Biashara ya kupangisha nyumba na fremu ni utajiri mkubwa watu wengi hawapendi kuwafumbua wenzao

Hakuna biashara kichaa kama ya kupangisha labda uwe na fremu Kariakoo. Real Estate kwenye nchi zetu hizi ni biashara isiyo na faida labda industry i satulate baada ya majiji kujaa.

Ukienda Mbeya watu wanajenga kwenye Mlima Kawetere...Ukija Dar watu wanajenga Pugu na Bagamoyo na Kibaha nk nk nani atapangisha jengo lako la thamani kwa bei itakayokulipa hizo ni dhahania na most of us uwezo wetu ni kujenga pembezoni kabisa na city center ambako thamani ya rental iko chini sana.

Nenda kawaulize walioacha nyumba zao Mbweni na Bunju Beach kwenda kazini Dodoma majumba ya nguvu waliyojenga kwa gharama kubwa wanapangisha kwa Laki 4 ...

Bora kuwekeza kwenye Bonds na Transportation siyo real estate huyo NHC tu mwenyewe anahaha...waulize mifuko ya hifadhi na maghorofa yao utapata jibu
Walau umesema ukweli kwanza kabisa ili ujenge fremu za kupangisha 500,000 na ziwe kumi na upate wateja wote kwa mkupuo huo uwekezaji wake si chini ya milioni 100...ila mzee kwenye transportation nako si mchezo..biashara ya kupangisha utaiona inafaida kama umerithi jengo...
 
ili kuweza kulipwa kodi ya 500000k /month hiyo nyumba iwe mbezi beach, Goba maeneo ya barabarani au karibu na barabara. na nyumba ya kodi hiyo unaongelea kuanzia 100mil kuijenga....otherwise umhamishe mtu mahala kwenye prime location weka kuanzia 300mil and up...

Huko chocho ndani ndani kodi huwa 30k mpaka 50k..
Kuna mtu namjua yeye alienda kujenga apartmnt gorofa turiani
Jamaa alizika zaidi ya 200 hko
Waisting huo alikuwa na uwezo wa kuzijenga goba, kimara
Nahs wakati mwingine wenge linachsngia

Ova
 
hapana sio connection .fanya wewe kama wewe .hizi connection zinakuja zenyewe ukijaribu.

Mwaka 2000 watu walinunua sana maeneo mikocheni kipindi hiko shamba kabisa.na mmoja ni ndugu yangu .kwa sasa hiyo mikocheni utagusa na kila mwaka kodi yake inazidi kupanda
Kama ulivyosema sasa hivi unakaa nje ya mji kwaio kwa mtazamo wako una majuto na unajutia fursa ambazo unaona wengine waliziona...
 
Hivi kwanini hawajengi? Je kuna mtu anafahamu chanzo cha hiyo ishu?
Siku hizi wanajenga au kununua nyumba zamani walikua wanaogopa serikali unajua hawa watu huwa wanaishi kiujanja ujanja na madili haramu mengi kwahiyo wanakaa mguu mmoja ndani mwengine nje lakini siku hizi hata huko nje mambo yamebadilika hawana namna.
 
Ukijenga nyumba faida yake ni baada ya miaka 10-15. Hapo uombe Mungu uwe hai. Hailipi hii biashara bora hata ukapande miti ya mbao
Uzuri humu hatufahamiani ila wapi tunaofahamiana moja kwa moja, wewe mfanya biashara ila hauna upembuzi na jinsi unavyoandika hapa "Huakika" wala sina haja ya kuendelea kukuelezea maana upeo wako uko hivyo.


Angalieni familia za kiarabu na asia wanawekeza kwenye nini kwa sana na wanavyofanya kama mtakuta wengi wanamiliki real estate au wanafanya vitu gani kwa sana.

Njoo utembelee machimboni uone milioni 10 ikifeli pesa ndogo inazalisha milioni 30_50 hii ni ndani ya wiki tatu tuu au mwezi mmoja sasa hapo utalinganisha na flat ngapi au hizi nyumba zako ngapi?.
 
Pesa ya kuwekeza kwenye nyumba za kupangisga uzuri akiozi mfano umeweka milioni 40 na kuendelea.sio kama ni biashara itakufa yani ni mtaji wa maisha .sasa chukua hiyo pesa kafanyie biashara unayo fahamu wewe kama ujaja kufa kwa presha
Milioni 40 prime areas hata kiwanja hupati. Sasa hivi ukitaka kuwekeza sinza lazima umuondoe mtu sio chini ya milioni 200. Bado hujajenga hapo
 
Nna kiwanja nilinunuaga ununio mwaka 2008 kwa Tsh milion 20, nimejenga nyumba kwa ghalama ya milioni 65, nakula Kodi laki nane kwa mwezi, upande vyumba vitatu sebule ,jiko, public toilet, master, Kodi Laki nne, na upande mwingine hivyo hivyo,kwenye kiwanja kimoja, mageti tofauti yakuingilia,

