kanyagio
JF-Expert Member
- Dec 10, 2009
- 1,021
- 365
ndugu zanguni, nimekaa nimefikiria kuhusu uanzishaji wa ka-biashara ka kukodisha Party and wedding tents pamoja na viti (kwa ajili ya harusi, sherehe nyingine, misiba, mikutano etc).. Lengo ni kuwa na tents size (ya kukaa watu kama 20-50) na size kubwa (watu 300-400). Tents hizi nimejaribu kuperuzi mitandao nikaona unaweza kuyaagiza toka CHINA.. na wameshaonyesha nia ya ku-supply.. gharama ya tents zinatofautiana ila nimeona moja 18x30m ambalo gharama inaenda mpaka 10,000 USD FOB (hapo hujaweka usafirishaji na insurance na kodi). Ila kuna supplier ambaye anauza 30USD per sq. meter na kaniambia ukitaka kujua watakaa wangapi inabidi uchukulie kuwa kila mtu anachukua nafasi ya 1.5 sq meter.
sasa wanajamii naomba msaada wenu katika masuala haya:
sasa wanajamii naomba msaada wenu katika masuala haya:
- Je biashara hii inaweza kulipa hapa dar es salaam? je mikoani
- Je ni ndiyo, je tents zinazoweza kupata wateja je ni zile kubwa (yaani ya >550 Sq M) au yale madogo madogo ya watu kama 20-50
- Je kuna watengenezaji hapa Tanzania? Contacts? gharama zake
- Competitors hapa ni akina nani zaidi ya "Maezeki"
- je location nzuri ya kufungua ofisi itakuwa wapi- kurahisisha upatikanaji wa wateja
- taarifa nyinginezo