na kuwaa na nia na kiu ambacho unataka kufanya ndio muhimu zaidi, so yes nitafatilia zaidi hizo sehemu, je una hint ya sehemu zingine uziweke hapa wazi mkuu?Pamoja sana
   
Loading...