Na ujenzi huwa nakaba Hadi penati, kuanzia mbao kila kitu nanunua mwenyewe,fundi Hana nafasi ya kuiba,

Kuna sehemu pia nimejenga chumba Master, sebule, jiko, public toilet, Kodi Laki mbili, kwenye eneo moja zipo tatu, na Kuna room moja Ina master na jiko, nakula Laki na 30,

Kuna sehemu mapinga kwa kibosha pia, sema kule Kodi zake hovyo,

Bibie nyumba zinalipa Sana tu,Kuna umri ukifika utajua hilo
Kiwanja cha milioni 20 mwaka 2008 sasa hivi thamani yake ikoje? Hiyo kodi ya laki 8 ulianza kuipata mwaka 2008/2009?
 
Biashara ya kupangisha frame na Nyumba ni biashara ya vilaza, Siwezi zika 100m (Thamani ya Eneo pamoja na gharama za Ujenzi) Kwa laki 5 kwa mwezi.

Nina msela wangu katumia gharama karibu ya 25 m Kujenga frame kwenye nyumba yake ambazo kwa sasa kila mlango unamuingizia elfu 80 kwa mwezi. Yani Milango yote hata Laki 5 hapati. Sahivi analia anatufuta mtaji wa Biashara, Nilimuonya sana ila alijiona ana maarifa. Jamaa ni hopeless kabisa.
 
Afadhali na wewe umesema hivi angalia jinsi kuna jamaa nilikueleza kwamba biashara hii inawafaa wasio na mawazo na upembuzi wa biashara.
 
kuna jamaa alinunua nyumb ya matope milion 20. akavunja akajenga frame 5. gharama za ujenzi wa hizo frame milion 15 akapangisha wapangaji wakawa wanamlipa kodi elf 50 kwa frame. kwa mwezi ni laki 2 na nusu kwa mwaka ni milion 3. gaharama za kiwanja na ujenzi milion 35 yeye kipato kwa mwaka milion 3. Hii ni biashara kichaa kabisa
Kwa upepo wa biashara ulivyo, pamoja na utovu wa elimu ya biashara, huyo jamaa yako yupo "njema" kwa kupata hata hicho kidogo kidogo pole pole!

Kuna watu wamewekeza mitaji mikubwa zaidi ya huo lakini matokeo yake wameangukia pua, nikimaanisha wamefirisika mazima, aidha kwa kutokuwa na elimu ya biashara ama kuanzisha biashara kwa kufuata mkumbo.
 
Epuka matapeli biashara ya kupanga nyumba na fremu hailipi kabisa labda uwe na bahati ya eneo. Mtu unajenga nyumba/fremu kwa miaka 5 kwa kujibanabana na mikopo na ukitafuta gharama ni zaidi ya 70m halafu unapangisha kwa laki tano . Majumba ya kupanga mengi ni tupu baada ya mabosi wenye pesa zao kwenda Dodoma. Hakuna wapangaji. Mara wapangaji wagome kulipa kodi. Labda useme biashara ya kujenga nyumba na kuuza au kujenga nyumba ya kuombea mkopo benki



Haya masuala ya kujenga nyumba bila malengo inabidi tuwe na mjadala wa kitaifa.
! Kwa uandishi wako nimeishia kucheka tu.
 
Hapo kionda morogoa mwak 2010 kuna mzeealistaafu zake Happ idara ya umwagiliaji kweli kapa hela zake Safi na kununua cruzer la kizamani na kaujenga fremu 12 Happ kionda don Bosco hapo mpka leo Hakuna fremu iliyokaliwa mtu akija anatak hat sehemu ya kuzugia bas anataka kwa elf 20. Mzee kachanganyikiwa na mpk sas ameenda kutafuta kazi dodoma ili kujikimu mnk hkn return aliyoiona. Hasara Sana ikiwa utajenga sehemu za ajabu fremu
 
Hapo kionda morogoa mwak 2010 kuna mzeealistaafu zake Happ idara ya umwagiliaji kweli kapa hela zake Safi na kununua cruzer la kizamani na kaujenga fremu 12 Happ kionda don Bosco hapo mpka leo Hakuna fremu iliyokaliwa mtu akija anatak hat sehemu ya kuzugia bas anataka kwa elf 20. Mzee kachanganyikiwa na mpk sas ameenda kutafuta kazi dodoma ili kujikimu mnk hkn return aliyoiona. Hasara Sana ikiwa utajenga sehemu za ajabu fremu
Goroko

Jeshi langu nakukubali sana dingi ila mwandiko wako ni wakibabe mnooo
 
Back
Top Bottom